Ni ukweli mchungu mkuu, ingawa watu wa Mbeya hupenda kujiamulia mambo yao wenyewe na huwa na misimamo mikali, tabia hii imechangia kuachwa pakubwa kimaendeleo ikilinganishwa na majiji mengine kwa sasa.
Kwa sasa Mbeya hakuna mradi hata mmoja wenye tija unaotekelezwa licha ya kuwa ni kitovu cha mikoa ya nyanda za juu kusini. Aidha, viongozi waliopo hawawezi kubuni mradi wowote wa maana kwa sababu tu za kisiasa.
Ni vigumu kuamini kuwa mkoa hauna supermarket yoyote kubwa na maana ambayo inaweza kutoa huduma hata kwa watalii kupata mahitaji yao ya msingi.
Mbeya inapakana na nchi mbili Zambia na Malawi, ambapo kumekuwa na biashara kati ya hizi nchi lakini ukiangalia mtizamo umewekwa zaidi katika mipaka ya kaskazini na inaonekana ndio kuna biashara kubwa zaidi. Mbeya na ukanda wote unavivutio vingi vya utalii lakini mkazo umewekwa ukanda wa kaskazini na ukanda wa ziwa kwa sasa. Siasa zinaimaliza Mbeya hakuna maendeleo.