Nyanswe Nsame
Senior Member
- Jul 9, 2019
- 166
- 182
Jiji la Mwanza latoa Tsh. bilioni 2.75, uchaguzi Nyamagana CCM kupeta
Serikali imetumia zaidi ya Tsh. Bilioni mbili (2) kuwawezesha kiuchumi wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika halmashauri ya jiji la Mwanza kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Fedha hizo zilitolewa na jiji la Mwanza zimetokana na asilimia 10 za mapato ya ndani kuwawezesha kiuchumi vikundi 848 vyenye jumla ya wanachama 8, 191.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, DK. Philis Nyimbi, amekutana na wanachama wa vikundi hivyo kujadili mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
DK. Nyimbi amesema fedha hizo zinatolewa na Serikali kupitia halmashauri bila riba ili kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi.
Amesema halmashauri hiyo, imetoa fedha hiyo kwa vikundi hivyo ambapo alidai katika vikundi 848 vijana wamejiunga katika vikundi 272 vikiwa na wanachama 3106.
"Vikundi 257 vikiwa na wanachama 4822 wamepata kiasi cha Tsh. Bilioni 1.3 huku vikundi 49 vya watu wenye ulemavu vyenye wanachama 263 vikikopeshwa kiasi cha Tsh. Milioni 375.
"Fedha ambazo zimetolewa kwa ajili ya makundi haya ni nyingi sana na zimesaidia watu wengi sana na hii imeonesha namna gani watu wanavyotumia asilimia 10 zinazotolewa na halmashauri," amesema DK. Nyimbi.
DK. Nyimbi amesema katika kipindi hiki ambacho nchi imeingia katika uchumi wa kati, Serikali inafanya jitihada kuhakikisha inawasaidia watu wake kujikwamua kiuchumi na kukuza pato la taifa.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la kutetea Haki za Wanawake na wasichana la Kivulini, Yassin Ally amesema changamoto iliyopo kwa baadhi ya wajasiliamali ni kutoitumia mikopo inayotolewa na halmashauri bila riba kwa tija.
Amesema wajasiliamali wengi wamekuwa wakitumia fedha hizo katika matumizi ambayo sio sahihi na wengine kuzitumia kwenye mambo ya sherehe (harusi) kwa kununua nguo.
Pia amesema wajasiliamali wengi wamekuwa wakianzisha biashara ambazo haziwanufaishi hatua ambayo amewasisitisha wajasiliamali kubuni biashara zenye tija na manufaa kwao.
Fedha ambazo zimetolewa na halmashauri hiyo ya jiji la Mwanza ni kuanzia kipindi cha mwaka 2016 - 2020, ambapo pia Serikali ilianza kutoa mikopo kwa wananchi wake tangu mwaka 1993.
MWISHO