Jifunze kutumia troubleshooting tool iliyomo kwenye OS ya PC yako kutatua matatizo ya PC yako kabla ujamwona fundi maana akina fundi Michael ni wengi

mathsjery

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Posts
2,249
Reaction score
1,813
NOTE:
Ninaposema troubleshooting tool maana yake ni tool inayoweza kukusaidia kujua na kutatua tatizo lolote kwenye PC.

sifundishi ila najaribu kukufumbua macho ukae ukifahamu kuwa hauitaji knowledge kubwa kutatua matatizo madogo madogo ndani ya PC yako.

Kumbuka kila kifaa kimeundwa na mfumo wake unavitu vidogo vidogo vinavyoendesha icho kifaa, sasa wamekiambia kifaa kwa kutumia lugha ya kifaa hicho kuwa kama kukitokea tatizo flani basi tatizo hilo litawakilishwa kwa code number flani.

Hivyo hivyo mtumiaji wa kifaa hicho ameundiwa software inayoweza msaidia kutatua tatizo la kifaa hicho bila kujua maana nzima ya code number flani, hapa namaanisha kuwa software hiyo ndiyo itatambua maana ya error code flani na kutatua au kupendekeza solution.

Sasa turudi hapa kwenye PC,
Watu wengi wamekuwa waking'ang'ana na google sio mbaya ila inamajibu mengi ya kila mtu ya uongo yamo, ya kweli yamo na vuguvugu yamo.

Sasa kama hauna knowledge utachagua na kuchagua, kujaribu na kujaribu lakini mwisho wa siku unaamua kutumia muda na nguvu nyingi kumbe ungemtumia fundi aliyemo kwenye PC yako ungemaliza mapematatizo lako.

Haujawahi kuta PC ina tatizo labda la network au graphic driver n.k, ukaamua kudownload software unayoamini itatarua tatizo na mwisho wake ulipoteza muda na mb au gb kadhaa?. Je, unaona sio tatizo?

Mwingine anapiga window kumbe tatizo RAM imakaa vibaya huoni kuwa unasumbumbuka na kupoteza vitu muhimu.

mfano: pc inakuambia error code flani pale unapofungua software flani baada ya kuinstall. tumia troubleshooting tool kucheck kama software hiyo ina match na OS yako kabla hauja unstall na kuinstall tena. Kumbuka software zingine zinachukua muda kuwa installed na kuwa uninstalled. Je, huoni hasara hapo?

mfano: pc haitaki kuunganishwa na wifi na wewe naye unaenda karuta au k'koo au unaanza tafuta driver na kila unayopakua inakataa kisa wifi na wakati unaweza kutumia troubleshooting tool kwa ajili ya network problem kwenye hiyo pc kwanini usianze na hiyo. Cheki mb zimeshapotea.

kuna wakati mwingine mambo mengine ni setting tu za PC wala sio driver n.k.

Mifano ni mingi acha nikomee hapa.
Troubleshooting tool ni built in software kwa window os, cheki kwenye pc yako pale kwenye window icon au alama ya window kisha search "Troubleshooting" hii ni software inayobeba diagnostic tools kadhaa, kwa hiyo unaweza click tool flani ili kukusaidia kutatua tatizo flani.

mfano ukiifungua hiyo software utakuta tool inaitwa "programs" hii itakusaidia kucheki problem zinazohusiana na program/software related issues na zingine ziko pale kama "hardware and sound" na "network and internet" na "system and security"
 
Hebu fafanua mkuu hiyo "window icon" naipataje? fafanua kama upo na begginers sio advanced mkuu. Mimi binafsi PC yangu imepoteza internet kabisa baada ya kufanya setting kwenye BIOS. Ukinisaidia nitashukuru
 
Hebu fafanua mkuu hiyo "window icon" naipataje? fafanua kama upo na begginers sio advanced mkuu. Mimi binafsi PC yangu imepoteza internet kabisa baada ya kufanya setting kwenye BIOS. Ukinisaidia nitashukuru


Itumie hiyo troubleshooting and tool kudetect na kufix hiyo issue.
 
Ebu ngoja nifike hom nijaribu kuifanyia makeke pc yng mana ukibonyeza kitufe cha wireless Wi-Fi inaunga fresh ila Bluetooth inakataa kabisa yn sijawahi kufanikiwa kuunga Bluetooth toka nimeinunua hii pc nishenda kwa mtalamu mmoja ivi lkn nae akachemka
 
Jaribu
 
Me machine yangu ukiwasha inapiga fen kwakasi af baada yamuda inajizima ishuikoje apoo
 
Me machine yangu ukiwasha inapiga fen kwakasi af baada yamuda inajizima ishuikoje apoo
Vitu vinavyofanya deni izunguke na pc kuzima ni vingi lakini vifuatavyo ndoa chanzo kikubwa.

CPU kuchemka au kufeli kwa RAM,

Kabla haujafikia na cpu just badili RAM au ichomoe RAM Kisha irudushie kama pc ina slot mbili za RAM iweke kule ambako hakukuwa kutumika hakikisha kabla haujafanya hivyo pc iwe imezimwa na battery liwe limechomolewa.
Kisha utarudishwa then jaribu kuwasha tena.


Kama haujafanikiwa fungua pc safisha vumbi mpaka kwenye deni na yale matundu ya kutolea hewa, ukimaliza funga kisha washabiki pc.

Ikishindikana ninja ramadhani mpya nafikiri ni zinauzwa kwa 40elfu hapo tatizo linatoweka.
 
kicha cha mada ni tofauti kabisa na maelezo kweli umetuweza... mi nikajua unaelezea namna ya kutumia troubleshooting kugundua tatizo kwenye PC ile imekuwa tofauti huu uzi ni [emoji706]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kicha cha mada ni tofauti kabisa na maelezo kweli umetuweza... mi nikajua unaelezea namna ya kutumia troubleshooting kugundua tatizo kwenye PC ile imekuwa tofauti huu uzi ni [emoji706]

Sent using Jamii Forums mobile app
Una haki ya kusikilizwa na kupendwa pia, ila punguza dharau mkuu, naomba utoe hiyo ndoo ya uchafu, uwezi kutupa Hii thread humo.

Hauna shukurani. Aiseh
 
mathsjery
nipo nna swali ila halihusiani na hii maada.


Hiv unaweza kutumia simu as a server?

Una haki ya kusikilizwa na kupendwa pia, ila punguza dharau mkuu, naomba utoe hiyo ndoo ya uchafu, uwezi kutupa Hii thread humo.

Hauna shukurani. Aiseh
 
mathsjery
nipo nna swali ila halihusiani na hii maada.


Hiv unaweza kutumia simu as a server?
Kama unamaanisha server kwa ajili ya kudevelop website kwa php, ndio ipo na inafanya kazi fresh, labda sijakusoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…