Kawaida yangu ni kuingiza watu chaka Lady (kwa maono yako)
Yes According to me ni
kilaza mzuri tu,otherwise awe ni mtu mwenye biashara nyingi nyingi na sio awe anategemea hiyo biashara ya kuvizia wateja wa msimu.
Kuna wafanyabiashara wenye biashara nyingi (wapo imara tayari) hawa sina shida nao kwasababu hawategemei income ya sehemu 1,wafanyabiashara hawa hawawezi kuacha fursa impite,hawa hawaoni shida kuzunguka hata nchi nzima wakitafuta fursa ya kile wanachokifanya.
Mfano no.1
Harmonize (konde boy mgahawa)
View attachment 1609380
Huyu ni mfanyabiashara mkubwa lakini angekua mdogo kwa biashara anayofanya tungemuita (BABA NTILIE),huyu hana shida ya mtaji my dear,huyu haungi ungi,yuko njema. Anazunguka na gari anatoa huduma.
Mfano.no 2
Biashara za Minadani
sijui kama umeshawahi kwenda mnadani lakini kama tayari utakubaliana namimi kule si wote ni wafanyabiashara wadogo unga unga mwana,kule kuna wafanyabiashara wenye capital nzito wanaenda minadani,anavyoenda mnadani sio kwamba hiyo ndio biashara anayoitegemea na kama ujuavyo minada haikai sehemu 1 leo iko hapa kesho iko pale lakini kote huko utawakuta hawa ma giants wapo minadani.
Jiulize je hao machinga wadogo,mama ntilie wadogo wadogo stand zikibomolewa au zikihamishwa huwa wanakuaga ktk hali gani? waulize machinga waliojengewa Machinga complex walipofukuzwa barabarani waende kwenye lile jengo nini kiliwakuta?
Uliza wale waliowekewa X frem kisha wakahama hizo frem za barabarani walipohamia frem zingine biashara zao zilikua ktk hali gani? kusanya data za hao watu kisha rudi soma tena Comment yako ulionijibu kisha utaniambia kati ya
mimi au
wewe nani anataka kuingiza wenzake chaka.
Suala la kukimbizana na Fursa linakuja baada ya kusimama na kuimarika ktk biashara yako,hao kina harmonize,kina Bakhressa,kina MO,na wengineo Walijiiimarisha wao kiuchumi kwanza kisha ndio wakaanza kukimbizana na fursa zinazokuja mbele yao.
Una ka biashara kamoja hako kabiashara ndio unakatagemea kakulishe kakuweke mjini kakusomeshee watoto halafu una risk eti unaenda kukaweka pembeni ya Kusanyiko la watu ambalo muda na siku yyte lile kusanyiko litapotea,haupo serious dear.
Sina shida na mtu anaefanya kazi posta yeye kama anaona eneo lake linamfaa na idadi hiyo ya wateja inamtosha ni
vizuri tu kila mtu aangalie upande wake,wewe kama hutaki wateja 24/7 na unaridhika na wateja wa 12/5 ni
vizuri kabisa yani tena vizuri kwasababu malengo yangu na yako yametofautiana,sijui plan zako kwa miaka miwili ijayo na wala hujui plan zangu kwa miaka miwili ijayo kwahyo ishu ni kila mtu aangalie TARGETS zake.
Kama huijui uliza uambiwe ila usiseme
"biashara gani"! biashara za ku run 24hrs zipo kibao kasumba ya watu kufunga biashara saa 12 jioni hadi 6 usiku maduka yamefungwa ni kutokana na tamaduni za kivivu watu walizokuzwa nazo tangu utotoni.
kama hadi leo hujawahi ona mahali popote bango limeandika
Service 24 hours na bado unadiriki uliza eti ni Biashara Gani ya kufanya 24 hrs Utakua haupo serious na swali lako.
Atleast umemaliza vizuri na hiyo Line.
Namalizia kwa kusema TENGENEZA WATEJA WAKO MWENYEWE uwe na uhakika na kesho yako,kuna watu ofisi wanafungua saa 6 mchana wanafunga saa 1 usiku,hao watu usiwaige wana wateja zao Permanent wapo pale,wewe jifanye unakimbizana na fursa wakati corona imekuja mwezi tu Vilio kila kona na hapo hatujapigwa Lockdown,tungepigwa je si ndio makamasi yangewatoka watu?
Jifunze kutengeneza wateja na usiingize watu Chaka Asante kwa challenge ya comment yako inayotaka ingiza wengine CHAKA.