Jiji la Arusha lamkana Mfanyabiashara Chambulo wadai 'amepotosha'

Jiji la Arusha lamkana Mfanyabiashara Chambulo wadai 'amepotosha'

Hiyo hela b90 huyo jamaa hajawahi kuimiliki lakini ukisikia mauzo ya hela hiyo maana yake
Mfano wewe una duka na kwa siku una wastani wa mauzo ya laki nne tu basi kwa mwaka utakuwa na mauzo ya zaidi ya milioni 100 hela ambayo hujawahi kumiliki kwa pamoja



Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Ni sawa na kukuambia toka uzaliwe hadi sasa umetumia Tshs. 90B, lakini kiuhalisia hata milioni 50 ya pamoja pengine hujawahi hata ishika
 
Inaonekana mfanyabiashara alikuwa akisaidiwa kutokulipa kodi sahihi huku na yeye akiwasaidia maafisa kuishi mjini; hiyo kujichanganya kwake kutapelekea kuangalia miaka yake yote kama alikuwa akilipa kodi sahihi, vinginevyo atalipa madeni ya miaka yake yote na penati.​
Hao wote mfanyabiashara na mkurugenzi, wanakwenda kumtajirisha mtu Fulani!!
 
We unaijua Arusha ama unaiskia?? Wafanyabiashara hapa walikuwa hawataki kulipa service levy, Wana malimbikizo makubwa ya NYUMA na Sasa huyu mkurugenzi amekuja kuisimamia SHERIA na kukusanya fedha za serikali, wafanyabiashara hawataki... Wanamuundia zengwe hivyo.. sababu tu ya kuisimamia mapato ya serikali.

Tume iliyoundwa na Makonda sio ya sakata hili, ni tume ya kufatilia kero na changamoto zinazokabili sekta ya utalii.

Chambulo ni mtata, kwenye maswala kama haya, Wacha uchunguzi wa kina ufanyike.. mbivu na mbichi zitabainika.

Asitishie watumishi wa kaisari Ili waogope kufata chao
Kodi inatosha,

Service levy ya nini,

Utitiri wa Kodi ndio unakwamisha uwekezaji na ajira sekta binafsi.
 
Alichoeleza DED ni kwamba walituma tu demand ya 3m ila baada ya kufunguka kwa makonda ndiyo wakaingia kuona jamaa anaingiza kiasi gani ndiyo wakagundua ana ingiza zaidi ya 90B kwahiyo kwa hapo inatakiwa alipe 200m+ .

TRA/DED ukiwazingua wanakubambikia Kodi kubwa tu ,kwahapo huyo mfanyabiashara akishupaza shingo atafunga hiyo kampuni yake ,inakuwaje usajili kampuni mbili zenye jina moja? Hapo tofauti ni "The" tu lakini kuhalisia ni kampuni moja sema jamaa wameamua waruke nae.

Kwakifupi jamaa wamechezea control number tu mzigo umelipwa 24m ila DED wamepiga 21m.
hoja ni, kwanini waligundua 90b baada ya makonda kuongea? kwanini hawakugundua kabla kama wao huwa wanatenda kazi kwa uaminifu kama walivyotumwa na serikali? na, mil.200 kwa mtu anayeingiza 9B ni issue? hapo uchunguzi unatakiwa kufanyika, kuna uzembe na mitego ya rushwa iliwekwa.
 
Aliyemwelewa atueleze, anadaiwa mil.200 ila ametumiwa demand note ya 3m na bado ni mwongo, jiji ni wasafi. what if ana ushahidi wa kutoa 24 kauweka pembeni, huyu mkurugenzi amejiridhisha hili?
kwa jinsi nilivyo msikiliza yule bwana anajua anacho zungumza... hadi wafanyabiashara wenyewe wenzake wameamua kumpa uanyekiti ujue wamemuamini...!

yani akili kubwa ikiongozwa na akili ndogo matatizo yake ndio kama hayo..! serikalini kungekuwa na double checking ya wafanya kazi wale wa sekta maalum wangeajiliwa kwa kufuata vigezo stahiki ili wafanye kazi kwa ufanisi... lakini kupeana kazi kama malipo ya uchawa matokeo yake ni aibu sana kwa Serikali...!​
 
Hiyo ni mzunguko wake tu na sio kwamba anazo hizo hela. Turnover yake kwa mwaka itakuwa inafika kabisa hiyo. Jamaa ana magari ya kitalii mengi mno na kila siku yako barabarani. Isitoshe ana hotel nyingi za kitalii. Chambulo ni tajiri mkubwa kwenye utalii ila uropokaji utamponza
Haiwezi fika hiyo ela jifunze kutumia akili
 
Back
Top Bottom