Uswahili una tugharimu ila fresh tu
Mwaka 2011 niliomba Kazi sehemu flani tukapigishwa usahili freshi wakasema watakao pita watapigiwa simu kufahamishwa
Ikapita wiki nimesha sahau hili tukio, meneja wa kampuni akanipigia simu anauliza we nani? Si nikaleta uswahili we wamtaka nani? Kauliza ni mwenye simu ama nikajibu uswahili wa kitanzania pale akakata simu
Ikafata meseji "unakumbuka ulifanya usahili tarehe flani napenda kukujulisha nafasi y'ako imeshukuliwa na mtu wa ziada baada ya wewe kutotoa ushirikiano kupitia mawasiliano ya simu"