Jihadhari na hiki kituo cha mafuta cha Victoria

Jihadhari na hiki kituo cha mafuta cha Victoria

Mtoa mada acha kukichafua kituo chetu bwana hapo kuna pisi kali za kutosha na zinaadabu balaa...uzembe ni wako ukiwa unaingia hapo victiria pampu za petrol zipo kivyake na disel kivyake kwann wewe ukosee kila mara au unaingia apo upo tungi?
Mkuu unaenda kwa pisi kali au huduma?
Pisi kali huwa hanana akili sana.
Ndio maana hawajui wanachokifanya.
 
Kwa ishu kama iliyomtokea mleta uzi gharama za kuclear tatizo zinaweza kufika kiasi gani.

Nauliza kwaajili ya kupata maarifa tu.
 
Unawekaje gari bila kumwambia mhudumu unahitaji mafuta ya aina gani? Huo nao uzembe. Nikifika kwenye kituo, kitu cha kwanza ni kumwambia mhudumu aina ya mafuta ninayohitaji. Wala sisubiri aumue mwenyewe. Kama ukimwambia unataka petrol akakupa diesel, sasa hapo kuna tatizo.
Pole sana.. ila nahisi kuna tatizo na kwako pia, why gari yako ipate hizo changamoto?

Kama una gari ndogo ila inatumia diesel ni vizuri uweke lebo ndogo kwenye sehemu ya kuwekea mafuta.

Na kama una gari kubwa inatumia petrol fanya hivyo..

Hii itakusaidia kuepuka makosa kama hayo maana pump attendant wamekariri kwamba gari ndogo zote ni petrol na gari kubwa zote ni diesel
 
How gari ya diesel uwekewe petrol? Au ulipeleka gari yako kwenye pump za petrol badala ya diesel? Maana pump zinaonyesha petrol wapi na diesel wapi
Pampu nyingi za kisasa zinadispense both petrol na diesel.

Petrolpump.JPG
 
Haya majibu. Hivi kweli hamjui kuna pump moja ina pipe ya diesel na petrol hapo hapo? Mtoa mada chukua jukumu kulinda gari yako.
 
Kwa ishu kama iliyomtokea mleta uzi gharama za kuclear tatizo zinaweza kufika kiasi gani.

Nauliza kwaajili ya kupata maarifa tu.
≈100,000 kwa gari dogo, gharama kwa ajili ya ku-bleed system ya mafuta na kumwaga mafuta kwenye tenki, tuki-assume uligundua kosa mapema na ukazima gari mara baada tu ya kuweka petroli, ili isiweze kufika, au kama imesha-pumpiwa isilete madhara makubwa.

dizeli ni mafuta mazito kuliko petroli, kwa hiyo yana lubricative property kwenye injini kati ya piston na kuta za cylinder, na kwenye pump. kuweka petroli kunafanya lubrication ipungue hence msuguano.

tuseme taa ya low fuel ilishawaka, akaweka petroli ya 10,000 ≈5 ltrs. akiongezea dizeli hadi tenki lijae ≈60 lts anaweza akadunda nayo tu bila ku-bleed system ya mafuta na gari isipate tatizo.
 
Pole sana mkuu mie sheli zilizokaa kitapeli tapeli huwa sijazi mafuta! Sheli chafu chafu wahudumu hawaeleweki! Sheli smart ni total nikizidiwa naweka Lake oil!
Tatizo hazipatikani kila mahali, mimi Camel na Panone naziogopa kama ukoma
 
Back
Top Bottom