Jifunze kutengeneza mafuta ya kujaza ndevu

Jifunze kutengeneza mafuta ya kujaza ndevu

Mi nafikiri utafute mafuta ya kujaza ela.Tujaze ndevu zitupe kazi ya kunyoa tena?
Hata sijaelewa watu wanafuga Kuku, mbuzi , ng'ombe wengine wantaka kufuga NDEVU? Haiingii akilini kweli familia , mke na watoto watalindwa kwa Ndevu?

Haya endeleeni na hiyo makitu
 
Ngoja namm naamini nikimalza darasa la saba namimi zitaota ntafanyia kaz huu uzi
 
Swali je naweza kutumia kwa nywele?
Weka mawasiliano coz hizo complications siyo kila mtu ana muda na vifaa vyakufanya hivyo
 
Habari zenu wapendwa? Naamini wote mko poa.

yna2 leo nimeamua kuwaletea somo la namna ya kutengeneza mafuta ya kujaza ndefu kwa wanaume (natural beard balm).Mafuta haya siyo kwamba yatajaza ndevu tu ila yanatafanya ndevu na mn'garo,kuondoa mfungamano,na kuondoa m'ba.

MAHITAJI

beeswax (sega la nyuki) 1tbsp

-kazi yake ni kufanya mafuta yetu yagande na vilevile inasaidia kufanya nywele in'gae.

Shearbutter 1tbsp
-inauwezo wa kujaza nywele na kuipa ulaini na mn'gao.

Coconut oil 2tbsp
-kazi yake kujaza nywele na kuondoa ukavu kwenye ngozi na kuifanya nywele in'gae (nakushauri tumia mafuta ya Nazi yasiyopikwa)

Sweetalmond oil 2tbsp
-kazi yake kuzuia nywele isikatike,kuipa nywele mn'gao,na kuijaza.

Lavender essential oil 10drops
-kazi yake kuondoa matatizo ya ngozi Kama m'ba..fangasi kwenye ngozi..kuzuia nywele kukatika na kujaza nywele.

Rosemary essential oil 5drops

-kazi yake ni kuifanya nywele kua nzito..ndefu.. kupunguza wingi wa mafuta..kuipa nywele ulaini na mn'gao.

JINSI YA KUTENGENEZA

weka sufuria jikoni ..weka maji yachemke ..chukua sufuria nyingine au bakuli la udongo weka beeswax na shearbutter..chukua bakuli lako/sufuria weka juu ya sufuria lenye maji huku ukikoroga taratibu hadi iyeyuke.

Kwanini tunayeyusha butter na beeswax juu ya sufuria nyingine badala ya kuiweka sufuria moja kwa moja kwenye Moto? Tunafanya hivi sababu ya kuepuka kuua vitamini zilizomo kwenye butter na beeswax.

Butter na beeswax vikiwa vimeyeyuka weka mafuta yaliyosalia isipokua essential oils..koroga Kisha ipua.

Acha yapoe kidogo weka essential oils..koroga vizuri Kisha weka kwenye vikopo tayari kwa kuuza/kutumia.

Nb: ukikosa Sweet Almond oil tumia castor oil sio yale ya rangi nyeusi.

Ahsanteni.

Moderators naomba msiuamishe huu uzi tafadhali.

Mchana mwema.

View attachment 1250851View attachment 1250853View attachment 1250854
Kutengeneza wengine hatuwezi, nikitaka kununua iliyo tayari bei gani na zinapatikana wapi?
 
Back
Top Bottom