Jihadhari na hiki kituo cha mafuta cha Victoria

Mtoa mada acha kukichafua kituo chetu bwana hapo kuna pisi kali za kutosha na zinaadabu balaa...uzembe ni wako ukiwa unaingia hapo victiria pampu za petrol zipo kivyake na disel kivyake kwann wewe ukosee kila mara au unaingia apo upo tungi?
Mkuu unaenda kwa pisi kali au huduma?
Pisi kali huwa hanana akili sana.
Ndio maana hawajui wanachokifanya.
 
Kwa ishu kama iliyomtokea mleta uzi gharama za kuclear tatizo zinaweza kufika kiasi gani.

Nauliza kwaajili ya kupata maarifa tu.
 
Hata kama wewe ni darasa la saba utashindwa kuegesha palipoandikwa diesel au petrol?
 
Unawekaje gari bila kumwambia mhudumu unahitaji mafuta ya aina gani? Huo nao uzembe. Nikifika kwenye kituo, kitu cha kwanza ni kumwambia mhudumu aina ya mafuta ninayohitaji. Wala sisubiri aumue mwenyewe. Kama ukimwambia unataka petrol akakupa diesel, sasa hapo kuna tatizo.
 
Haya majibu. Hivi kweli hamjui kuna pump moja ina pipe ya diesel na petrol hapo hapo? Mtoa mada chukua jukumu kulinda gari yako.
 
Kwa ishu kama iliyomtokea mleta uzi gharama za kuclear tatizo zinaweza kufika kiasi gani.

Nauliza kwaajili ya kupata maarifa tu.
≈100,000 kwa gari dogo, gharama kwa ajili ya ku-bleed system ya mafuta na kumwaga mafuta kwenye tenki, tuki-assume uligundua kosa mapema na ukazima gari mara baada tu ya kuweka petroli, ili isiweze kufika, au kama imesha-pumpiwa isilete madhara makubwa.

dizeli ni mafuta mazito kuliko petroli, kwa hiyo yana lubricative property kwenye injini kati ya piston na kuta za cylinder, na kwenye pump. kuweka petroli kunafanya lubrication ipungue hence msuguano.

tuseme taa ya low fuel ilishawaka, akaweka petroli ya 10,000 ≈5 ltrs. akiongezea dizeli hadi tenki lijae ≈60 lts anaweza akadunda nayo tu bila ku-bleed system ya mafuta na gari isipate tatizo.
 
Pole sana mkuu mie sheli zilizokaa kitapeli tapeli huwa sijazi mafuta! Sheli chafu chafu wahudumu hawaeleweki! Sheli smart ni total nikizidiwa naweka Lake oil!
Tatizo hazipatikani kila mahali, mimi Camel na Panone naziogopa kama ukoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…