Jiko la gesi lilivyozima ndoto na uhai wa Familia ya Abedi Falhum Msangi

Subhanallah. Hatari jamani mpk tutaogopa.

Kuna habari pia nilisoma kuna mdada na wtt wake wawili pia walikufa kwa moto. Alikuwa nje anawasha jiko la mkaa kumbe mtt mmoja yupo ndani anafungua gesi. Mama kamaliza kuoka mkaa nje ile anaingia na jiko Lake kufika mlangoni tu kukalipuka. Mtt mmoja alikuwa nje kuona mama yake anawaka na moto maskin akaenda akamvamia. Walikufa wote. Baba wa huyu dada kupata taarifa na yeye akaanguka kwa mshtuko na kufa pia.
 
Hii stori kuna vitu havijakaa sawa. Huwezi kuwa umezingirwa na moto halafu uwe macho unaingia na kutoka.

Mtu aliyeungua kiasi hicho hawezi kuongea na kukupa stori namna hii.
Weweee. Tema mate chini.

Hapo mtu yyt atataka kuhakikisha anaokoa familia yake hasa wtt wadogo mpk yeye mwenyewe aishiwe na uwezo kabisa kabisa.
 
Watoto ni wakuwaangalia Sana,Jana nimemchapa was kwangu nilipata taarifa alikutwa anachezea Gas jikoni
Nimempiga marufuku kuingia jikoni
 
Inasemekana ni kweli yametokea lakini changamoto ni huyo mwandishi. Ameweka chumvi na pilipili nyingi.
 
Hiiiiih... Pole sana haikuleta Madhara mengine??
Ahsante Mkuu,haikuleta madhara kwa sababu Moto ulikuwa unawaka kwenda juu bila kikomo hivo mtu akawahi akalizima,laiti Kama Moto ungesambaa kwenda pembeni au ungechelewa kuzimwa nyumba ingeungua maana Moto ulifikia Gypsum
 
Elezea vizuri ili tujue ulipokosea umakini unahitajika ili kuepuka hatari
Hakukuwa na makosa ya kibinadamu Bali Hitilafu na jiko lenyewe,Yani Moto ulianza kuongezeka zaidi ya kawaida mpaka kufikia kwenye ceiling
 
Inasemekana ni kweli yametokea lakini changamoto ni huyo mwandishi. Ameweka chumvi na pilipili nyingi.
Kuna pilipili na chumvi iko wapi, na ukute ameelezea kifupi mno.

Ujuaji mwingi sana humu jf.

Just agree with him kama hutaki keep silence

Pole kwa wote waliohusika.
 
Kama unapikia gesi, usipende kuwasha, kuinjika, na kutoka. Ni hatari pia. Upishi wa gesi uwe hapo.
Gesi ni mpishi haraka. Mara nyingi sufuria huwa ina- overflow, na inazima jiko. Gesi inaendelea kutoka, wewe hupo!
 
Watoto ni wakuwaangalia Sana,Jana nimemchapa was kwangu nilipata taarifa alikutwa anachezea Gas jikoni
Nimempiga marufuku kuingia jikoni
Sasa vyema utumie ile ya plate ambayo unawasha tu kwa switch yake. Na switch yake ipo safe mtt hawezi kuzungusha. Mie tangu nimeanza kutumia gesi zaidi ya 10 yrs now natumia jiko la plate
 
Sasa vyema utumie ile ya plate ambayo unawasha tu kwa switch yake. Na switch yake ipo safe mtt hawezi kuzungusha. Mie tangu nimeanza kutumia gesi zaidi ya 10 yrs now natumia jiko la plate
Ninatumia zote mbili,ya plate ndio ilizingua fundi akasema ina tatizo ikabidi ninunue ndogo,
Nitatafuta la plate Tena,
 
Kuna pilipili na chumvi iko wapi, na ukute ameelezea kifupi mno.

Ujuaji mwingi sana humu jf.

Just agree with him kama hutaki keep silence

Pole kwa wote waliohusika.
Kama mnataka silence muweke haya mabandiko huko nyumbani kwenu. Macho yanawezaje kuona ukiwa katikati ya moto unaungua? Tena unatoka nje na kurudi ndani ya nyumba mara tatu huku ukiwa unaungua.

Tumia ubongo wako vizuri.
 
Mkuu majiko ya auto yanakuwaje mkuu hebu fafanua kidgo Kama una experience na uzoefu wake
Yale yasiyohitaji kuwashwa na kiberiti,yaani ukizungusha tu batani ndani kuna spark inarusha cheche ambayo uenda kutana na gas kisha inawasha, madukani ulizia majiko ya gas ya automatic bei kuanzia elf 70
 
Kama unapikia gesi, usipende kuwasha, kuinjika, na kutoka. Ni hatari pia. Upishi wa gesi uwe hapo.
Gesi ni mpishi haraka. Mara nyingi sufuria huwa ina- overflow, na inazima jiko. Gesi inaendelea kutoka, wewe hupo!
Hatari kubwa iliyo kwenye nyumba nyingi ni hawa wanaoitwa ''wadada wa kazi''. Kwa vile treatment ya hawa wasichana siyo nzuri kwenye familia nyingi, wanakuwa wanaacha kazi mara kwa mara na kusababisha familia nyingi kutafuta replacement kila baada ya muda fulani. Hatari ni kuwa unakuta wengi ni wageni wasioelewa madhara ya gesi. Wengine wanafanyishwa kazi nyingi kiasi ambacho huwafanya kushindwa kuwa makini wanapotumia jiko la gesi. Unaweza kukuta msichana anafanya kazi nyingi kwa mpigo, anapika, anafua, anabembeleza mtoto...
 
Usiombe kuchomwa na gas, moto wa gas mwilini ni first burn.
Mimi nilikuwa nachoma taka nikasahau kutoa kopo la dawa ya mbu, hadi leo na alama mkononi sema sababu ya rangi yangu inanihifadhi nilibabuka mkono.
Ukichoma taka hakikisha Hakuna kopo tupu la perfumes, dawa ya mbu, au chupa tupu ya plastic ya maji iliyofungwa hilo ni bomu hatari sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…