Jifunze kumpa mwanamke wako hela bila sababu, utanishukuru baadaye

Jifunze kumpa mwanamke wako hela bila sababu, utanishukuru baadaye

Halali nyie wanawake muwe matajiri pamoja nawewe mleta uzi

Tukiwa watano ,tukimtumia kwasiku ,unaenda kununua boti ya uvuvi na chenji inabaki
 
Mtoa mada usikute anakaa kwa Shemeji yake na hapa kaagizwa akalete karanga mbichi na shemeji yake ili amshughulikie vilivyo dada ake.

Nirudi ktk Mada.

Kutuma tuma hela kipumbavu unamjenga Mwanamke wako kuwa Mpumbavu na Mtegemezi.

Mama ako au Baba ako uliwahi kumtumia hela bila kuomba mara kwa mara kama unavyowatumia hao Malaya?

Binafsi natuma hela ila yenye maelezo yanayoeleweka yaani hela nitatuma ila uje na hoja za msingi na si vinginevyo, unaweza kuomba laki 3 kama hoja yako ni nzito utatumiwa hata laki 5.
Wewe mpe hela bwana!! Acha porojo nyingi😂
 
Hivi mwanaume akiamua kumpa pesa mwanamke wake tena anayotafuta kwa jasho lake shida huwa ni nini mbona watu wako na makasiriko sana? Ambae unaona huwezi kutoa pesa usitoe hamna sheria unavunja, hamna dhambi unatenda ila usishangae wanaume wengine kuwapa pesa wanawake zao kila mtu anatumia pesa zake namna anavyotaka.
Yaani ni ajabu, yamewatoka kweli😂😂😂
 
Huu uzi una watu wake, wanajulikana, lazima wawepo ili kuusherehesha, wakikosekana hao huu uzi ni batili. Ngoja nianze comment moja moja.
😂😂😂😂 kwendaaaaa!
 
Hivi mwanaume akiamua kumpa pesa mwanamke wake tena anayotafuta kwa jasho lake shida huwa ni nini mbona watu wako na makasiriko sana? Ambae unaona huwezi kutoa pesa usitoe hamna sheria unavunja, hamna dhambi unatenda ila usishangae wanaume wengine kuwapa pesa wanawake zao kila mtu anatumia pesa zake namna anavyotaka.
Tusamehe dada ni makasiriko tu ya kukosa hela. Imagine mwezi mzima sijashika laki halafu naona mtu anahonga laki mbili lazima nishangae.
 
Tusamehe dada ni makasiriko tu ya kukosa hela. Imagine mwezi mzima sijashika laki halafu naona mtu anahonga laki mbili lazima nishangae.
Uchoyo hata haukupendezi😂
 
Hayo ni madhara ya kuvutia bangi chooni unakua na mawazo ya mavi mavi tuu upuuzi mtupu 🚮🚮
 
Tusamehe dada ni makasiriko tu ya kukosa hela. Imagine mwezi mzima sijashika laki halafu naona mtu anahonga laki mbili lazima nishangae.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kindly refer to the heading above..

Na hii sio mwanamke wako tu, hata yule ambaye unamtaka. Kwa mfano; [emoji116]

Money transfer successful! TSH 200,000.00 was sent to NMB Bank account no 41510040XXX (MILLICENT MZURI) ref:XXX4298373. Thanks for using Exim Mobile, call 0800 780 111 for any assistance needed.

Au,

AirtelMoney
Umetuma Tsh270,000.00 kwenda kwa MILLICENT MZURI. Salio lako jipya ni Tsh2,100,000.00. Muamala No: CI240503.1856.N57337

Hiyo miamala yote uwe umemtumia hata bila kuombwa. Kwa mfano huo muamala wa kwanza unakuwa umeutuma jana usiku wa saa saba wakati amelala, akiamka asubuhi anakutana na notification tu. Aisee, mapenzi utayasimulia katika muktadha wa tofauti sana.

Pengine huo muamala wa pili uwe umemtumia leo week end baada ya binti kukwambia anaenda kwenye birthday ya rafiki yake. Halafu muamala unafuatiwa na SMS hii, "baby pls manage that little token from me. Love always" [emoji4] .

Hawa wanawake tunawalaumu bure tu. Tatizo ni kwamba hatuwapi PESA. Kwao pesa ndio kila kitu; nguvu za kiume, uaminifu, utulivu, upole, utu wema, usikivu, unyenyekevu n.k (mengine ongezea mwenyewe).

Sasa wewe hela hutumi, binti anajikaza anakuomba unaanza stori, sijui "ooh baby nipo mbali msibani huku tandahimba ndanindani nina cash tu na mawakala wako mbali" [emoji23], wakati siku hizi kuna sim banking, mobile money transfer n.k

Hata kama huna sim banking, mwanaume unakosaje akiba kidogo kwenye simu kwa ajili ya dharura?!!! Kwanza siku hizi kutembea na cash ni ushamba.

Wanaume tutafuteni pesa. Dunia haina huruma kwa masikini wote lakini hasa sisi WANAUME.

N:B
'MILLICENT MZURI' NI JINA LA KUSADIKIKA TU.
Kwa hiyo hizo Pesa tunakwenda kuziokota halafu tunawatumia tu wake zetu?
Tulichawahi kuwatumia hizo pesa mama zetu?
 
Back
Top Bottom