Kwa huu mtido wa kuanika taarifa za mteja ni udhaifu wa halmashauri ya jiji la Arusha ktk ukusanyaji wa mapato na wameonesha kukosa umakini kwa kiwangi kikubwa na kibaya kabisa TAMISEMI wana makubaliano ya kubadilishana taarifa na taarifa za mlipa kodi ni siri lakini hawa jiji wamemuanika mfanyabiashara taarifa zake za kikodi kitu ambacho ni kosa. Wao wanatakiwa kumalizana kisheria mahakamani na siyo kuleta kwenye social media. Hakika ningekuwa Samia ningemfuta kazi Mkurugenzi. Na uliyeleta uzi hapa kama unampenda Mkurugenzi wako futa hii thread
Siku chache baada ya Mwenyekiti wa chama cha mawakala wa utalii Tanzania (TATO) Wilbard Chambulo kuituhumu Halmashauri ya jiji la Arusha kudai kuwa ameilipa Halmashauri hiyo milioni 24 kwenye kodi aliyokuwa akidaiwa lakini akashangazwa kuona taarifa za malipo alizopatiwa zinaonesha kuwa amelipa milioni tatu (3) pekee hivyo kuibua hisia hasi na madai ya uhujumu wa fedha za umma kwa baadhi ya maafisa wa Halmashauri ya jiji hilo leo, Jumatatu Aprili 15.2024 Halmashauri hiyo imekanusha vikali madai hayo
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Mhandisi Juma Hamsini amesema madai ya Chambulo ambaye ni mfanyabiashara na mdau wa masuala ya utalii wa muda mrefu si ya kweli, kwa kuwa baada ya kuibua tuhuma hizo Halmashauri ya jiji la Arusha na ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Arusha ilifanya ufuatiliiaji wa taarifa za mifumo ya kikodi za Chambulo (kwa kuwa hakuna fedha inayopokelewa mkononi), na baada ya ufuatiliaji huo wamejiridhisha masuala kadha wa kadha yanayoleta utata wa ushiri wake kwenye ulipaji wa kodi za serikali hususani zile anazopaswa kulipa kwenye Halmashauri hiyo
Mhandisi Hamsini amesema inadaiwa kuwa Chambulo anamiliki kampuni mbili tofauti ambazo ni 'The Tanganyika Wilderness Camps Limited' na 'Tanganyika Wilderness Camps Limited' ambazo kampuni zote hizo licha ya kwamba zinafanya shughuli zake kwenye maeneo mbalimbali lakini usajili wake umefanyika Arusha, lakini namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) inayotumika ni moja jambo ambalo linaleta majawabu kuwa mmiliki wa kampuni hizo ni mtu mmoja ambaye ni Wilbard Chambulo
Hata hivyo Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa kwenye kumbukumbu za kikodi inaonesha kuwa mauzo ya mfanyabiashara huyo Kwa mwaka yanafikia bilioni 90 ambapo katika fedha hiyo kodi anayopaswa kulipa Halmashauri ni milioni 200 na ushee ambayo kimsingi anadaiwa kwa kuwa licha ya kwamba anaeleza kulipa milioni 24 lakini 'demand note' aliyotumiwa na Halmashauri ni milioni tatu (3) pekee
Ameendelea kufafanua kuwa kampuni ya 'Tanganyika Wilderness Camps Limited' ililipa shilingi 3,347,002.75 kama 'service levy' na kampuni ya 'The Tanganyika Wilderness Camps Limited' ililipa 'service levy' ya shilingi 19,273,028.51 ambayo kiuhalisia inakaribia milioni 20, hata hivyo itambulike kuwa kampuni inayoonekana kwenye mfumo ni ile ya 'Tanganyika Wilderness Camps Limited' iliyolipa shilingi milioni tatu (3) na ushee, na ile kampuni ya pili ambayo ni 'The Tanganyika Wilderness Camps Limited' taarifa zake hazisomi kwenye mfumo husika
Suala la kampuni ya 'The Tanganyika Wilderness Camps Limited' kutoonekana kwenye mfumo linaleta ukakasi kuhusu taarifa sahihi za kodi za mfanyabiashara husika kwa kuwa kampuni hiyo inadaiwa fedha nyingi, hivyo alichokisema mfanyabiashara huyo hakina uhalisia kwa sababu amedai kulipa kodi ya milioni 24 kwa kuwa amejumlisha milioni tatu na ushee aliyolipa kwenye kampuni ya kwanza na milioni 19 na ushee aliyolipa kwenye kampuni ya pili, jambo ambalo halikubaliki kwa kuwa kila kampuni inajitegemea na inapaswa kulipa kodi yake kwa makadirio yake
Amesema inawezekana hiyo ni sehemu ya janjajanja inayotumiwa na mfanyabiashara huyo kwa kuamua kufungua kampuni nyingine kwa kuwa ameona kampuni ya awali ina deni kubwa, na ndio maana kampuni yenye deni kubwa la zaidi ya milioni 200 ndio ambayo haionekani kwenye mfumo
Aidha, Mhandisi Hamsini amedai kuwa amekuwa akimfahamu mfanyabiashara huyo kwa muda mrefu tangu wakati yeye (Mkurugenzi) akihudumu Halmashauri ya wilaya ya Serengeti, ambapo amekuwa akisumbua kwenye ulipaji wa kodi za serikali, na kuongeza kuwa licha ya sintofahamu yote hiyo lakini mfanyabiashara huyo hajawahi kufika kwenye ofisi za Halmashauri ya jiji la Arusha kueleza hoja zake badala yake amekuwa akiwakimbiakimbia maafisa wa Halmashauri pale wanapotaka kutimiza majukumu yao.....
(inaendelea)