Jiji bila timu ya ligi kuu ni kama kuvaa fulana bila bukta

Jiji bila timu ya ligi kuu ni kama kuvaa fulana bila bukta

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mji kuitwa Jiji sio lelemama. Jiji huwa na vitu vingi sana kuliko mji na halmashauri. Unapoona jiji linashindwa kuwa na timu ya ligi kuu ni ama hilo Jiji limeharakishwa kuitwa Jiji kisiasa au viongozi wa hilo Jiji hawapaswi kuongoza hilo Jiji.

Mpira unapendwa duniani kote na unatoa Burudani na ajira nyingi sana hata kwa watu wa chini kabisa wanaouza karanga na wapiga kiwi.

Unaweza kuwa na timu ya ligi kuu kwa kupandisha timu ndogo au kununua timu ya ligi kuu.
 
Mleta mada unahisi tatizo hasa linatokana na nini?
Wanaopata nafasi wanasubiri maagizo TU kutoka mamlaka ya teuzi. Wakipewa amri ya kuhakikisha kuwa....... itakuwa. Wenyewe hawajui kuwa mpira ni ajira kwa watu wengi sana, unapunguza uhalifu na magonjwa ya akili pia.
 
kukiwa na timu nzuri za mpira wa miguu ndo maendeleo
wazazi somesheni watoto
 
kukiwa na timu nzuri za mpira wa miguu ndo maendeleo
wazazi somesheni watoto
Huna ujualo, Simba na Yanga wakienda singida kucheza na singida big stars mashabiki watakula na watarudi kuku wa kienyeji, mafuta ya alizeti, asali na mademu wao wazuri wanapata kama sio wachumba basi watahongwa, achilia mbali watu wa migahawa na guest houses. Kiongozi wa Jiji anatakiwa kufikiria multiplayer effects za mpira kwenye uchumi wa watu wake.
 
Mechi ya Dodoma jiji Vs Ihefu Mashabiki hawafiki hata 500 kuangalia mechi. Bongo miyeyusho , wanazipenda timu mbili Tu.
 
Mwanza usimba na uyanga umejaa tele kuliko hata kariakoo kwenyewe, hakuna timu ita survive mwanza
 
Mwanza usimba na uyanga umejaa tele kuliko hata kariakoo kwenyewe, hakuna timu ita survive mwanza
Nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa
Sina pesa ya kulipa mwanasheria ningeandika mengi
Saivi nipo pwani natafuta maisha ila home ntarudi
 
Back
Top Bottom