Jifunze kwa wengine waliofanikiwa nawe utatoboa kimaisha

Jifunze kwa wengine waliofanikiwa nawe utatoboa kimaisha

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,753
Reaction score
9,575
Habarini wadau wangu,

Natumai mko vyema na mnaendelea na majukumu yenu ya kutafuta ugali wa kila siku.

Ni bora leo tukaongelea jambo hususani lenye kuleta tija katika mstakabari wa maisha yetu. Je, kwanini unasema maisha yamekuwa magumu, vitu vimepanda kama ndege angani ilahali bado uko vilevile haujapanda kama hivyo bidhaa?

Angalia Je ni sehemu au ni mahali gani wewe upo kwa sasa na je hatua gani unaichukua ili kutoka hapo ulipo sasa? Je umeshafanikiwa kwa sehemu fulani katika yale malengo yako uliyopanga kwa mwaka huu? Je ulianzia wapi na unaendelea wapi? Je, umeweka jedwali au umelist yale malengo, miopango yako na je umeshajisemea moyoni kuwa nitaanza na hili na kumaliza na lile?

Je, umeshaona wengine walivyotoboa au toka mahali walipokuwa mwanzo na je umekwenda kujifunza kwao? au umeshachukua hatua gani kuwakabili ili ujifunze kwa yale ambayo wameshapitia wao? Bado muda ungalipo ni vyema kujifunza kwa wale waliiopanda juu sasa ili kuapnda juu pasipo kulalalma kuwa maisha magumu ilihali hatua haujachukua kutoka hapo?

Waweza kujiuliza ni sababu zipi zakufanya usitoboe? Au kutoka ama kuanzisha kitu ambacho kikapanda nawe ukaona nuru au mafanikio kwa hicho?

TUANGALIE SABABU ZA MKWAMO HUO
A) Kuchukualia mambo kiuwepesi ndiko kunafanya ubaki vilevile ulivyo na usipande juu
B) Kuona muda bado unakusubiri wewe
C) Kudhani kuwa uliumbwa kwenye hali hiyo bila wewe kuchukua hatua ya kutoka hapo ulipo
D) kuwa na mawazo mgando kila mara
E) Kuona kuwa yupo mtu atakutoa bila wewe kujisumbukia kung'ang'ana kutoka hapo

Ukiwaza vya juu na kutaka kujifunza kitu utatoboa ila ukitaka uwe mwenye usingizi na kulala na tu utaweza kuona mstakabali wako.

Mithali 19:15-29 " Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa. Yeye aihifadhiye amri huihifadhi nafsi yake; Bali yeye asiyeziangalia njia zake atakuwa juu".

Ni vyema kujifunza kwa wengine waliotangulia nakwenda kujua walitokaje na kuwa juu katika kazi, biashara zao na utavuka tu.

ACHA NISEME KUWA PAMBANA, TAFUTA NA TIA BIDIII NA JUHUDI KWA YALE UYAFANYAYO UTAVUKA TU NA KUPANDA JUU.

Wasalaamu
LADYF

CC: Kilimbatzz , Half american , Demi , Mwifwa , Asprin , Bosco Henry, mpwayungu village

Karibuni wadau nipigieni kura sasa sijui ndo utaratibu huu hahaaa.
 
habarini wadau wangu

Natumai mko vyema na mnaendelea na majukumu yenu ya kutafuta ugali wa kila siku
Kufanikiwa kuna makandokando mengi, ikiwemo bahati, kuabudu shettani na mengine kama hayo.
utajifunza hadi uzeeke na hayo mafanikio utakuwa unayasikia tu amini usiamini.
 
Mungu Fundi haswaa...tena si wa kimchezo mchezo na katuzidi sana sisi Binadamu kwa akili na maarifa.

Kiukweli pesa tunatafuta sana maana ndiyo maisha hayo, ila kuhusu mafanikio kimaendeleo ni kitu kingine kabisa ukilinganisha na juhudi tunazotumia, na ndipo naelewa nyimbo za;

1. Christina Shusho - Ni kwa neema tu.

2. Edson - Ni kwa neema tu na rehema.

Maisha hayana kanuni kabisa, yani utapambana sana usiku na mchana ukizingatia mashauri mbali mbali tena ukiambatanisha na kanuni za Entrepreneurship, Accounts, Marketing, Economy pamoja na Watu waliokuzidi maendeleo isipokuwa pasipokuwa na baraka zake Mungu ni sawa tu na kuufukuza upepo.

SULUHISHO:

Jitahidi uwe unatoa zaka na sadaka inavyopasa.

Tenda mema kadri unavyoweza maana dunia ni Watu na huzunguka.
 
kufanikiwa kuna makandokando mengi, ikiwemo bahati, kuabudu shettani na mengine kama hayo.
utajifunza hadi uzeeke na hayo mafanikio utakuwa unayasikia tu
amini usiamini
Ni kweli usemayo ila jifunze kwa wale ambao ni wa muhimu sana
 
Back
Top Bottom