Jiji la Dodoma 2025 limetenga milioni 300 kuweka kamera za ulinzi barabarani (CCTV ) yakitokea matukio kama la Tundu Lissu 2017 zinachakachuliwa

Jiji la Dodoma 2025 limetenga milioni 300 kuweka kamera za ulinzi barabarani (CCTV ) yakitokea matukio kama la Tundu Lissu 2017 zinachakachuliwa

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Badala ya kubana matumizi/ kuondoa matumizi mabaya wakati huu ambao misaada imesitishwa mathalani sekta ya afya kutoka USAID fedha kama hizi zingesaidia kuziba gaps zinanunuliwa CCTV camera ambazo ukitokea uhalifu hazitoi msaada wowote na kukaa kama mapambo tu... mfano tukio la Lissu 2017, Camera zilikuwepo lakini siku hiyo hazikufanya kazi sasa hizi nazo zinaenda kusaidia nini kama kukiwa na matukio zinachakachuliwa?

======
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema Jiji la Dodoma kwa mwaka huu wa 2025 limetenga bajeti ya shilingi milioni 300 kwa ajili ya kuweka kamera za ulinzi (CCTV Camera) katika barabara za jiji hilo.

Akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Anwani za Makazi katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma, Senyamule amesema hatua hiyo ni tafsiri ya kuendelea kuunga mkono operesheni iliyofanyika ya anwani za makazi kwani kupitia camera hizo usalama na utulivu utaongezeka na kuimarika.

Senyamule amebainisha kuwa kamera hizo zitalinda miundombinu ya mawasiliano, kwani kumekuwa na changamoto ya wizi wa nguzo za anwani za makazi, hivyo wizi huo utadhibitiwa.
1739014353349.jpg
 
Kwani eneo alimoshambuliwa Lissu halikuwa na hizo camera?
 
Ujinga mtupi,anuani za makazi zilichimbiiwa kwa fito za miti baada ya muda mfupi nyingi zilioza zikaanguka watu wakajiokotea chuma chakavu,hizo hela ni bora warudie kuchimbia upya kwa nguzo za chuma
 
Back
Top Bottom