Jiji limemshinda William Lukuvi?

Jiji limemshinda William Lukuvi?

Lukuvi kama lukuvi ana matatizo yake na mojawapo ni kuwa hayupo pro-active na ni lay-back style of management ndo chanzo, na pili siasa kaweka mbele mno na hii ni kwasababu ili jiji aonavyo yeye lina mawaziri wote na washika dau so ilo linamtisha but kitu ambacho anaweza fanya kikampa sifa ni kama kuondoa omba omba, uchafu uliokithiri na ufanya-biashara za ovyo ovyo koz mengine yanaitaji support ya juu na kujua budget na timetable iko vipi mfano msongamano wa magari na taa za usiku za barabarani..
 
  • La tatu ni siasa kuwepo kila sehemu hata pasipostahili, siku hizi hata magari ya usafi hayapati tender kama hakuna kaushikaji fulani na makada!
hapa ndipo ilipo kasoro ya Kimfumo , kulikua na haja gani kumuondoa Kandoro na kumpeleka Mwanza ?
hebu niwarudishe nyuma kidogo, mnakumbuka Mwaibula ? huyu alikua akipambana uso kwa uso na madereva washenzi wa daladala, hakuwahofu, ila walimuhofu kuliko hawa Majembe sijui.
katika hali isiotolewa maelezo ghafla akanyang'anywa mamlaka yake, wakamnyima nguvu zake....yako wapi sasa.....kazi aliyokuwa napambana nayo mwaibula kwa ghalama nafuu sana leo wamepewa Majembe, kwa ghalama nyingi sana.
siasa kila kitu, siasa kwenye mambo ya kiufundi inaligharimu Taifa hili.
 
Wa kulaumiwa ni mkuu wa nchi, tangu aingie madarakani amebadilisha wakuu wa mikoa mara tatu. Katika kipindi cha miaka minne Mkoa wa Dar es Salaam umebadilishiwa mkuu wa mkoa mara tatu, hiki ni kipindi kidogo sana ufanisi wa kazi kwa kiongozi mmoja hauwezi kuonekana kwa muda mfupi.

Kila kiongozi ana mipango yake ya kazi na muda wake wa kutekeleza, huwezi kumbadilisha kiongozi kwa muda mfupi halafu utegemee ufanisi mkubwa wa kazi.

Awamu ya nne tumeshuhudia wakuu wa mikoa watatu na kwa mtaji huo huo awamu ya tano tunaweza kushuhudia tena wakuu wa mikoa watatu, kwa maana hiyo Mkuu wa nchi akimaliza vipindi vyake viwili atakuwa amebadilisha wakuu wa mkoa wa Dar es Salaam mara sita.

Jiji litaendelea kuwa chafu na vile vibanda vya Machinga vilivyoondolewa na Makamba vitashamiri muda sio mrefu kwani muda wa kupuuzia sheria mara nyingi huwa karibu na uchaguzi. Serikali hua haipendi kuwakera wapiga kura katika kipindi hiko.
 
Kuna mamatizo matatu hapa

  • la kwanza ni uwezo wa lukuvi akiwa kama lukuvi, hili nadhani liko wazi kwamba lukuvi hana ile calliber ya kuongoza miji yenye matatizo kama Dar, ni personality au elimu... i dont know
la pili ni ugumu wa kuongoza Dar kutokana na mfumo wake, labda hatuhitaji mkuu wa mkoa at all... tujiulize meya wa jiji letu ana kazi gani? RAS wetu ana kazi gani? polisi wamegawaje mkoa? elimu wamegawaje huu mkoa?
  • La tatu ni siasa kuwepo kila sehemu hata pasipostahili, siku hizi hata magari ya usafi hayapati tender kama hakuna kaushikaji fulani na makada!
Naomba kuuliza swali hapa.Kama ulivyosema ndivyo,basi majukumu ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ni yapi? ni kina nani wako accountable kwake?
Na huyu Meya wa jiji anaripoti kwa nani?
 
Kazi ya Ukuu wa Mkoa ni kazi demanding, ni saa ngapi Mbunge atatumikia Jimbo lake na wakati huo huo atumikie mkoa wake?

Huyu katoka Isimani, aje aendeleze Dar es Salaam. Kwake nani ataendeleza?

Kama si lazima kuleta mkuu toka nje ya mkoa, wakuu wa mikoa waongoze mikoa wanayotokea.
 
Awamu ya nne tumeshuhudia wakuu wa mikoa watatu na kwa mtaji huo huo awamu ya tano tunaweza kushuhudia tena wakuu wa mikoa watatu, kwa maana hiyo Mkuu wa nchi akimaliza vipindi vyake viwili atakuwa amebadilisha wakuu wa mkoa wa Dar es Salaam mara sita.

Jiji litaendelea kuwa chafu na vile vibanda vya Machinga vilivyoondolewa na Makamba vitashamiri muda sio mrefu kwani muda wa kupuuzia sheria mara nyingi huwa karibu na uchaguzi. Serikali hua haipendi kuwakera wapiga kura katika kipindi hiko.
Halafu kama suala ni Meya wa jiji,Huyu Makamba aliweza vipi kulimudu jiji? wakati huo wa makamba hata usafi ulikuwa angalau.Na sidhani kama Population Growth ya jiji ndio inaleta difference kati ya Lukuvi na Makamba.
 
lukuvi Kimeo Tu, siasa ilimleta Dar , na sasa tumeula wa chuya.
 
kwani CCJ na Lowassa ni ndugu moja ?

Na wewe je Una undugu na Kimtaaa kule Tanga kinaitwa jina lako??? au... Tuacheni utani Lukuvi JIJI limemshinda kwani yeye sasa anaangalia Ubunge tu hawezi kukomand kitu si unajua wadanganyika tumezoweya kusukumwa
 
umenikumbusha Vidaladala vya Tanga, sijawahi kufika kwenye hako kamtaa, ila naonaga daladala zikiwa zimebeba jina NGUVUMALI.....MY WONDERFUL NAME, ni jina la babu yangu.
 
atakuwa amebadilisha wakuu wa mkoa wa Dar es Salaam mara sita.

halafu wanapobadilishwa - wanalipwa marupurupu kibao - usafirishaji wa mizigo etc. yote hiyo kodi ya watanzania - jamani - this is too much!!!!

Jiji la Dar es Salaam linaelekea pabaya - pamoja na uchafu mwingi, msongamano wa magari - naona amani inadidimia - barabarani watu madereva wanataka kupigana - iko siku watakuwa wanashuka kwenye magari - wanapigana - halafu amani ndio itakuwa hamna tena -
Wamachinga na mgambo - siku wamachinga watakapoamua kujiunga na kuchukua silaha za kijadi na kujipigiania - wao na mgambo - ndio itajulikana wazi kuwa amani hamna.

- hakuna planning yoyote - ni mradi tu kumekucha - kumekuchwa
- viongozi gani wanakaa tu ofisini - hata hawajui kinachoendelea - wako kwenye mashingingi - wakitoka ni kwenye mastarehe -
- sidhani hata wana muda wa kusoma magazeti, kuangalia TVs - wameshiba mno kodi za watanzania - SIJUI TUMPE NANI UONGOZI??????

- Hivi kweli wanaweka vipipa (vidogo) vya kutupia taka; magari ya kuzolea taka mabovu na yanamwaga taka na kusambaza walizozoa; yako machache sana -
- asubuhi malori mabovu, makubwa yanabeba cement toka kiwandani - wazo - yanaelekea mjini - yanasababisha foleni mtindo mmoja - yaani - kweli Dar es Salaam imekuwa FUJO - MWENYE NGUVU APITE - WANYONGE SHAURI YAO.........................
NARUHUSIWA KUMWONA LUKUVI IN PERSON???? - NO MR. PRESIDENT NAWEZA KUONANA NAYE NIKAMWELEZA YANAYOTOKEA - IN CASE HANA WA KUMHABARISHA KWANI YUKO BUSY ABROAD????? SIJUI SYSTEM INASEMAJE??? Nisaidieni nipate access ya kumwona Rais................!!!!!!!!!!!!!!!
 
halafu wanapobadilishwa - wanalipwa marupurupu kibao - usafirishaji wa mizigo etc. yote hiyo kodi ya watanzania - jamani - this is too much!!!!

!

Kumbe ni kamradi kamebuniwa ka kuinuana wakati jiji linazidi kudidimia kila siku.Shame on us!
 
Elimu ya Lukuvi na usafi wa jiji wapi na wapi ! kama jiji liliwashinda "wasomi "kama Kandoro, Makamba na Chipungahelo kwanini leo tuone elimu ya Lukuvi ndio kikwazo. Uchafu wa jiji la Dar ni tabia ya wakazi wake, wakzi wa dar ndio wachafu!
 
Tatizo la jiji hili ni kubwa kuliko tunavoweza kufikiri wajameni!

lakini pia its a true reflection ya mahali nji hii ilipofikia.

hakuna mipango, hakuna utekelezaji, hakuna tathmini!

Kero za jiji hili sio msongamano wa magari tu...ni pamoja na the fact kwamba hata makazi yenyewe yapo yapo, hayajapangiliwa, na hii inaleta mtihani mwingine kwenye suala zima la miundombinu: bara bara, mifereji ya maji machafu, simu, umeme nk...hakuna mipango!

sasa kwa hali hii tusitegemee miujiza, walau kwa sasa...system nzima inahitaji a radical revamp,na watu wa namna hiyo nina mashaka kama wapo miongoni mwa waliomo kwenye mfumo!
 
Nadhani mnamuonea mnyalukolo bure, kwani kutofukiwa kwa mashimo kwenye geti la kuingilia ofisi ya mkuu wa mkoa huko Dodoma ndio ishara kuwa alishindwa kazi? Mbona huko Bagamoyo watu wameiba mamilioni ya mapesa toka kwenye mradi wa barabara ya Msata -Bagamoyo ; na hata kwenye halmashauri yenyewe ya Bagamoyo and yet huko ndiko anakotoka mkuu wa nchi; Je kutoogopa kwa hawa mafedhuli [ DED huteuliwa na Rais] kuwa huko ndiko anatoka kiongozi wa nchi kuna maana Rais ameshindwa kutimiza wajibu wake?

Mnyalukolo Lukuvi ni homeboy na ukweli lazima tuseme; unajua kwa sisi wazazi ukiona nyumbani kwako watoto hawazingatii wajibu wao kwa mambo yaliyodhahiri kama kufanya usafi ama chochote kile kilichopo kwenye utaratibu wao ni dalili kuwa wewe mwenyewe una kasoro! wazazi wenzangu watakubaliana na hili!
 
Naomba kuuliza swali hapa.Kama ulivyosema ndivyo,basi majukumu ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ni yapi? ni kina nani wako accountable kwake?
Na huyu Meya wa jiji anaripoti kwa nani?

mimi nimeuliza swali... sasa na wewe umeniuliza swali!! Ok..
 
Elimu ya Lukuvi na usafi wa jiji wapi na wapi ! kama jiji liliwashinda "wasomi "kama Kandoro, Makamba na Chipungahelo kwanini leo tuone elimu ya Lukuvi ndio kikwazo. Uchafu wa jiji la Dar ni tabia ya wakazi wake, wakzi wa dar ndio wachafu!
Jamani msitake ku-justify makosa ionekane kila kitu ni shwari.
uchafu wa Dar sio suala la tabia za watu.ni kwamba hakuna ufatiliaji wa sheria zilizoowekwa wala hakuna accountability kwa watendaji wa jiji.Usitake kusema eti unawabembeleza wakazi wa jiji kuwa wasafi,kamwe jambo hili halitawezekana kwa kuwaomba au kwenda kisiasa zaidi.
Lazima kiongozi uwe na sifa ya ubunifu na uwezo wa kumotivate watu wako ili malengo yako yafanikiwe.Pamoja na sababu zote za ukubwa wa jiji na system ya uongozi lakini na kauzembe kwenye uongozi wa mkoa ni kakubwa sana na kanachangia kuharibu.
 
mimi nimeuliza swali... sasa na wewe umeniuliza swali!! Ok..
ohh! sorry.Lakini hii ndio lifestlye yetu ya kujibu kwa maswali.No wonder jiji linanuka kwa ajili hii.
But am sore nilivosoma post yako i though you know much than me kuhusu madaraka ya ukuu wa mkoa wa Dar.Na ndio maana nikataka kukudadisi ili unifafanulie.
Ila mimi nijuavyo Mkuu wa mkoa ana mamlaka juu ya wakuu wa wilaya na anaweza kuwatuma akiwa pamoja na meya.
sore again for disturbance.
 
- Kwa ni Lukuvi amekuwa RC kwa muda gani so far?

Es!
nafikiri anazaidi ya mwaka, ila sina hakika, tatizo hali imezidi luwa mbaya kuliko kawaida, malundo ya Taka katikati ya mji, mji unanuka sana, mfumo wa majitaka umedorola, wamachinga wametapakaa kila mahala.
kweli inakera sana, bado naamini Siasa ambayo ilimuongoza JK kumleta Lukuvi DSM inaendelea kututesa, ndo maana tunamkumbuka Kandoro hata Makamba Yusuph.
 
upande wa kwanza ni lukuvi hawezi na upande wa pili ni sisi wenyewe...hata aje lowassa hapa na nguvu zake atatoka kapa... sisi ni watu wagumu na walalamishi lakini hatuko responsible na mambo yetu,, hebu angalieni unakuta nyumba chafu, majani yameoteana, bado tutasema ni serikali
 
Back
Top Bottom