Jifunze TENSES hapa

Welcome to Present Continuous Tense

The present continuous verb tense indicates that an action or condition is happening now, frequently, and may continue into the future.

- Tendo linafanyika sasa, au mara kwa mara, na linaweza kufanyika hapo baadae.

Formula yake ni [am, is, are] + verb [present participle].

Nafsi zimeshatajwa:
Singular (umoja)
First - I
Second - You
Third - He (masculine), She (feminine) and It (objects and animals).

Plural (wingi)
First - We
Second - You
Third - They

Kwa kufata formula ya [am, is, are] + verb [present participle] nitaweka mifano kwa kufatisha nafsi hizo hapo juu.

Singular:
I am writing a letter - Ninaandika barua
You are writing a letter - Unaandika barua
He/She/It is writing a letter - Anaandika barua.

Plural:
We are writing letters - Tunaandika barua
You are writing letters - Mnaandika barua
They are writing letters - Wanaandika barua

Note: Nafsi ya pili umoja na wingi zote zinatumia "are".

Nitaendelea...
 
Mkuu kwa hiyo nikisema ..Me and Mother we are going to church ..nitakuwa sahihi hapo kwenye Are au ni is?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo mko wawili, ni wengi tayari, are ndiyo sahihi.

My mother and I are going to the church.

Hutakiwi kuongeza neno we. We ni kiwakilishi, so kama usingetaja nani na nani ndo we inatumika.
 
Just simple..
Use 'The' followed by common noun
and don't use it for proper noun
 
Mwambie pia kwamba 'me' cannot be used as a subject. Utamfafanulia vipi It's all up to you[emoji16][emoji16][emoji16]
Hapo mko wawili, ni wengi tayari, are ndiyo sahihi.

My mother and I are going to the church.

Hutakiwi kuongeza neno we. We ni kiwakilishi, so kama usingetaja nani na nani ndo we inatumika.
 
" I went to collect the children to the Dar express bus service but they don't their in that bus "

No hivo bro

Sent using Jamii Forums mobile app
HAHHAHAHHAHAHAHAHHAHAHHAHAHHZAHAHHAHAHHAHAHAHAHHAHAHAHHHAHAHAHAHHAHAHAHAHHAHAHAHAHAHHAHAHAHHAHAAHAHHAHAHAHHAHAHHAHAHAHAHHAHAHAHAHHAHAHAHHAHAHHAHAHAHAHHAHAHAHAHAHAHHAHAHHAHAHAHAHHAHAHHAHAHAHAHHAHAHHAHAHHAHAHAHAHAHHHAHAHAHHAHAHAHHAHAHAHHAHA
 
Tuweke jambo sawa kidogo hapa. Katika sarufi (grammar) wakati (time) si sawa na njeo (tense). Wakati (time) ndiyo hugawanyika mara tatu, yani, uliopita, uliopo na ujao lakini njeo (tense) ni lile umbo la kitenzi(verb) ambalo hujidhihirisha kwa namna mbili kuu, umbo linaloonesha wakati wa sasa na lile la wakati uliopita.Tukichambua maumbo haya kwa kila muktadha, yani , uliopo ama uliopita, tutapata maumbo tofautitofauti kadiri mzungumzaji anavyotaka kuwasiliana. Hivyo, neno TALK linaweza kuwa talked, talking ,talk(s) n.k.

Kumbuka hali ya kitenzi kuwa katika wakati uliopita ama wa sasa haina uhusiano wa moja kwa moja na wakati(TIME).Tazama mifano ifuatayo:

If I were a woman, I could bear children.(Je, unadhani huu ni wakati gani, uliopita ama wa sasa? Je, hizo tense ni wakati gani, were/could?) Tazama mfano unaofuata:

Could you give me a pen? (Unadhani huu ni wakati gani, tensi gani?, Je nikikwambia hivi maana yake ninakwambia jambo lililopita? Hapana hii ni sasa, present lakini kitenzi cha wakati uliopita.

Kwa kifupi, katika mifano yote hiyo hapo juu vitenzi vinaonesha wakati uliopita lakini lakini wakati ni wa sasa hivi.

Kwa minaajili hii, Kiingereza hakina umbo maalumu kuashiria future tense. Wengine husema hakina future tense, bali kina wakati ujao tu. Waingereza wao hutumia tense mbalimbali kueleza masuala ya wakati ujao. Tazama mifano michache hapa chini:

1. I am going to marry her next week.(going to)
2.I will go to school on Saturday.(will)
3.Exams start this weekend.(present tense)
4. I am about to finish my studies.(about to)
5. I am visiting my mum this evening.(present continuous)

Mifano hii inathibitisha kuwa hakuna umbo maalumu kudhihirisha future tense katika English. Na hii inathibitisha tense si sawa na time(wakati), kwani utaona hapo present tense imetumika kuelezea masuala ya wakati ujao na kule mwanzoni tuliona maumbo ya wakati uliopita yametumika kueleza matukio ya present time.

Mkanganyiko huu unatusumbua sana sisi ambao tunajifunza Kiingereza kama lugha ya pili. Na ukisoma kw akuchambua kama hivi, ndiyo unachanganyikiwa kabisa. Usomaji mzuri ni ule wa kupewa muktadha(context) , kisha unapewa kanuni indirectly na kuoanisha na muktadha uliopewa. Kwa mfano, unataka kujifunza wakati ujao, utapewa kisa cha Jolita anataka kuoa mwakani. Utawasikiliza kisha utaona miundo wanayotumia na wewe kuweza kuiga huku mwalimu akisiriba kwa kanuni.

Ninawasilisha
 
Umenisaidia pa kuanzia pre-form one ifikapo mwezi wa 9
 
Tenses za lugha gani? Weka na lugha zingine. Hizo tushajifunza shuleni

Sent using my Nokia Torch
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…