Jiji la Dar es Salaam ndio nguzo kuu kwenye kufanikiwa, vijana kimbilieni huko

Jiji la Dar es Salaam ndio nguzo kuu kwenye kufanikiwa, vijana kimbilieni huko

Miezi 3 TU umebadirika this is Dar, kikubwa uvumilivu km wewe mtoto wa mama usije baki na mama yako uendelee kunyonya
Hasa napendelea biashara
Hapa nilipo nafanya biashara ya duka nikipiga picha huko jinsi kulivyo na muingiliano mkubwa wa watu pesa itakuwepo nitatoboa bila kulima endapo mnayoyasema yana ukweli
 
Maisha popote penye riziki mkuu, mi Kuna sehemu npo mwaka wa 2 huu yaani nahisi kama nilichelewa kupajua yaani siwezi kwenda popote hata uniambie wapi

Hapa nimejipa likizo ijumaa narudi huko, na hakuna hata network ya internet huko, lazima ndo pananiweka mjini na napakubali kinoma
Unapiga mishe gani
 
Hongera sana mkuu, mapambano mema
 
Sehemu yoyote yenye watu, mchanganyiko wa jamii mbali mbali ni rahisi kufanya biashara.

Kwa Dar watu ni wengi kuliko majibu ya sensa, watu milioni 5 sio haba

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Ukweli, Lakini dar Kuna harakati ukifanya unapata Lakini harakati kama hizo ukizifanya mikoani hupati kitu.
 
Kama hzo biashara zinalipa, ni kwa nn uliziacha ukaingia kufanya kazi ya ualimu?
Sababu ni Nyingi mno, kubwa Lakini ni wazazi nadhani unaelewa wazazi wetu wa Kijijini, kama ningetia ugumu kwenda kwenye ajira ningetengwa na Kila mtu.
 
Sababu ni Nyingi mno, kubwa Lakini ni wazazi nadhani unaelewa wazazi wetu wa Kijijini, kama ningetia ugumu kwenda kwenye ajira ningetengwa na Kila mtu.
Jibu ni simple tu, hizo harakati ulizokuwa unazifanya ulikuwa unapata pesa ndogo sana zaidi ya mshahara wa mwalimu thus why wazazi wakaona ni kheri uende uwalimu tu, that's all acha kona kona.
 
Hapa nazungumzia nyanja za mafanikio kwa sisi wasakatonge, nimezaliwa Moshi-kilimanjaro nimezunguka pande Nyingi za Tanzania Lakini dar-es salaam ndio Kila kitu kwa mtu ambae ana chachu ya mafanikio.

MWANZA.
Ukienda Mwanza na hakika asilimia 100% utashindwa kujua uanzie wapi umalize wapi, labda uchague kua machinga na shida ya kua machinga ni bidhaa kutoka, unaweza kupigwa doro kuanzia asubuhi mpaka jioni mpaka utamani kurudi Kijijini kitu ambayo uwezi kuikuta dar Maeneo kama buhongwa, igoma ndio wamejaa machinga na wengi wao ni mwendo wa doro, useme ufungue labda frame kupata katikati ya Jiji ni ngumu huwezi kupata kama una mtaji mdogo. (Usisahau wasukuma wanauza kwa madawa)..kwahiyo na conclude kwa kusema Mwanza sio sehemu nzuri kwa anaeanza kutafuta maisha. Labda ufanye kuzunguka minadani kupeleka bidhaa pande za Magu na kwimba.

MOROGORO.
Ni sehemu nzuri ya kuishi sio kutafuta Hela itakuchukua miaka mingi kuanza Kuona mafanikio, Huu mji ni kama njia ya kwenda dar watu hakuna kabisa, wafanyabiashara wa jumla kutoka pembezoni mfano ifakara, kilombero wakifata mzigo ni moja kwa moja dar, kwa sababu ya ukaribu kijana usijichanganye kwenda Morogoro kuanza kutoka chini.

ARUSHA.
Huku na penyewe mambo ni Yale Yale tu kwa msakatonge labda Uwe machinga kwa kumwaga chini "sendozi" za kina dada jioni mitaa ya mianzini Hapo au stand (jiandae kukimbizwa na migambo), frame uwezi kupata mjini Ukiwa na mtaji mdogo.

Kwanini nasema dar es salaam ndio Kila kitu? Fanya wepesi uje mjini, dar es salaam chochote unauza ukipata location nzuri, Kuna watu waliofanikiwa kwa umachinga wakiwa manzese,ilala mbagala,mbezi,chanika, mbande,kigamboni n.k unaweza usifanye mishe zako kariakoo na Bado ukatoboa, ni kwa sababu muingiliano ni mkubwa.

.....nilikua nanunua viatu vya wadada kariakoo namwaga pale manzese nauza kuanzia asubuhi mpaka usiku saa 4, guess nitakua nimekusanya shingapi?. Mtaji nilioaanza nao ni kama laki 7 Lakini progress unaiona na mtaji unakua, je huko kigoma,mpanda, bariadi unaweza kumwaga viatu barabarani na usiuze hata kimoja.

Nilifanya harakati za viatu Hapo karume nachukua viatu ndani kwa jumla namwaga nje, ndani ya mwezi nikawa na pointer wengi sana Pamoja na wafanyabiashara wa jumla kutoka mikoani huko naanza kuuza saa 11 usiku kufika saa 2 asubuhi jamaa zangu wa gairo nawahesabia mzigo wote tunapatana nachukua changu, hivi nitajie mkoa gani hii inafanyika? Labda Hapo Soko la mtumba memorial Moshi tena kwa kiwango kidogo.

Nimefanya harakati Nyingi sana hapo na Kila harakati niliofanya ilinilipa, mpaka nikaondoka Jiji ilo. Mikoani Huku mzunguko hamna, pesa ni ngumu, ukifungua harakati wachawi ni wengi sana, Sasa kijana unakaa kigoma, mpanda katavi, babati, njombe, shinyanga na unaridhika kabisa?
Sasahivi Niko vijijini huku na mtaji Sasa Lakini Cha kufanya sikioni naona kama nitazika pesa.

Tokeni huko nendeni kwenye Jiji lenye pesa nyingii.
Kauli mbiu ni tutabanana hapa hapa daslam
 
Jibu ni simple tu, hizo harakati ulizokuwa unazifanya ulikuwa unapata pesa ndogo sana zaidi ya mshahara wa mwalimu thus why wazazi wakaona ni kheri uende uwalimu tu, that's all acha kona kona.
Maana kama unaweza kuanza na laki 7 na progress unaiona...namaanisha kutoka kununua mzigo wa laki 5 mpaka kununua mzigo wa million 2 huoni progress?...utalinganisha na mtu anaepata pesa constant miaka yote?...
 
Sio kweli mkuu.
Kama kweli kwenye business yako ungekuwa unapata pesa ya kutosha kuzidi mshahara wa mwalimu i bealive wazazi wako wangekushauri ukomae na biashara tu badala ya kuajiriwa tena secta yenye mshahara finyu kama uwalimu, lakini kwa vile biashara ilikuendea mlama ukawa huna budi tu kwenda huko u-teacher so acha propaganda za kitoto.
 
Anachosema mleta mada namuelewa vizuri ila ustaarabu wa pesa lazima uwepo mimi nilianza kodogo kidogo tena nilianzia kwenye boda nikahamia kwenye genge na likakua na kua duka genge now nina harakati tofauti ila naamini ningekua mkoa wangu wa kilimanjaro mpka nione faida ya genge au duka inhekichukua mida sana kujitanua ki mtaji dar ni sehemu nziri sana zipo riziki usizotarajia imagine mzigo uko kwenye guta na mtu anaununua wote unajiuliza urudi sokoni au usepe home kwahyo dar kwa mtu anaetaka kutoka aje akiwa kajipanga na ajue anataka nini kwa wakati gani.
 
Sababu ni Nyingi mno, kubwa Lakini ni wazazi nadhani unaelewa wazazi wetu wa Kijijini, kama ningetia ugumu kwenda kwenye ajira ningetengwa na Kila mtu.
Japo umewafunua watu macho na nimekubali ulichoandika ila hapa umefeli kama kweli uliacha biashara iliokua inaingiza pesa vizuri na kwenda ualimu ambao kila mwezi wa tano wanasubiri kusikia mishahara imeongezwa au bado umekwama sana labda kama biashara ziligoma na kwa upambanaji ulioandika sidhani kama ingekua rahisi kuacha biashara hata kama ni ngumu
 
Kama kweli kwenye business yako ungekuwa unapata pesa ya kutosha kuzidi mshahara wa mwalimu i bealive wazazi wako wangekushauri ukomae na biashara tu badala ya kuajiriwa tena secta yenye mshahara finyu kama uwalimu, lakini kwa vile biashara ilikuendea mlama ukawa huna budi tu kwenda huko u-teacher so acha propaganda za kitoto.
Soma uelewe, nimekwambia dar ni sehemu nzuri ya kuanza kwa mtu asiyekua na kitu, Kuliko huko mikoani. swala la kwenda kwenye ajira ilo ni swala kingine mkuu wengine wazazi wetu huko vijijini wanaona ajira ni Kila kitu kuliko hizo harakati zako, Niko na mtaji wa kutosha kwa Sasa wa kufanya harakati Lakini location nilipo ndio naona kama harakati sizisomi....Niko njiani kurudi huko mambo yakitiki.
 
Back
Top Bottom