Jifunze kumuacha aende

Jifunze kumuacha aende

muache aende ,asee ni ngumu balaa co rahc kama neno lilivy as me no yake nimefuta ila kichwan ipo nateseka hapa nimekuwa mfungwa
 
mimi siwezi kuacha aiseee eti nimuache aende labda aniache yeye niende
haha kumbe hujaelewa je mfano ww dem anazngua kila cku ata ujitume vp yy hatunz kumbu kumbu anasahau huyo ni wa kumuacha aende
 
nilimuacha aende baadae akarudi,nikamsamehe.
leo ameniacha niende na mimi nimeenda
kama mm sema nimeenda kroho upand nataman ata anipigie cm japo hajatulia sema itakuwa umackin umechangia na mm baada ya hapo nimeelimika cingii in relation kama cna hela watajaninyang'anya tonge tena
 
haha kumbe hujaelewa je mfano ww dem anazngua kila cku ata ujitume vp yy hatunz kumbu kumbu anasahau huyo ni wa kumuacha aende
wewe ndio ujaelewa....mimi sijui kuacha mpaka niachwe mimi
 
• Kamwe usihisi kama ulimwengu ndio unakaribia mwisho pale akupendae anapokuacha.

MUACHE AENDE !

• Kujaribu kumlazimisha mtu akupende ni sawa na kujaribu kumlazimisha Nguruwe kutambua usafi na uzuri. Usimlazimishe akupende, mwache mwenyewe akupende, kama hakupendi...

MWACHE AENDE !

• Wewe ni wa thamani mno kulilia penzi. Mtu ambae anakupenda kweli atakuheshimu na hataku 'treat' kama uchafu. Kama atakuchukulia wewe kama uchafu...

MUACHE AENDE !

• Usipoteze muda wako wa thamani kujaribu kumshawishi au kuomba mapenzi. Mtu mwingine pembeni anakupenda wewe kwa dhati, ila wewe uko busy mno kumuogesha nguruwe! Kwanini?

MUACHE AENDE !

• Usikasirike pale mtu wako anapompenda mwingine tofauti na wewe. Siku zote hua ni vigumu kumshawishi NYANI kwamba Asali ni tamu kuliko ndizi...

MUACHE AENDE !

• Mwanamke/mwanaume yeyote anaekuchukulia kirahisi siku zote atachukulia faida kwako, atakugeuza atakavyo kama chapati akijua hufurukuti, yeye sio Mungu wa kukufanya atakavyo...

MUACHE AENDE !

• Kuna watu hawatakupenda hata kama utajitoa kiasi gani kwao. Ni sawa tu. Kukukataa kwao haimaanishi kwamba una kitu kibaya, bali ni maana kwamba hawako kwa ajili yako. Usilazimishe duara kuwa pembe tatu...

MUACHE AENDE !

CHA KUJIFUNZA

• Hauwezi badilisha maoni mabaya ya watu juu yako, ila unaweza ukazuia maoni yao mabaya yasikubadilishe wewe kama wewe!

• Acha kichwa chako kiongoze moyo wako kukuondoa katika mahusiano sumu. Lengo la mahusiano sio kuleta mafadhaiko ila ni kuongeza furaha juu ya ile uliyokuwa nayo mwanzoni ulipokuwa haupo ktk mahusiano.

Jifunze kumuacha aende hata ni kama kwenye ndoa, vitabu vya dini vinaruhusu kabisa kuvunja ndoa kwa kesi ya Uzinzi.

NI NGUMU SANA ILA KWA MUSTAKABALI WA FURAHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE ME NAKWAMBIA MUACHE AENDE MPE NA NAULI KABISA!

Kama ipo ipo tu...!

Tupo pamoja??
Nirahisi kusema ila kutekeleza hilo jambo nichangamoto esp. unapompenda mtu kwa dhati
 
Ni bora kumwacha aende maana maisha ni mafupi kutwa nzima kulalamika unaumizwa muda wakutabasamu na kufurahi ni mchache kuliko wa kuumia na kulia
Huna appriciation hakuna zuri amabalo umeona umefanyiwa kila siku ni lawama na kusemea maneno ya hovyo
kutwa kujisifu kuwa hapa huchomoi kwakuwa wajiona ni mzuri na bora kisa wanawake wanakulilia nje
kwako kila siku ni kuna vitu vya wanawake mara kanga,mtandio shower cap,ky jelly ukiulizwa wajibu jeuri
majibu ni yamkato na ya hovyo mtu bado yupo na wewe
ukiambiwa 'Ilove you ,I miss you unaguna na kusema makubwa ,ukipigiwa simu sentensi ya kwanza ni unasemaje , matusi na maneno ya shombo ni kawaida kwako kuyatoa .
OOOGH!Nenda baba nendaaaaa
 
Back
Top Bottom