gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,272
- 20,692
Haya jamani leo ni siku nyingine ambayo ninataka tupike mkate kwaajili ya familia.
Mkate ni chakula ambacho huliwa wakati wa kufungua kinywa.hupikwa kwa kutumia unga wa ngano ama wa muhogo lakin huwa na kiasi kukubwa cha wanga na hivyo unapotumiwa kama kifungua kinywa hukusudiwa kumpatia mlaji nguvu na joto mwilini.
Sasa tuangalie jinsi ya upishi wa mkate.
Mahitaji:
a) unga wa ngano kg 1 (kwa familia yenye watu wengi let say 4)
b)hamira gm 50
c)mayai 4
d) chumvi kijiko kimoja cha chai
e)sukari nijiko 2 vya chakula
f) maziwa fresh robo l500 ml kama unauwezo kama la basi tumia maji.
Namna ya kupika
1) chekecha unga wa ngano kwenye chekeche ili kuondoa particles kubwa pamoja na kuingiza hewa ndani ya chembe za unga.
2) weka hamira chumvi pamoja na suukari kisha koroga kwa mkono hadi uchanganyike vizuri kabisa.
3) koroga mayai yako 4 pembeni kwenye bakuli kisha mimina koroga yachanganyike ndipo uyamimine kwenye mchanganyiko wako uyachanganye kwa mikono.
4) Weka maziwa kwenye mchanganyiko wako na kisha ukande unga kwa vidole vyako hadi ulainike uwe kama wa kupikia chapati. hakikisha wakat unaukanda usizidishe maji manake kadiri unga unavyozidi kuumuka ndivyo unavyozidi kuwa laini. wakati wa kukanda kunja vidole vyako vinne na uvitumie kukandia unga usitoboe unga kwa vidole kwani hautaukanda zaidi ya kuutoa hewa tu.
5) Chukua chombo chako cha kukokea kipake blue band kwa ndani kisha kata unga kwa size ya chombo chako na uutengeneze kwa umbo la tin yako ndipo uuweke. kama huna baking tins za mkate waweza kutumia hata tin ya cake ila uzikate kwa maumbo ya mstatili. kama nacho hiki huna basi tumia sufuria yako ipake blue band ukate unga kwa umbo la viduara uueke ndani visiwe vikubwa sana yawe na umbo dogo la wastani tu.
6) Washa oven yako kwa nyuzi joto 120 dk kabla, kisha weka chombo chako cha kuokea na funga mlango. subiria baada ya dk 30 mkate wako utakuwa umesha iva. ii kujua kama umeiva vizuri chukua kitu chenye ncha kali choma kwenye mkate basi kile chombo kikitoka kikavu jua mkate wako uko tayari.
Zima jiko na toa mkate wako nje uweke pakavu ili upoe. kumbuka kwamba mkate kwa ajili ya afya hufaa uliwe siku moja baada ya kuokwa. hapa ahauwa na ladha nzuri zaid na huwa umesha lainika vya kutosha. usiufunike mkate wako kama bado haujapoa usije ukajaa mvuke. na usiuweke kwenye unyevu.
mkate huu waweza kuutumia kutengenezea sand wich ama kuliwa jinsi ulivyo tu.
haya basi nawatakieni mapish mazuri kwa ajili ya sikukuu ya x-mass na mwaka mpya.
mke mwezangu AshaDii nakuomba uwaekee ile picha ya mkate tunayopikaga nyumbani kwajili ya chai
==================
Kutoka kwa Mdau
==================
"Chibudee
MKATE WA MAYAI
Vipimo
Mayai 4
Sukari ¼ Kikombe
Unga wa Ngano Vijiko 5 ½ vya chakula
Hiliki ya kusaga ½ kijiko cha chai
Baking powder ½ Kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Chukua bakuli la kiasi, weka sukari, iliki na vunja YAI MOJA BAADA YA JENGINE KWENYE KIBAKULI KANDO NDIPOSA UMIMINE KWENYE BAKULI KUBWA LA SUKARI
2. Changanya sukari, iliki na mayai kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cake mixer), mpaka sukari ivurugike yote na kuumuka.
3. Washa jiko lako (oven) 350F lianze kupata moto au makaa..kwa watumiao makaa…
4. Weka baking powder kwenye unga na uanze kuuchanganya kidogo kidogo kwenye mchanganyiko wa mayai na sukari.
5. Hakikisha kila ukiweka unga kidogo unauchanganya vyema usiwe na madonge. Na kupunguza madonge..chunga unga wako kwa tungio…
6. Mimina unga ndani ya sufuria ya kuchomea keki ya kiasi.
7. waweza kuweka karatasi kwa ndani ya sufuria umbo la mduara au kama ni baking tray umbo la mraba kwa kuipakia mafuta ili mkate usishike unapotaka utoa baadae.
8. Ingiza sufuria ndani ya jiko (oven) na oka kwa dakika 20 au 30 vile vile makaa ya chini yawe kiasi tu kuliko ya juu ya mfiniko.
9. Uhakikishe mkate wako kama umeiva kwa kijiti cha kuchomea mshikaki au toothpick. Ingiza kijiti katikati ya mkate kisha kitoe na ukiguse uangalie kama kikavu mkate umeiva kama bado kuna ubichi basi rudisha mkate kwa dakika 5 nyingine kisha ukague.
10. Wacha mkate upoe kisha utoe ndani ya sufuria na uweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.
=====================================
=================================
==========================================
==========================================
=================================
=====================================
Threads nyingine zinazohusu ujuzi na utaalamu wa mapishi mbalimbali ya mkate.....
1. Mkate wa ufuta
2. Mkate Wa Sinia - Mkate Wa Kumimina Aina Ya Kwanza
3. Naan bread
4. Jinsi ya kupika mkate wa haba soda

Habari za jioni wapendwa. Za masiku kadhaa?
Leo tunapika mkate wa unga wa sembe
Mahitaji:
Unga sembe glass 1
Unga ngano glass 1
Sukari glass 1 (unaweza kupunguza kidogo)
Maziwa glass 1
Mafuta 1/2 glass
Mayai 4
Iliki iliosagwa 2tbs
Bp 2tbs
Jinsi ya kupika:
Saga sukari yako uweke kwenye bakuli safi pamoja na mayai. Tumia mashine ya cake kusagia hadi ifure/ivimbe.
Weka mafuta saga, weka maziwa saga, weka unga wa ngano na bp(bp imix kwenye unga kabla kumimina kwenye mchanganyiko) changanya vizuri halafu malizia kwa kuweka unga sembe na iliki usage vizuri.
Chukua trey au sufuria safi weka baking paper Mimina mchanganyiko wako na uoke.
Ukiwiva utoe na uwache upoe. Mkate wa sembe utakua tayari kwa kuliwa.
Picha zinagoma ...
=================================
MKATE WA MAYAI
Mahitaji
1)mayai 12
2)unga kikombe 1 na robo..
3)hiliki 1/2 tablespoon
4)baking powder 2 teaspoon.
5)sukari 1/2 kikombe
6)zabibu kavu 1/2 kikombe....
6)vanilla powder au vanilla essence ama flavor upendayo.
Namna ya kutayarisha.....
1)Vunja mayai yote kwenye bakuli then mimina sukari na hiliki......changanya kwa handmixer hadi sukari iyayuke na kufanya povu....
2) washa jiko 300°-350° ili lipate moto....
3) kwenye bakuli lengine,changanya unga na baking powder....
4)weka vanilla ama flavor upendayo....
5)mimina unga kwenye mchanganyiko wako kidogo kidogo huku ukichanganya vizuri na handmixer...hadi kumaliza
6)mimina mchanganyiko kwenye trey...then tupa tupa zabibu juu yake....
7)weka kwenye oven mkate wako hadi uwive na kua brown....
Swahili sponge cake (mkate wa mayai) tayari kwa kuliwa....
==========================================
MKATE WA TAMBI
Mahitaji
1)Tambi 500g
2) maji 3-4cups
3)sukari 1 cup
4)1/4 hiliki iliyotwangwa
5)tui la nazi 1 cup
6)samli 1 tablespoon.
7)Arki ya rose au flavor yoyote unayopendelea
Namna ya kutaarisha
1)changanya maji,sukari,hiliki na tui la nazi kwenye sufuria
2)weka kwenye moto mdogo mdogo hadi vichemke
3)vunja vunja tambi na uweke
4)pika hadi tui la nazi likauke
5)pakaza samli juu yake
6)washa oven 300°-350° then oka mkae wako....hakikisha unawiva vizuri...
7)mkate wa tambi tayari kwa kuliwa...
==========================================
MKATE WA CHILLA
Mahitaji
Mchele kikombe 1
Hiliki kiasi
Sukari 1/2-3/4
Yai 1
Tui la nazi vikombe 2
Hamira kijiko cha chai kimoja
Namna ya kutaarisha
1)Osha mchele na roweka hadi uwe laini kiasi.
2)weka mchele,hiliki,yai,hamira na tui la nazi kwenye blenda....saga hadi viwe laini
3)mimina kwenye bakuli...subiria uumuke
Namna ya kupika
1)weka chuma cha kuchomea(usitie mafuta) katika jiko moto kiasi... kikipata moto chota upawa mmoja wa mchanganyiko wako na mimina kwenye chuma chako...zungusha ili utandazike
2)funika na ufunikio juu..ukiona mkate wafanya vitundu tundu toa na weka pembeni.
3)fanya hivo hadi umalizie zilobaki
Mkate wa chila tayari kwa kuliwa
=================================
MKATE WA KUMIMINA
Mahitaji
1.Mchele kikombe 1
2.Tui la nazi kikombe 3/4- 1
3.Hamira 1 teaspoon
4.Hiliki kiasi
5.Ute wa yai 1
6.Sukari 3/4 kikombe
Namna ya kutaarisha
1)Roweka mchele usiku 1
2)Saga kwenye blenda mchele,hamira,tui la nazi,hiliki hadi viwe laini..
3)weka sehemu ya joto ili uimuke..
4)washa oven moto kiasi 300-350°..mimina sukari na ute wa yai kwenye mchanganyiko wako then changanya vizuri...
5)weka sufuria jikoni mafuta kidogo yakipata moto mimina mchanganyiko wako
6)baada ya dakika 5-10 mkate ukishaanza kushikana funika kwa ufuniko then weka kwenye oven hadi uwive na kuwa rangi ya brown
7)subiria mkate upoe ndipo uukate vipande vipande
8)mkate wa kuminina tayari kwa kuliwa..
=====================================
MKATE WA UFUTA
Mahitaji
1)unga wa ngano 3 mugs
2)tui la nazi au maziwa 2-2.5 mugs
3)hamira 1teaspoon..
4)yai 1
5)chumvi kiasi.
6)samli au mafuta
7)ufuta
Namna ya kutayarisha...
1)Changanya unga,hamira,tui la nazi,yai na chumvi...uchangane hadi uwe laini kama wa kaimati ila huu uwe mzito kidogo..
2)Wacha hadi uumuke...
Namna ya kuchoma....
1)Hakikisha chuma cha kuchomea kinagandisha vizuri na sio kinachopikiwa mafuta.....vizuri ukiroweke kwa maji ya chumvi
2)Weka chuma kwenye moto then nyunyizia maji ya chumvi alafu chukua mchanganyiko wako kiganja kimoja na utandandaze...nyunyiza ufuta juu yake...
3)Ukikaanza mkate kukauka geuza chuma na ukifudikize kwenye moto hadi mkate uwe dark brown
4)toa mkate kwa kutumia kisu.then pakaa juu samli/mafuta...fanya hivo kwa iliyobakia
5)mikate ya ufuta tayari kwa kuliwa...
Threads nyingine zinazohusu ujuzi na utaalamu wa mapishi mbalimbali ya mkate.....
1. Mkate wa ufuta
2. Mkate Wa Sinia - Mkate Wa Kumimina Aina Ya Kwanza
3. Naan bread
4. Jinsi ya kupika mkate wa haba soda
Last edited by a moderator: