Tetesi: Jiji la Dar kutanuliwa

1. Katika kuhimiza uwekezaji jiji la Dar es Salaam kutanuliwa kujumuisha wilaya za Mkuranga, Kibaha, Bagamoyo na Kisarawe.

2. Pia, uwanja wa ndege wa kimataifa na bandari kujengwa Bagamoyo.

**Forthcoming Kisarawe Digital City.
Hii ndio fursa ya kununua mashamba pwani
 
Dar bado inaeneo kubwa Sana la kuendelea kupokea watu hata kufikia million 10. Nasema hivyo Kwa sababu
Ni muda sasa wa kuachana na vinyumba vya chinichini coz vinakula eneo tu. Haiwezekani eneo la sq.m 2500 likawa na vijumba sita vinavyobeba kaya 6 angali eneo Hilo Hilo lingejengwa kitu Cha gorofa 8 zinekaa hata kaya 36. Tena itaepusha mengi kama kuchimbachimba vichoo sita eneo moja angali ilikuwa ni mpango mji mzuri kitu kinaunganishwa kwenye public sewarage. Tungepunguza hicho kipindupindu kinachowasumbua hapo
 
Watu wetu wanachelewa sana kufikiri.

Weka barabara Sita Mwenge Bagamoyo.
Weka speed train Dar - Chalinze - Msafara.
Dar - Bagamoyo - Chalinze.
Weka Barabara Sita Dar - Moro.
Weka speed train Dar to Moro via Chalinze.

Pima viwanja na Jenga mji wa kisasa standard Bagamoyo, kopesha watu nyumba, Jenga mji wa kisasa Kibaha, Vigwaza, Chalinze na Morogoro halafu kopesha watu nyumba.

Piga marufuku watu kujenga baadala yake kuwe na estate agents wanaojenga maeneo maalum yaliyopendekezwa na Serikali halafu watu wakopeshwe hizo nyumba, hii iwe Tanzania nzima.

Ndani ya miaka 10 tutakuwa mbali sana, tuache blah blah
 
Not really naibobi ni jiji dogo sana kieneo
 
Kama vile nakuelewa alafu sikuelewi. Kwani huwezi kwenda kujenga kisarawe mpaka paitwe Dar, inamaana pakiitwa Dar hapo kisarawe itapunguza au kuongeza Nini? Tuanzie hapo kwanza
Dar inajumliha utawala, mapato nk.
 
kKabla ya huo utanuzi tunakumbushia tu mkoa wetu wa Chato vipi ???????
 
sijui ni kwa nini serikali yetu hawakuliona hili mapema wakalitanua.

walikuwa wanaogopa gharama? "Sidhani"

ukiwa na jiji lenye eneo kubwa hata mapato nayo yanakuwa makubwa
Wasingeliona nadhani wahahusika wakuu walikuwa na mitizamo Yao ama hawakuwa na elimu ya kutosha
 
Unaongelea jiji la Dar au mkoa wa Dar...
Jiji huwa ni Wilaya moja tu.
Ukisema Dar es Salaam kama jiji wengi hawajui kama utawala uliopita ulifanya nini. Bado akilini watu wanaitazama eneo lote la wilaya tatu za awali, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni.
 
Kwa pesa zipi za sisi masikini?
 
Kobazi wanahusika vipi hapo mbona sijaelewa.
 
Ukisema Dar es Salaam kama jiji wengi hawajui kama utawala uliopita ulifanya nini. Bado akilini watu wanaitazama eneo lote la wilaya tatu za awali, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni.
Well,actually utawala uliopita haukufanya makosa....
Hadhi ya Jiji huwa inapewa Wilaya na si mkoa.
Kumbuka
Dar ilipewa hadhi ya Jiji mwaka 1961,ikiwa sehemu ya mkoa wa Pwani....
So,pindi ilipo megwa na kuwa Mkoa, hiyo hadhi ilitakiwa iende kwa mojawapo ya Wilaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…