Jiji la Arusha lamkana Mfanyabiashara Chambulo wadai 'amepotosha'

waziri2020

Senior Member
Joined
May 31, 2019
Posts
197
Reaction score
468
Siku chache baada ya Mwenyekiti wa chama cha mawakala wa utalii Tanzania (TATO) Wilbard Chambulo kuituhumu Halmashauri ya jiji la Arusha kudai kuwa ameilipa Halmashauri hiyo milioni 24 kwenye kodi aliyokuwa akidaiwa lakini akashangazwa kuona taarifa za malipo alizopatiwa zinaonesha kuwa amelipa milioni tatu (3) pekee hivyo kuibua hisia hasi na madai ya uhujumu wa fedha za umma kwa baadhi ya maafisa wa Halmashauri ya jiji hilo leo, Jumatatu Aprili 15.2024 Halmashauri hiyo imekanusha vikali madai hayo

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Mhandisi Juma Hamsini amesema madai ya Chambulo ambaye ni mfanyabiashara na mdau wa masuala ya utalii wa muda mrefu si ya kweli, kwa kuwa baada ya kuibua tuhuma hizo Halmashauri ya jiji la Arusha na ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Arusha ilifanya ufuatiliiaji wa taarifa za mifumo ya kikodi za Chambulo (kwa kuwa hakuna fedha inayopokelewa mkononi), na baada ya ufuatiliaji huo wamejiridhisha masuala kadha wa kadha yanayoleta utata wa ushiri wake kwenye ulipaji wa kodi za serikali hususani zile anazopaswa kulipa kwenye Halmashauri hiyo

Mhandisi Hamsini amesema inadaiwa kuwa Chambulo anamiliki kampuni mbili tofauti ambazo ni 'The Tanganyika Wilderness Camps Limited' na 'Tanganyika Wilderness Camps Limited' ambazo kampuni zote hizo licha ya kwamba zinafanya shughuli zake kwenye maeneo mbalimbali lakini usajili wake umefanyika Arusha, lakini namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) inayotumika ni moja jambo ambalo linaleta majawabu kuwa mmiliki wa kampuni hizo ni mtu mmoja ambaye ni Wilbard Chambulo

Hata hivyo Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa kwenye kumbukumbu za kikodi inaonesha kuwa mauzo ya mfanyabiashara huyo Kwa mwaka yanafikia bilioni 90 ambapo katika fedha hiyo kodi anayopaswa kulipa Halmashauri ni milioni 200 na ushee ambayo kimsingi anadaiwa kwa kuwa licha ya kwamba anaeleza kulipa milioni 24 lakini 'demand note' aliyotumiwa na Halmashauri ni milioni tatu (3) pekee...

MWisho

Screenshot_20240415_180053_Video Player.jpg
Screenshot_20240415_181529_Video Player.jpg
Chambulo (1).jpg
 
Huyu Jamaa ananitia hasira,kwahiyo suala la kujua ana kampuni mbili zinazotumia tin Moja analijua Leo?Na linahusiana vipi na Hilo panga la milion 21?Huyu anaonekana pia ni mmoja wao na mgao kala,waache majibu mepesi Kwa maswala ya msingi.
 
Siku chache baada ya Mwenyekiti wa chama cha mawakala wa utalii Tanzania (TATO) Wilbard Chambulo kuituhumu Halmashauri ya jiji la Arusha kudai kuwa ameilipa Halmashauri hiyo milioni 24 kwenye kodi aliyokuwa akidaiwa lakini akashangazwa kuona taarifa za malipo alizopatiwa zinaonesha kuwa amelipa milioni tatu (3) pekee hivyo kuibua hisia hasi na madai ya uhujumu wa fedha za umma kwa baadhi ya maafisa wa Halmashauri ya jiji hilo leo, Jumatatu Aprili 15.2024 Halmashauri hiyo imekanusha vikali madai hayo

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Mhandisi Juma Hamsini amesema madai ya Chambulo ambaye ni mfanyabiashara na mdau wa masuala ya utalii wa muda mrefu si ya kweli, kwa kuwa baada ya kuibua tuhuma hizo Halmashauri ya jiji la Arusha na ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Arusha ilifanya ufuatiliiaji wa taarifa za mifumo ya kikodi za Chambulo (kwa kuwa hakuna fedha inayopokelewa mkononi), na baada ya ufuatiliaji huo wamejiridhisha masuala kadha wa kadha yanayoleta utata wa ushiri wake kwenye ulipaji wa kodi za serikali hususani zile anazopaswa kulipa kwenye Halmashauri hiyo

Mhandisi Hamsini amesema inadaiwa kuwa Chambulo anamiliki kampuni mbili tofauti ambazo ni 'The Tanganyika Wilderness Camps Limited' na 'Tanganyika Wilderness Camps Limited' ambazo kampuni zote hizo licha ya kwamba zinafanya shughuli zake kwenye maeneo mbalimbali lakini usajili wake umefanyika Arusha, lakini namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) inayotumika ni moja jambo ambalo linaleta majawabu kuwa mmiliki wa kampuni hizo ni mtu mmoja ambaye ni Wilbard Chambulo

Hata hivyo Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa kwenye kumbukumbu za kikodi inaonesha kuwa mauzo ya mfanyabiashara huyo Kwa mwaka yanafikia bilioni 90 ambapo katika fedha hiyo kodi anayopaswa kulipa Halmashauri ni milioni 200 na ushee ambayo kimsingi anadaiwa kwa kuwa licha ya kwamba anaeleza kulipa milioni 24 lakini 'demand note' aliyotumiwa na Halmashauri ni milioni tatu (3) pekee...

MWisho

View attachment 2964450View attachment 2964451View attachment 2964452
makonda
 
Back
Top Bottom