Jifunze mapishi na namna mbalimbali za kupika mkate

Jifunze mapishi na namna mbalimbali za kupika mkate

mmh! sasa napata idea hapa, sijui tufanyeje ila da AshaDii tusaidiane naomba iwe hawa wote tutakao wapa kama professional cooks wawe wanatufundisha jinsi ya kupika mapish mageni wazo liwe hivi Madame B Thanda hawa ni professional cooks sasa tuongeze na wengine watupe ujuzi zaid sie tufuatilie recipes tu halafu siku tutaalikana wote ambao ni memba wa jukwaa tuje na pishi ambalo tumejifunza ili tuonje je tunasoma kweli ama la??

Poa mamito.
 
hivi umeisoma vzr post yangu?? kila mmoja niametoa kile ambacho nilona ni anakipenda mbona hujacomment kwa lara 1 na Ciello nilivyowaambia kwenye post husika?? ama kwa King'asti?? sasa wewe ndo unaifanya kuwa bulling but nimetumia kama joke na kama nilivyofanya kwa wengine.

Girls!!! Tuendeleeni kupika jamani...mambo mengine madogo sana kuyakuza..kaa kimya mamushka uepushe shari...wakati mwingine kupuuzia ni dawa tosha
 
Last edited by a moderator:
haya jamani leo ni siku nyingine ambayo ninataka tupike mkate kwaajili ya familia.
mkate

mkate ni chakula ambacho huliwa wakati wa kufungua kinywa.hupikwa kwa kutumia unga wa ngano ama wa muhogo lakin huwa na kiasi kukubwa cha wanga na hivyo unapotumiwa kama kifungua kinywa hukusudiwa kumpatia mlaji nguvu na joto mwilini.

sasa tuangalie jinsi ya upish wa mkate.

mahaitaji:
a) unga wa ngano kg 1 (kwa familia yenye watu wengi let say 4)
b)hamira gm 50
c)mayai 4
d) chumvi kijiko kimoja cha chai
e)sukari nijiko 2 vya chakula
f) maziwa fresh robo l500 ml kama unauwezo kama la basi tumia maji.

njia.

1) chekecha unga wa ngano kwenye chekeche ili kuondoa particles kubwa pamoja na kuingiza hewa ndani ya chembe za unga.

2) weka hamira chumvi pamoja na suukari kisha koroga kwa mkono hadi uchanganyike vizuri kabisa.

3) koroga mayai yako 4 pembeni kwenye bakuli kisha mimina koroga yachanganyike ndipo uyamimine kwenye mchanganyiko wako uyachanganye kwa mikono.

4) tia maziwa kwenye mchanganyiko wako na kisha ukande unga kwa vidole vyako hadi ulainike uwe kama wa kupikia chapati. hakikisha wakat unaukanda usizidishe maji manake kadiri unga unavyozidi kuumuka ndivyo unavyozidi kuwa laini. wakati wa kukanda kunja vidole vyako vinne na uvitumie kukandia unga usitoboe unga kwa vidole kwani hautaukanda zaidi ya kuutoa hewa tu.

5) chukua chombo chako cha kukokea kipake blue band kwa ndani kisha kata unga kwa size ya chombo chako na uutengeneze kwa umbo la tin yako ndipo uuweke. kama huna baking tins za mkate waweza kutumia hata tin ya cake ila uzikate kwa maumbo ya mstatili. kama nacho hiki huna basi tumia sufuria yako ipake blue band ukate unga kwa umbo la viduara uueke ndani visiwe vikubwa sana yawe na umbo dogo la wastani tu.

6) washa oven yako kwa nyuzi joto 120 dk kabla, kisha weka chombo chako cha kuokea na funga mlango. subiria baada ya dk 30 mkate wako utakuwa umesha iva. ii kujua kama umeiva vizuri chukua kitu chenye ncha kali choma kwenye mkate basi kile chombo kikitoka kikavu jua mkate wako uko tayari.

zima jiko na toa mkate wako nje uweke pakavu ili upoe. kumbuka kwamba mkate kwa ajili ya afya hufaa uliwe siku moja baada ya kuokwa. hapa ahauwa na ladha nzuri zaid na huwa umesha lainika vya kutosha. usiufunike mkate wako kama bado haujapoa usije ukajaa mvuke. na usiuweke kwenye unyevu.
mkate huu waweza kuutumia kutengenezea sand wich ama kuliwa jinsi ulivyo tu.

haya basi nawatakieni mapish mazuri kwaajili ya sikukuu ya x-mass na mwaka mmpya.

mke mwezangu AshaDii nakuomba uwaekee ile picha ya mkate tunayopikaga nyumbani kwajili ya chai

hapo kwenye rangi mkuu hiyo si lita moja na nusu kweli au sijaelewa vizuri.. gfsonwin
 
Last edited by a moderator:
nitaoka mkate wa sikukuu mchana wa leo. sasa ngoja nifanye mapema nikuletee wa moto uone jinsi ulivyo mtamu.
mie na AshaDii tumeolewa na Kaizer.hatuolewi tena kwani mwanamke hanaga mitala.

Afadahali niletee ukiwa moto kabla Kaizer hajarudi toka Nyumba ndogo. Mi nashauri mngekuja huku kwangu. I am like King Mswati II the only difference mimi natoa full services kama zinavyotakiwa. Najua wewe na AshaDii won't regret. Mpango wangu nifikishe walau wake 10. Sasa hivi wako 8 na majina yao nitakwambia siku nyingine. Picha yao ya maandalizi ya kunipokea leo jioni wamenitumia sasa hivi, hii hapa:

Basketball-Wives-season-4-cast-20111.jpg
 
Last edited by a moderator:
Alafu nimeona hapo juu Superman anataka kuleta posa... Utanipa feedback umeamua vipi! Maana kama wewe unaondoka hata mimi nitaondoka, siwezi tena maisha bila uke wenza... :becky:

Usisahau kumkaribisha na chai yetu ile ya special recipe kunywea huu mkate wako mtamu.. Lol.

milk_tea.jpg
AshaDii wewe pekee ndo unanielewa. Hebu Mwambie Teacher gfsonwin mje naye basi. Njooni na huo mkate na chai ya hiriki na mdarasini. Hebu njoo kwanza my dear, are u ok?

superman-2.jpg
 
Last edited by a moderator:
Mmh? Upendeleo na ubaguzi huu sasa.....

BTW unaifanyia promo Blue Band au? Nikitumia Tan Bond au siagi nyingine mkate utageuka kitumbua au?

Huku Torabora Blue Band haifiki, tutakoma tunaopenda mkate.

Babu Asprin unalalamika Upendeleo na Ubaguzi kwani na wewe unataka?
 
Last edited by a moderator:
nimemkatalia mie nishazoea maisha yetu pamoja sasa ta utengano siyawezi kabisa.

You are inside the baloon. Come outside and see life. Njooni wote na utagundua maisha ni mazuri na matamu zaidi ya ulivyozoea. Masharti na vigezo kuzingatiwa.
 
Mdogo wangu gfsonwin hivi hewa inasaidia nini kwenye mikate na chapati??

hewa katika mapsh yyte yale hasa ya kukanda ni muhimu sana. sasa nataka nikurudishe kwenye shule ndogo ya food&microbiology, hewa husaidia kazi ya kuumuka. and they are responsible for the break within the loaf.
 
Alafu nimeona hapo juu Superman anataka kuleta posa... Utanipa feedback umeamua vipi! Maana kama wewe unaondoka hata mimi nitaondoka, siwezi tena maisha bila uke wenza... :becky:

Usisahau kumkaribisha na chai yetu ile ya special recipe kunywea huu mkate wako mtamu.. Lol.


milk_tea.jpg
Nakuombea uachike ili nikuoe mimi.kwa mavitu haya hata siwezi kukubali.niruhusu nianze kuleta posa
 
Last edited by a moderator:
Nakuombea uachike ili nikuoe mimi.kwa mavitu haya hata siwezi kukubali.niruhusu nianze kuleta posa
hahahah! mnamwonea Kaizer wivu siyo?? mwenzenu huwa anafaidi zaid ya haya. hivi unajua sasa hivi anaandaliwa x-mass cake mwenzenu.
 
Last edited by a moderator:
You are inside the baloon. Come outside and see life. Njooni wote na utagundua maisha ni mazuri na matamu zaidi ya ulivyozoea. Masharti na vigezo kuzingatiwa.

hahahah@ Superman bana unajua kumtoa nyoka pangoni kweli yaaani unachonga mashairi mazuri ili tu tujitose kwako sio?? ila sie Kaizer anatupa kila tukitakacho jamani lol!
 
Last edited by a moderator:
jamani hivi wadada wote wa humu jamvini sio wapish?? mbona jukwaa halina watu hili?? wakati nilijua ndo sehem ya kwanza watu wote kuingia lol!

sasa mie naanza kuwavuta mmoja baada ya mwingine hadi mje mpike mkate khaa1
haya Smile, Preta, Kongosho amu ( ooh wewe unaumwa pole mwaya), King'asti tena wewe unapendeleaga sana kula sandwich njoo hapa folen za shop rite zipungue, Zion Daughter, Ciello, lara 1 sio kila siki nyie na mmu tu hao washefa mtawapikia nn ama ndo kuwalisha junky foods za migahawani?? snowhite sio wewe na miiko tu njoo ujfunze mapish mapya aatii cacico sio kila siku folen city bakery njoo ujifunze hapa upike mwenyewe, Paloma, BADILI TABIA Juliana Shonza sio unakalia majungua tu njoo ujifunze kupika. na wengine woote njooni

tueni mwanamke anasifiwa mapish na usafi toopppppppppp!

wataka mkate upi mwali wangu!
mie ninao wa karanga
kuna wa zabibu kavu
kuna wa asali kati kati
kuna wa jam
kuna wa hiliki
kun awa chumvi
kuna mkate bubu
kuna mkate wa skonzi!
nambie tu wataka nikuandalie mkate upi kungwi wangu!
 
wataka mkate upi mwali wangu!
mie ninao wa karanga
kuna wa zabibu kavu
kuna wa asali kati kati
kuna wa jam
kuna wa hiliki
kun awa chumvi
kuna mkate bubu
kuna mkate wa skonzi!
nambie tu wataka nikuandalie mkate upi kungwi wangu!

mie nimepika mkate wa kawaida si umeuona hapo baaada ya kuuandaa??
kesho uekee recipe ya mkate wa karanga niliula kwa mtu ulikuwa mtanu kweli mwali.
 
gfsonwin, asante kwa recipe sijawahi pika mkate wa mayai, nitajaribu nione unakuwaje
 
Back
Top Bottom