Jifunze mapishi na namna mbalimbali za kupika mkate


Mhh...
 

Umenikumbusha mbali sana, bi mkubwa alikuwa akiupika huu lakini yeye akitumia unga wa dona tu na tuliuita MKATE WA DONA. Miye hupenda lile tandu (sijui kama ni sahihi kuliita hivyo kama la wali) lake la juu hasa.
Asanteee...upishi mpya huu ntajaribu in shaa Allah
 

Upo huu hupikwa kwa sembe tupu. Hua unakorogwa tu km uji na tui la nazi na ingredients zengingine ukishakua mzito huokwa.
 
Mrs kharusy na ule unasongwa si mkate wa sembe pia? Nliwahi kumuona mama akimpikia wifi yangu alikua mjamzito aliutamani ila ni mtamu sana unakua kama brown hivi.

Huu unausema ww jaan ndo wenyewe haswaa unawekwa hadi mdalasini...very tasty hauchanganywi na ngano huwa..
 
Je, badala ya kuweka sembe, ukaweka dona inakuwaje? Mimi naupa jina 'mugate' kwa maana ya mchanganyiko wa mkate na ugali ambavyo ni ingredients kuu (50% each).
 
Je, badala ya kuweka sembe, ukaweka dona inakuwaje? Mimi naupa jina 'mugate' kwa maana ya mchanganyiko wa mkate na ugali ambavyo ni ingredients kuu (50% each).

Jaribu tu mkuu halafu utuletee mrejesho
 
upo huu hupikwa kwa sembe tupu. Hua unakorogwa tu km uji na tui la nazi na ingredients zengingine ukishakua mzito huokwa.
basi mie nlokuwa naujua ni huu. Na sukari yake huunguzwa kama ya puding. Unakolezwa na spices. Mkate nlikuwa naupenda huu. Kwa wiki lazima niupate mara 3 au hata 4 kula.
 

Hiyo ni cake au mkate? wingi wa sukari na mayai unaondosha hilo jina na hivyo kuwa keki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…