Jihadhari na aina hii mpya ya utapeli kwa njia ya simu

Jihadhari na aina hii mpya ya utapeli kwa njia ya simu

Sasa hapo unaibiwa vipi, vitu vingine tujiongeze.
Wewe ndo umesema tujiongeze,wengine je wana akili kama yako?!Mnaweza kuzaliwa baba mmoja ,mama mmoja hata kuzaliwa mapacha lakini mnatofauti ya uelewa.
 
Hiyo namba inakupigia simu na kukuliza unajua unaongea na nani?Ukitaja tuu jina labda Oswald anadakia aah unajua kutambua sauti hii pia ni namba yangu isave ndo maelezo ya mizinga inaanzia hapo ooh baba kalazwa.Niazimie laki2
Shida ina anzia kuuacha uswahili na kutaka kuonekana mzungu

Piga uswahili wa swali kwa swali unajua unaongea na nani nawe unamuuliza kwani wanifahamu mimi nani? Atatoka mbio mwenyewe
 
Shida ina anzia kuuacha uswahili na kutaka kuonekana mzungu

Piga uswahili wa swali kwa swali unajua unaongea na nani nawe unamuuliza kwani wanifahamu mimi nani? Atatoka mbio mwenyewe
Kweli mkuu!
 
Shida ina anzia kuuacha uswahili na kutaka kuonekana mzungu

Piga uswahili wa swali kwa swali unajua unaongea na nani nawe unamuuliza kwani wanifahamu mimi nani? Atatoka mbio mwenyewe
Kweli mkuu!
 
Habari wana JF,

Tukiwa humu ni kama Ndugu tunabadilishana mawazo na kuamshana fikra. Jana jumatatu jioni nimepigiwa simu na hiyo namba. Anachofanya yeye ukishapokea ni kukuliza unajua unaongea na nani!? Ukikosea ukajichanganya kumjibu hapo ndio mizinga ya hela huanza tena ndefu.

Kajichanganya kwangu baada ya sauti yake kumfananisha na mtu ambae kanisaidia hela wiki iliyopita kwa kujua hali niliyokuwa nayo. Tigo tusaidieni hiyo ni namba ya kampuni.

Nawasilisha.
🙏
 
Anachofanya yeye ukishapokea ni kukuliza unajua unaongea na nani!?
As usually mimi kama Mtanzania watu kama hao hukutana na swali hili!na lazima wakate simu.

'Wewe ulikuwa unamtaka nani'?,simu ni chombo chako una umiliki kamili so unaweza kumuuliza mtu unavyotaka siyo yeye akupangie so mazingira kama haya ukitapeliwa umetaka mwenyewe.
 
Hayo ni mawazo yako,wengine hawajui wanakuja kujua washaliwa Pesa!
 
Kweli mkuu!
Uswahili una tugharimu ila fresh tu

Mwaka 2011 niliomba Kazi sehemu flani tukapigishwa usahili freshi wakasema watakao pita watapigiwa simu kufahamishwa

Ikapita wiki nimesha sahau hili tukio, meneja wa kampuni akanipigia simu anauliza we nani? Si nikaleta uswahili we wamtaka nani? Kauliza ni mwenye simu ama nikajibu uswahili wa kitanzania pale akakata simu

Ikafata meseji "unakumbuka ulifanya usahili tarehe flani napenda kukujulisha nafasi y'ako imeshukuliwa na mtu wa ziada baada ya wewe kutotoa ushirikiano kupitia mawasiliano ya simu"
 
Mi sijaona hapo Utapeli. Nimeona kuna Mpumbavu mmoja amepiga simu akitaka kujua kama upande wa pili ni mpumbavu mwenzie. Yaani uniulize najua naongea na nani halafu uje unitapeli? How? Hayo si mawazo ya kipumbavu?
Sio mawazo mkuu ni simu unapigiwa somo heading vizuri na maelezo!
 
Back
Top Bottom