Makuku Rey
JF-Expert Member
- Dec 31, 2013
- 3,497
- 3,823
Mkuu tujadili hili suala kwa Hoja!
1. Njia ya barabara nne inajengwa wapi? na kwa maelezo yake ilitakiwa iwe ina pitika sasa. hata hivyo hiyo barabara ilianza kuboreshwa tangu makambako mpaka Igawa. mbeya hawakufika ila kulikuwa na mpango tangu enzi na enzi.. huyo dadako alisema akiingia tu ata anza ujenzi. sasa miaka minne. ujenzi umefika hatua gani.? 😂😂 Wana jua wabongo wengi vilaza, wana subiri waanze ujenzi mwaka 2025.?
2. Jengo la wazazi meta limeanza kijengwa kipindi cha sugu. hata hivyo si sugu wala dadako wote hawahusiki. hata chuo Cha UDSM kina jengwa Mbalizi. kwa taarifa yako kule ni jimbo la Mbeya Vijijini.. Dadako hagusi kule. hata mbunge wa kule haimuhusu hiyo. Hata hivyo hizo hazikuwa ahadi zake kipindi cha kampeni.
Lakini umeona majengo ya Muhimbili, Benjamin na CHATO.. huko kote unadhani ni wabunge wa maeneo hayo wamehusika.??
3. Unaishi mtaa gani na kuna kituo gani cha afya. Hivi unajua mtu akiwa uyole aka umwa ghafla ana lazimika kwenda Igawilo kule juu, anyway hivyo pia vimejengwa kwa hela za Covid. Hahusiki huyo dada enu.
4. stand ya Mkoa kuanza kujengwa baadaye.😂😂. dadako ni mbunge wa mkoa..? hata hizo barabara nne walia saini kwa mbwembwe pale kabwe zipo wapi? usiamini saaana story za baadaye.
5. Maji ya Mto kiwira .... mradi ulianza kipindi cha Sugu. ila hayajafika mpka leo. ila dadako ali jirecord kipindi ni naibu spika eti aliulizia bungeni.. basi hiyo clip akawa ana tereza nayo wakati wa kampeni.😂😂
6. Shule kila mtaa... 😂??. una changanya mtaa, kata, kitongoji na tarafa.. mtaa wa sokoni uyole kuna shule gani imejengwa, kata ya Ghana shule ipi ime jengwa.?
Hebu jaribu ku compare MBEYA Chato, mbeya na Dodoma, Mbeya Na Tanga.
hata Sumbawanga soon wata wazidi. wana barabara nne wale..
MBEYA WAKATI WA MVUA MATOPE, WAKATI WA KIANGAZI VUMBI.
Moja haikai mbili haikai.
Hivi unadhani kwa nini Bajaji Nyingi barabarani. sababu ni kuwa hakuna njia mbadala. hata barabara nyingi mbadala zilijengwa kipindi cha Sugu.
Kwa maslai mapana ya JiJi Letu.
Tupaze sauti , Maendeleo yaje. Kama Mama na Dada haziivi tujue moja.
Mtu akitoka Tukuyu na anataka kwenda Mjini, hana haja ya kupitia Uyole, kuwe na barabara ya mkato. mtu anaye ishi Veta na anafanya kazi Uhindini hana haja ya kupita Mwanjelwa.. Hiyo ndiyo MIZUNGUKO ...
Umeongea point tupu mkuu ila watakuja wanyakyusa wanaojua Mbeya ni Uyole tu watakupinga!
Jiji la Mbeya lingegawanywa katika halmashauri mbili ili kurahisisha maendeleo,jiji la Mbeya ni pana sana aisee kwa bahati Mbaya wafanya maamuzi wanaijua Mbeya barabarani tuu(TANZAM).