Jifunze tofauti kati ya wivu na kutojiamini kwenye mahusiano

Jifunze tofauti kati ya wivu na kutojiamini kwenye mahusiano

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
Wivu kwa maana rahisi ni kutojiamini muda wote unahisi kuna watu wenye sifa zaidi yako watakuibia mpenzi wako, Wivu hukoleza mapenzi.

Kutojiamini ni wivu uliopitiliza kiasi yaani muda wote unahisi umpendaye ana njama mbaya dhidi yako kiasi cha kila siku kuwa na migogoro isiyoisha,Kutojiamini ni sumu ya mahusiano.

DALLI ZA KUTOJIAMINI
1. Asipojibu meseji kwa wakati tayari unahisi kafanya makusudi.

2. Asipoitikia simu yako wewe unajua yupo anafanya kitu kibaya.

3. Ukimpigia simu akiwa anaongea na mtu mwingine tayari unahisi yupo anakusaliti.

4. Siku haiishi bila kumuwazia mabaya yaani unahisi kama vile hakupendi au anakudharau.

5. Muda wote unahisi kama anakudanganya tu hakuna siku unamuamini.

6. Unakuwa mwepesi kukasirika kwa vitu vidogo vidogo tu.

7. Hujui bahati mbaya kila kitu kwako unaona ni njama mbaya aliyoipanga kukufanyia.

8. Akiwa na marafiki zake tayari unahisi anakusaliti au wanamshaurii mabaya kukuhusu wewe.

Ikiwa kila migogoro ya mahusiano yako chanzo ni dalili zaidi ya nusu kati ya hizo kuna uwezekano mkubwa kati yenu kuna mmoja ana tatizo la Kutojiamini.

Kutojiamini kuna leta migogoro na ni ngumu kuwa na mahusiano yenye afya nzuri ikiwa kati yenu kuna migogoro ambayo chanzo chake kikubwa ni Kutojiamini.

Dalili pia za wivu ni kama za kutojiamini sema kama nilivyokwiaha kusema juu kwenye utangulizi kuwa wivu ni Kutojiamini kuliko na kiasi na huwa hakuna migogoro kwenye wivu wa mapenzi bali hukuza mahusiano yenu ya mapenzi , bila wivu wa kiasi mahusiano huwa hayana raha.

Kwenye wivu kuna upendo lakini kwenye kutojiamini kuna upendo wa mashaka ndio maana kutojiamini ni chanzo kingine cha kuvunja mahusiano au kufanya watu wakuogope kwa sababu tu ya migogoro kila siku, hakuna anayependa migogoro ya kila siku .

Kutojiamini chanzo chake ni nini?

Kuna vyanzo vingi vya tatizo hilo yawezekana ikawa ni sababu za kimazingira au za kuzaliwa nazo( kurithi).

Tuone sababu chache zifuatazo:

1. Kuwa na historia ya kusalitiwa : Mara nyingi tatizo la Kutojiamini linaonekana kwa watu ambao wana historia ya kusalitiwa na wenzi waliowapenda sana hivyo wanakuwa hawana imani tena watu , na mara nyingi tatizo linakuwa kubwa kama muhusika ataamua kuingia kwenye mahusiano mapya bila kupona kwa jeraha lake la kwanza hivyo matokeo yake anakuwa anaishi na mtu wa pili kama vile ni mtu yule wa kwanza.

Tiba ya tatizo hilo ikiwa chanzo ni hiki basi tiba yake ni kujiponya majeraha kabla ya kuingia kwenye mahusiano mapya.

2. Chanzo kingine ni tabia yako ya kutafuta ukamilifu wa 100%; Tatizo hili ndio chanzo cha kutoamini kuwa kuna bahati mbaya ndio maana mwenzio akifanya vitu bahati mbaya tayari unajua ni makusudi kakufanyia na tayari ni mgogoro huo , hutaki kumuona kama na yeye ni binadamu bali unamuona kama ni malaika ambaye hakosei hata kidogo.

Tiba yake hapa ni kujifunza kupuuzia baadhi ya vitu vinavyotokea kwenye mahusiano yako muhimu tu visiwe vina madhara makubwa kwenye safari yenu , kuna mambo unaweza kuyapuuzia na yasilete madhara kwenye mahusiano yenu lakini ukikata kufuatilia kila kitu lazima mtakuwa na migogoro mingi sana kwenye mahusiano yenu .

3. Chanzo kingine ni kuathiriwa na huyo umpendaye yaani unayempenda anakuwa na historia ya kukusaliti hivyo tayari kumuamini tena inakuwa ngumu hivyo anakujengea tabia ya Kutojiamini tena na matokeo yake ni kuwa na mashaka dhidi ya matendo yake.

Tiba ya hapa inachukua muda wa kutosha na lazima yeye ndiye akutibu kwa kukuaminisha kuwa kaacha tabia zake za awali .

4. Chanzo kingine ni urithi; Tayari umezaliwa upo hivyo tu yaani una tatizo la Kutojiamini la kuzaliwa nalo.

Hapa kuna tiba kutoka pande mbili ambazo ni kutoka kwako na anayekupenda,Lazima ujikubali kuwa una tatizo na kujidhibiti pale uwezapo na huyo akupendaye inabidi ajue kuwa una kasoro hiyo Hivyo lazima ajifunze kuishi na wewe.

#fikia ndoto zako
 
Siwezi kuwa na wivu uliopitiliza na mtoto wa mtu tuliyekutana ukubwani
 
Dooh kwa kweli naomba sana nisije kufikia hatua hiyo
 
Back
Top Bottom