Tetesi: Jiji la Dar kutanuliwa

Tetesi: Jiji la Dar kutanuliwa

Upanuzi wa mkoa na jiji la Dar es salaam uende sambamba na;
1. Kupima makazi yote ambayo hayajapimwa.
Maeneo mengi ya Dar es salaam ni squatters
2. Tuondoe viwanda mjini tukaviweke nje kabisa ya mji.
Eneo lote la chang'ombe, Vingunguti na Kipawa litumike kwa shughuli nyingine.
Nadhani ingefaa kutenga wilaya nzima ya Mkuranga au Kisarawe kuwa eneo la viwanda.
Wazo zuri.
 
Dodoma ndo baaas tena.
Mi nilidhani watafikiria kuibadili Mtwara ndo liwe lango la kibiashara ili kupunguza watu kuendelea kurundikana Dar.
Mana sasa hv Mlugaluga anaplan kuhamia Dar. Mikoani kwao hakuendelezwi tena.
Wangeimarisha bandari ya Mtwara na uwanja wa ndege.
Hakika.Lakini pia Mtwara kunahitajika kuwe na Reli itakayosaidi kusafirisha mizigo kutoka bandarini mpaka kwa walaji.
 
Mimi binafsi napendekeza Pwani yote iungane na Dar halafu irudishiwe jina la Mzizima, na wilaya ya Ilala ibadilishwe jina iitwe wilaya ya Sinza na ikave hadi Mbezi Mwisho kisha wilaya ya Ubungo ifutwe, yani kifupi wilaya za Mzizima ziwe Sinza, Kinondoni, Kigamboni, Bagamoyo, Kisarawe, Chalinze na Mkuranga, wilaya za Rufiji na Kibiti zifutwe na wilaya ya Mafia ihamishiwe Lindi hapo ndio itapendeza
 
1715692701356.png
... bajameni! ... si Darisalama ilivunjwaga lakini?
😅
 
Jiji la Dar ni dogo mno, watu wamebanana hapo katikati hata hewa safi hakuna wala mpango mji.
Ilitakiwa Pwani nzima iwe ndani ya Dar.

Ona majiji ya wenzetu kama Nairobi, Lagos etc yalivyo makubwa, ndo mana hatuwezi kuyafikia kimaendeleo.

walimbukeni wanakwambia Dar kubwa, "panda helcopter uone kama hauzunguki Dar nzima ndani ya dakika 20" 😀
Kwa mantiki hiyo unataka kuwaondoa baadhi ya wakazi walio lundikana pale Samara, Kariako, Manzese, Mbagara n.k uwapeleke Mkata, Manarumango na Mdaula? Mji unajiganga wenyewe kutokana na Uongozi uliopo mafarakani kutii taratubu, kanuni na Sheria zinazo endesha Mji ama Jiji.
 
Back
Top Bottom