Jiji la Dodoma kuwaomba wafanyabiashara kuchangia pesa kwa ajili ya anuani za makazi (postcode) haijakaa sawa

Jiji la Dodoma halikupewa fedha za mradi huu au ni serikali imeishiwa?​

 
Kwa kuwa deni la taifa bado ni himilivu, basi serikali ikakope kuliko kutafuta fedha kupitia wafanyabiashara. Endapo itafanya hivyo, wafanyabiashara wataitumia kama fursa nzuri kwao kukwepa kodi kwa kupitia njia ya "tax avoidance"

Unapotaka msaada wa kifedha kutoka kwa mfanyabiasha ni lazima kwanza u "compromise" naye kwanza juu ya fidia utakayompa kwa namna moja ama nyingine. Hapo sasa itajitokeza changamoto nyingine mpya kwa maafisa wa TRA kukusanya mapato ya serikali.
 

Wilaya ya Sumbawanga watu wamefanya kazi kwa siku 13 wamelipwa siku nne tu. Kwa siku wanalipwa elfu 20,just imagine na hili jua watu wanapuyanga kuanzia saa moja asbuh hadi saa 12 kisha wanalipwa elfu ishirini? hiyo hiyo nauli plus chakula? Mwafwaaaaa
 

Hii michango inalipwalipwaje? tunaomba michango hii ilipwe kwa kutumia control number. Vinginevyo fedha zitaibiwa sana​

 
Kwenda mbali wap? Kuweka vibao?
Kwan mda wanaplan kuhusu swala la anwani za makazi hawakujua kuwa kutaitajika kuwekwa vibao?
Alaf sio dodoma tu wanaoweka vibao, Nyamagana wameweka vibao had vijijin pia lakin sikusikia wakiomba msaada kutoka kwa wafanya biashara
 
Kimsingi ile kodi ya ardhi inaratibiwa na TRA kupitia Tanesco. Kiutendaji TRA inawajibika kwa serikali kuu na siyo halmashauri.

Sent from my SM-G935U using JamiiForums mobile app
Inaelekea uko jikoni kabisa lakini kuna hoja watueleze kwa uwezo wao wa ndani wamefanya nini na siyo kuomba fedha zote za mradi kutoka kwa wananchi.
 
Mapato na matumizi ya Halmashauri yanatofautiana. Mpaka wamefikia hatua ya kuomba msaada kwa wafanyabiashara ina maana wanapumulia mitambo. Its a simple logic.

Sent from my SM-G935U using JamiiForums mobile app
 
Inaelekea uko jikoni kabisa lakini kuna hoja watueleze kwa uwezo wao wa ndani wamefanya nini na siyo kuomba fedha zote za mradi kutoka kwa wananchi.
Kimsingi kuchangia ni hiari kitakacho patikana kitarahisisha kukamilika kwa mradi wa muda mfupi. Kumbuka Jiji lina matumizi mengine ya lazima ya kila mwezi , hivyo kutegemea vyanzo vya ndani pekee haiwezi kumudu gharama za miradi yote kwa wakati.

Sent from my SM-G935U using JamiiForums mobile app
 
Kumbuka pia ukusanyaji wa mapato kwenye halmashauri zetu bado ni tatizo kubwa.....lazma mkurugenzi awe na uwezo mkubwa wa kusimamia vema makusanyo ya mapato ili kuweza walau kumudu matumizi ya halmashauri.

Sent from my SM-G935U using JamiiForums mobile app
 
Nimeshindwa nikujibu nn, ngoja nikudharau nipotezee
 
Tuliwahi aminishwa enzi za Jiwe kuwa jiji la Dodoma linaongoza katika ukusanyaji wa mapato, wakati huo mkurugenzi wa jiji alikuwa Kunambi vipi sasa mambo yamegeuka?
Si wakati wa jiwe tu, hata Sasa wamevunja rekodi ya mapato na sio kwa Dodoma tu ni nchi nzima. Jiwe awamu yake ilikuwa trillion 1.4 kwa mwezi , wao trillion 2. Alafu wanasema eti makusanyo hayatoshi
 
Huyo ni wa kumpuuuza. Dar wameweka vibao, na mikoa mingine hadi raisi aakasifia kuwa Sasa hivi watendaji wake wamewekwa kwenye vibao vya mitaa
 
Si wakati wa jiwe tu, hata Sasa wamevunja rekodi ya mapato na sio kwa Dodoma tu ni nchi nzima. Jiwe awamu yake ilikuwa trillion 1.4 kwa mwezi , wao trillion 2. Alafu wanasema eti makusanyo hayatoshi
Mchwa hawa wanataka kuvimbisha matumbo yao!
 
Ukichomoa hio proposal ndio wanaanza kukuletea figisu wachukue kwa nguvu..

Hii nchi wafanya biashara tunateseka sana... Only God knows
 
nilipokuwa nasoma, niliaminishwa kuwa ombaomba wote Tz walitoka Dom, nikaamini. na sasa Halmashauri yao inatembeza bakuli, nazidi kuchanganyikiwa. makao makuu yamehamishiwa huko na sasa tunaona rais anavo "upiga mwingi" na wafadhili ktk kuomba mikopo nk... dah!
hivi, Tz haina wataalamu wa fani husika za uchumi! wanaanzishaje mambo wasiyoyaweza!? wanaanzisha jambo, wanali-promote kwa nguvu zote baadae wanagundua, kumbe linahitaji fedha ambazo hawana...duh! wanaanza kuzungusha bakuli - tozo za aina kwa aina na bado hazitoshi ...dah!
Rais anaonya kuhusu mfumuko wa bei halafu wanaongeza bei za mahitaji muhimu kama mafuta bila kuelezea mikakati ya kitaifa ya kupambana na huo mfumuko! tunashangilia na kusifu kama mazuzu, tukoje!?
bungeni, pamoja na watu kutangaziwa kuhusu mfumuko wa bei, Waziri Mkuu anaonya wafanyi biashara kutopandisha bei, halafu yanaishia hapo! hakuna ufuatiliaji wala nini. mwambieni bei zimeshapanda. huenda, hawajui kwani wanalipiwa kila kitu kwa kodi zetu...nk. tumtafute aliyetuachia laana, kama hajafa.
tukiambiwa dawa ni KATIBA MPYA tunaweka watu ndani, loh!
 
Sio wajibu wa wafanyabiashara kufanya hilo zoezi,mda huo Serikali inakuwa inafanya nini? Kwani hawakupewa bajeti ya hilo zoezi?
 
Pesa wanazopiga madili haziwatoshi? Huu mkoa Omba omba ni kama laana🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…