SoC02 Jifunze kukumbuka, lazima utasahau

SoC02 Jifunze kukumbuka, lazima utasahau

Stories of Change - 2022 Competition

tujuemoja

Member
Joined
Jul 26, 2022
Posts
7
Reaction score
2
"Watu wengi wakimaliza vyuo wanakwenda mtaani mahali ambapo kuna malengo yao, yanawasubiri Lakini hakuna anayejua kama ndio malengo yake"

Mitazamo na mifumo yetu ya elimu, imewapa giza vijana, Wamekuwa wakiamini na kuaminishwa Shuleni ndio mahali pekee na bora katika kufanikiwa kimaisha huku wakiwafunga kutambua na kugundua fursa zingine nje ya elimu.

Akili haipatikani kwa kwenda shuleni tu kila siku, bali kwa kutambua na kupambanua kitu ambacho unaweza kufanya na ukafurahia na kikakuletea kipato.

Siku zote Elimu isiyo na msaada ni mzigo kwa Mwanafunzi mwelewa,

Dunia yetu imejaa matajiri na wafanyabiashara wakubwa ambao hualikwa kutunuku Vyeti wasomi wakubwa duniani, lakini sio kuwaalika kwenda kusoma darasani.

Usiwe na akili mgando kuamini kufikia mafanikio ni kupita njia moja tu ya elimu, kumbuka kuna njia sahihi na uhakika kwa kila mtu sahihi, tumia akili kutambua.

Siku zote kila mtu ni bora katika eneo ambalo ameliamini na kuwekeza kwalo, Wengine ni bora katika ufugaji, ukulima, uvuvi, ulinzi n.k

Kufanikiwa katika kila lengo ikiwemo hata lengo la elimu kunategemeana na shabaha ulioielekeza kwayo.

Shabaha ni (nguvu, jitihada, Uvumilivu, Rasilimali, Muda, Mawazo) uliojikita kuwekeza kwenye lengo lako.

Shabaha ni Kukataa kuvutiwa na fursa au lengo lolote lile ambalo halipelekani na maono yako.

Shabaha ni Kuchagua Mwelekeo unaouamini ni sahihi, bila kutamani Mwelekeo mwingine mzuri japokuwa sio sahihi kwako kwa wakati huo.

MALENGO NI MKE.
"Siku zote ni vigumu sana kwa mwanaume Rijali(mwenye akili timamu) kukubali kuchaguliwa mke, maana anaweza asimfae maishani mwake)

Mke hachaguliwi kama nguo za mitumba sokoni, bali akili hutoa vigezo na masharti yampasayo njiwa (mwanamke) kabla hujafanya Maamuzi ya kufungiwa nira naye.

Ndivyo yalivyo malengo huwezi kuchaguliwa maana wewe ndiye unayetamua nini unapenda na mahali gani au njia gani unaweza ukapita hadi kufikia malengo yako tu huku jamii, rafiki, wazazi wakikuongoza tu kukufahamisha njia mbalimbali ambazo hutumiwa kufikia malengo.

Cha ajabu mara kadhaa wanafunzi wamekuwa wakipangia kwenda kusomea vitu ambavyo sio ndoto kwao hata kama wakalala hawawezi kuziota ndoto hizo.

Imani yangu inanituma kuamini kwamba kutumikia lengo la elimu kama sio ndoto yako ni sawa na kuchepuka kwenye ndoa yako. Jambo ambalo ni baya na litakugharimu namna ya kurudi kuwaelewesha mkeo nyumbani ulikuwa wapi jana usiku mpaka uje leo nyumbani, yaani mkeo ni sawa na malengo yako.

Baada ya kumaliza chuo ndipo watu hutumia akili kutambua na kugundua malengo yao, huku wakiwa na huzuni pamoja na hasira kwa kupoteza muda kwenye elimu ni ufunguo wa maisha kumbe sio ufunguo wa maisha upo mtaani ukiwasubiri wamalinze kurandaranda mashuleni.

Asili ya mtu haijifichi ni sawa na kusema malengo ya mtu ayajajificha sema tu haja amua kuyatafuta maana hayana notisi wala mitahara kama ilivyo shuleni.

ZIFUATAZO NI FAIDA ZA KUDUMU KWA MKE MMOJA(MALENGO YAKO) PASIPO KUCHEPUKA.

01.ANAKUPA KASI YA KUYAFIKIA MATOKEO AU MATUNDA YAKO KWA HARAKA.

Hii ni kwa sababu ya kuachana na kurandaranda kwenye Malengo ambayo sio yako. Hivyo kwa kuelekeza akili, nguvu, mali na Rasilimali zote kwenye hilo lengo, linakutunuku stahashahada mapema na kwa wakati.

02.ANAKUJENGEA JINA NA KUKUHESHIMISHA.
Malengo pekee ndio hukufanya utambulike katika dunia ya sasa. Tunaweza sahau majina yako tukakukumbuka kwa kile unachokifanya na tukakuita kwacho. Mfano, Mama maboga, Mama Ntilie, Dereva Boda, Barafu, Mboga nk.

03.ANAKUPUNGUZIA MAJUTO.
Kutumikia malengo ambayo sio yako ni sawa na kuhesabu pesa ambazo hazikuhusu.
Hii ni kwa sababu unautumia muda mwingi kumtumikia kitu ambacho hukipendi na huna imani nacho kama kitakupa hata ajira.

MAWIFI NA MASHEMEJI WAKUANAO MAKINI KATIKA MKEO(MALENGO YAKO)

01.WATU WEMA NA WAZURI LAKINI SIO SAHIHI KWAKO KWA WAKATI WAKO WA SASA.

Ni kweli sio maadui zako na mnashirikiana vizuri katika maisha, lakini mnatofautiana katika malengo mliojiwekea.
Mtu kuwa adui wa malengo yako sio lazima akuchukie au aonyeshe hali yakutokukupenda, la hasha, ni kushindwa kuwa ndege wawili wenye mabawa sawa kuruka pamoja.
Pia kuna marafiki amabao wanataka utumiki maono yao tu na huku ukisahau ya kwako kuwa nao makini sana.

02.MAAMUZI YASIYO SAHIHI.
Kugundua ndoto yako ni vita kubwa sana ni sawa na kukosea kuoa, kwa sababu itakutengenezea maisha ya majuto mpaka unaingia kaburini.
Maamuzi sahihi hutegemeana na taarifa sahihi katika kitu unachotamani kufanya, na zinaweza zikawa taarifa za jumla au taarifa maalumu.

Mfano:"CHANGAMKIENI FURSA MATIKITI NI DIRI KIPINDI HIKI". hiyo ni taarifa ya jumla tu kutoka katika vyombo vya Habari, Hivyo ili kurihakiki wazo hilo unapaswa kukutana na watu husika ambao hujikita katika mambo hao ya matikiti.

Pia, maamuzi sahihi utegemeana na ujuzi wako ulionao. Kitu ambacho unaona kwa kweli nikifanya nafanya vizuri bila kigugumizi na moyo umeridhika kufanya hicho kitu. Kwa kufanya hivyo Utazeeka uzee mwema.

03.KUPAMBANA NA AMBAYE APAMBANI NA WEWE.
Mitazamo yetu imetawaliwa na ubinafsi, kitu kinachopelekea kutokubali mwenzio afanikiwe kabla yako.
Siku zote Jifunze kupambana na wewe mwenyewe, yule wa jana.
Riziki ni kama hajali, hata huchukie mwenzako asipate muda ukifika atapata tu. Ndio stahili yake.

HITIMISHO
Lengo la kuandika maudhui haya ni kufungua vichwa vya vijana wenzangu kuhusiana na mfumo halisi wa maisha kwa sasa, ambao ukitegemea kwenda kukariri shuleni na uje kufanya mtaani unakuferisha.
Ukifika mtaani kubali kujifunza, kubali kukosolewa na kubali kubadilika.
#KuwaTaswira ambayo ni fumbo kwao #

Mwandaaji :-
©tujuemoja
(David Malunda)
MWANAFUNZI CHUO CHA RUCU
 
Upvote 0
Back
Top Bottom