Jiko la gesi lilivyozima ndoto na uhai wa Familia ya Abedi Falhum Msangi

Nimekuelewa mkuu. Ila aliyeleta hii stori amefanya exaggeration nyingi sana. Mtu ambaye amezingirwa na moto hawezi kuingia na kutoka ndani mara tatu. Halafu ikawaje macho yakawa bado yanaona?
Wewe unashangaa mtu aliyeungua Moto kutembea Kuna means mwaka juzi alipata ajari mbaya ya gari akajikuta yupo amelala Rami ikaja gari nyingine ikamgonga pia
Jamaa akiwa ramini akawa anataka kuamka ila anarudi chini,kumbe ndio anakata roho hivo
Pia usiwe mvivu kusoma,humu Kuna Uzi was Yule jamaa alipigwa usoni na waya wa umeme akaungua ,alizimia week kadhaa na alipoamka alisimulia
 
Sawa mkuu, tukihoji namna hii ndio tunapata maarifa.
 
Habar wakuu ujumbe huu nimeupata kutuko group moja nikaona ni vyema kushare wa Watanzania wenzangu Ili tuchukue tahadhari[emoji24][emoji24][emoji24] Inauma Sana

Ndugu zangu nataka kuwapa uzoefu na ushuhuda wa kifo Cha jamaa na mdogo wangu Abeid falhum,

Asubuhi saa12 ya Tarehe 19, May nimeamka nikashika simu yangu nikakuta Missed Call 08 za Baba yangu. Wakati najiandaa kumpigia nikaona Notification ya msg kuifungua nakuta ujumbe "..abeid na familia yake wamelipukiwa na gesi Jana usiku, wamelazwa Muhimbili.."
Nikampigia Baba, akanambia tu kifupi kuwa taarifa zipo hivyo.
Nikafunga safari muda huo huo kuelekea Muhimbili,

Nikafika Muhimbili haikuwa ngumu Sana kuingia Wodini sababu nilikuwa na kitambulisho kinachonitambulisha kuwa pia ni Medical Personnel.

Mungu wangu naingia wodi ya SEWAHAJI jicho langu linakutana na Ndugu yangu ABEID, ameungua uso wote hauna ngozi, kwa uchungu sana abeid akaanza kulia.

"..akhaa, kaka nimeungua ndugu yangu, nimeungua aisee, niangalie nilivyoungua.." kiukweli Nilishindwa kumkazia Abeid macho yakiwa yamewiva na machozi nikatoka nje ya wodi nikafuta machozi, nilipojiona nipo sawa sawa nikasema sasa naweza kurudi wodini.

Nikamkuta Abeid pia ametulia, nikampa pole kichwani nikasema hapa sina Cha kuongea na Abeid nikatafuta stori ambayo nitazuga nae pale wodini, akatulia! Unajua nilikuwa Nina mawazo na maswali mengi iweje waungue wote watano, nikajisemea hapa Hilo swali ni gumu kuuliza acha akipona atahadithia. Nikamuaga, nikamwambia naomba nikawaangalie pia Watoto, shemeji na Dada wa kazi.. Iko hivi Abeid alikuwa na familia ya watu wanne na yeye watano. Watoto wawili, Mke na Dada wa kazi, Masikini waliungua woteee.

Kesho nikarudi kumjulia hali mara hii Abeid Wala Hakulia tukawa tunapiga stori pale wodini katikati ya stori bila ya kumuuliza akaanza kunihathia
"...ilikuwa mida ya saa1 usiku (jumatano) nipo nyumbn wife akiwa jikoni akaniita jiko linasumbua kuwaka ni jiko lile la plate, basi nikaenda jikoni na mwanangu wa mwisho akanifata, nilipofika jikoni Bali kujali harufu ya Gesi nika'switch jiko, kaka! kiasi cha sekunde 0 wote tukawa tunaogelea kwny moto, nikamshika mtoto kukimbia nae nje sabb mlango ulikuwa umerudishwa tu, wote tukiwa tunawaka nikambwaga mtoto nje, ndani zimejaa kelele nikarudi tena ndani, sebule imelipuka pia lkn mtoto mwngn alikuwa chumbani (chumba Cha watoto) nikaingia huko kote kunawaka mwanangu anawaka nikamvuta akiwa analia huku anaungua nikakimbia nae nje, Hilo tukio lote la kuungua ninalokuelezea ni ndani hata dakk 5 hazifiki aisee, Moto mkali nikamtupa mtoto nje, nikawa nimewabakiza Mke na mfanyakazi ndani nikiwa naungua nikaona zoezi la kuingia na kutoka ni gumu nikaenda jikoni sabb jiko na sebule ni karibu, nikaushika mtungi wa Gesi nauburuza kuelekea nje (huku nawaka moto) nikautupa nje. Nikarudi tena ndani moto umepungua nasikia harufu ya ngozi yangu namna inanuka kwa kuungua na moto, Mke wangu na msichana wa kazi wote wameungua sabb ya uoga walikuwa wanagalagala huku wanaungua, nikawavuta nje, Wote tukalala nje tunasubiri msaada wa majirani, wengine wakawa wanatufunika na kutuzima moto wengine wanajaribu kuudhibiti moto kuunguza Nyumba.."

Anamalizia "...braza toa Gesi nje ndugu yangu ni hatari sana, hatari mnoo!!

Baada ya kumaliza kuongea na Abeid, nikamuaga kutembelea SEWAHAJI wanawake kumuangalia Mke wa Abeid na Dada wa kazi, wameungua aisee ingawa wanaongea macho wanaona lakini moto wa Gesi umeunguza miili Yao vibaya sana..

Tarehe 23 Alfajiri mtoto wa Abeid wa miaka miwili Akafariki dunia haraka Saa7 mchana wa siku hiyo hiyo tukamzika, tarehe 24 ikawa ni siku tunayomfariji Abeid huku tukiwa tumemficha taarifa za kifo Cha mtoto wake

Tarehe 25 alfajiri Abeid Akafariki, tukasafirisha kuelekea Moshi- Usangi kumhifadhi Abeid, tupo njiani tarehe 26 May alfajiri tukapigiwa simu Dada wa kazi ambae amelazwa Muhimbili amefariki, tukazika haraka Ili tuwahi taratibu za kumhifadhi dada wa kazi, ikawa ni lazima tusafirishe Mwili wa Dada wa kazi maana ni Mkazi wa Masasi.

Tukasafirisha tukazika tukarudi Dar.

Mind you wodini amebaki Mke wa Abeid, na mtoto wa miaka mitano.
Tarehe 31 May Mke wa Abeid Akafariki.

Familia ya watu watano, wanne wamefariki imebaki na Mtoto mmoja tu, Tunamuombea Mwenyezi ampe Ahueni.

Abeid alipokuwa kitandani NENO ambalo alikuwa akisisitiza tuwe makini na Gesi, tufanye namna Gesi ikae nje ya jiko, mpira wa Gesi ndiyo uingie jikoni hata ikivuja na kulipuka haiwezi kuleta madhara kiasi kile.
Dah poleni sana.... hiyo tarehe 23 nilikuwa huku mkoa mmojawapo wa kanda ya kati na mmoja kati ya watu wa karibu wa familia hiyo akanielezea hili tukio,,, so sad asee
 
nilipofika jikoni Bali kujali harufu ya Gesi nika'switch jiko

Tatizo lililosababisha madhara lipo hapa.
 
Ukiweza gas jengea nje, kama una uwanja wa kutosha jiko kuu na dinning lafaa liwe nje ya nyumba, nyumba ni kwa ajili ya kulala tu, wageni wanaishia nje kwenye garden
Kaka hizi ni dudra za mungu ,chukulia mfano ukishaweka mtungi wa gesi nje,je shoti ya umeme utaiweka wapi, je hujawahi kuskia nyumba imeungua kwa sbb ya hitilafu ya umeme, pia utaotoa nje umeme kikubwa ni kumuomba Allah azilinde familia zetu na Mali zetu,.Naunga mkono tahadhari ni muhim, japo alilolipanga Allah lazima litimie narudia lazima litimie tu.
 
Kosa namba waliacha gas itoke kwanza ndipo wakawasha hii ni hatari sana gasi inakuwa ishasambaa nyumba nzima so ukiwasha tu kiberiti nyumba yote inalipuka.
Inatakiwa uwashe kwanza kiberiti ndipo uwashe gas
Majiko ya gas ya plate si ni automatic?
 
Kuna maafa yalitokea kijana aliingia choo cha shimo akiwa na taa ya chemli akaona Mende wengi akachukua spray Ili awue wadudu alizalisha bomu hatari lililofumua choo na yeye
Hii imekaaje mkuu, mbona sielewi!
 
Hii stori imenisisimua sana. Siku kama tano zilizopita nilijisahau nikaacha gesi inatoka, wife alivyoingia akahisi harufu. Akafunga jiko vzr na kufungua milango na madirisha na sisi tukatoka nje. Nilijisikia vibaya sana
Uliacha gesi inatoka wapi, ilikuwaje!!?. Ongea vizuri ili tujifunze tujiepushe na kosa ulilofanya!
 
Hii imekaaje mkuu, mbona sielewi!
Choo cha shimo utoa gas, taa ya chemli ni chanzo cha moto , dawa ya mbu ya kuspray ni SAwa na petrol so gas ya dawa ya mbu ilipofikia moto wa chemli ikalipuka mlipuko ukapokelewa na gas toka shimo la choo ikalipuka.
Ndio maana shimo la choo usipoweka toleo la kutoa hewa na ikakosa pa kutokea ulipuka
 
Back
Top Bottom