Jiko la gesi lilivyozima ndoto na uhai wa Familia ya Abedi Falhum Msangi

Kama mnataka silence muweke haya mabandiko huko nyumbani kwenu. Macho yanawezaje kuona ukiwa katikati ya moto unaungua? Tena unatoka nje na kurudi ndani ya nyumba mara tatu huku ukiwa unaungua.

Tumia ubongo wako vizuri.
Hii story kama in tukio lililotokea kule Tanga, ni tofauti kabisa na lilivyosimuliwa?
Tukio la kule Tanga, in short, ilikuwa siku ya sikukuu karibu na alfajiri, watu wamelala, mtu katoka huko ana njaa Kali, kaweka sufuria jikoni apashe moto chakula, ka -switch on gas, (inavyosemekana), akaanza kutafuta kiberiti, ile kukipata (imeishachukua muda, labda pengine mambo ya tingas), ile kukiwasha pap! Ikawa "boooom" nyumbani mzima!
 
Habar wakuu ujumbe huu nimeupata kutuko group moja nikaona ni vyema kushare wa Watanzania wenzangu Ili tuchukue tahadhari[emoji24][emoji24][emoji24] Inauma Sana

Ndugu zangu nataka kuwapa uzoefu na ushuhuda wa kifo Cha jamaa na mdogo wangu Abeid falhum,

Asubuhi saa12 ya Tarehe 19, May nimeamka nikashika simu yangu nikakuta Missed Call 08 za Baba yangu. Wakati najiandaa kumpigia nikaona Notification ya msg kuifungua nakuta ujumbe "..abeid na familia yake wamelipukiwa na gesi Jana usiku, wamelazwa Muhimbili.."
Nikampigia Baba, akanambia tu kifupi kuwa taarifa zipo hivyo.
Nikafunga safari muda huo huo kuelekea Muhimbili,

Nikafika Muhimbili haikuwa ngumu Sana kuingia Wodini sababu nilikuwa na kitambulisho kinachonitambulisha kuwa pia ni Medical Personnel.

Mungu wangu naingia wodi ya SEWAHAJI jicho langu linakutana na Ndugu yangu ABEID, ameungua uso wote hauna ngozi, kwa uchungu sana abeid akaanza kulia.

"..akhaa, kaka nimeungua ndugu yangu, nimeungua aisee, niangalie nilivyoungua.." kiukweli Nilishindwa kumkazia Abeid macho yakiwa yamewiva na machozi nikatoka nje ya wodi nikafuta machozi, nilipojiona nipo sawa sawa nikasema sasa naweza kurudi wodini.

Nikamkuta Abeid pia ametulia, nikampa pole kichwani nikasema hapa sina Cha kuongea na Abeid nikatafuta stori ambayo nitazuga nae pale wodini, akatulia! Unajua nilikuwa Nina mawazo na maswali mengi iweje waungue wote watano, nikajisemea hapa Hilo swali ni gumu kuuliza acha akipona atahadithia. Nikamuaga, nikamwambia naomba nikawaangalie pia Watoto, shemeji na Dada wa kazi.. Iko hivi Abeid alikuwa na familia ya watu wanne na yeye watano. Watoto wawili, Mke na Dada wa kazi, Masikini waliungua woteee.

Kesho nikarudi kumjulia hali mara hii Abeid Wala Hakulia tukawa tunapiga stori pale wodini katikati ya stori bila ya kumuuliza akaanza kunihathia
"...ilikuwa mida ya saa1 usiku (jumatano) nipo nyumbn wife akiwa jikoni akaniita jiko linasumbua kuwaka ni jiko lile la plate, basi nikaenda jikoni na mwanangu wa mwisho akanifata, nilipofika jikoni Bali kujali harufu ya Gesi nika'switch jiko, kaka! kiasi cha sekunde 0 wote tukawa tunaogelea kwny moto, nikamshika mtoto kukimbia nae nje sabb mlango ulikuwa umerudishwa tu, wote tukiwa tunawaka nikambwaga mtoto nje, ndani zimejaa kelele nikarudi tena ndani, sebule imelipuka pia lkn mtoto mwngn alikuwa chumbani (chumba Cha watoto) nikaingia huko kote kunawaka mwanangu anawaka nikamvuta akiwa analia huku anaungua nikakimbia nae nje, Hilo tukio lote la kuungua ninalokuelezea ni ndani hata dakk 5 hazifiki aisee, Moto mkali nikamtupa mtoto nje, nikawa nimewabakiza Mke na mfanyakazi ndani nikiwa naungua nikaona zoezi la kuingia na kutoka ni gumu nikaenda jikoni sabb jiko na sebule ni karibu, nikaushika mtungi wa Gesi nauburuza kuelekea nje (huku nawaka moto) nikautupa nje. Nikarudi tena ndani moto umepungua nasikia harufu ya ngozi yangu namna inanuka kwa kuungua na moto, Mke wangu na msichana wa kazi wote wameungua sabb ya uoga walikuwa wanagalagala huku wanaungua, nikawavuta nje, Wote tukalala nje tunasubiri msaada wa majirani, wengine wakawa wanatufunika na kutuzima moto wengine wanajaribu kuudhibiti moto kuunguza Nyumba.."

Anamalizia "...braza toa Gesi nje ndugu yangu ni hatari sana, hatari mnoo!!

Baada ya kumaliza kuongea na Abeid, nikamuaga kutembelea SEWAHAJI wanawake kumuangalia Mke wa Abeid na Dada wa kazi, wameungua aisee ingawa wanaongea macho wanaona lakini moto wa Gesi umeunguza miili Yao vibaya sana..

Tarehe 23 Alfajiri mtoto wa Abeid wa miaka miwili Akafariki dunia haraka Saa7 mchana wa siku hiyo hiyo tukamzika, tarehe 24 ikawa ni siku tunayomfariji Abeid huku tukiwa tumemficha taarifa za kifo Cha mtoto wake

Tarehe 25 alfajiri Abeid Akafariki, tukasafirisha kuelekea Moshi- Usangi kumhifadhi Abeid, tupo njiani tarehe 26 May alfajiri tukapigiwa simu Dada wa kazi ambae amelazwa Muhimbili amefariki, tukazika haraka Ili tuwahi taratibu za kumhifadhi dada wa kazi, ikawa ni lazima tusafirishe Mwili wa Dada wa kazi maana ni Mkazi wa Masasi.

Tukasafirisha tukazika tukarudi Dar.

Mind you wodini amebaki Mke wa Abeid, na mtoto wa miaka mitano.
Tarehe 31 May Mke wa Abeid Akafariki.

Familia ya watu watano, wanne wamefariki imebaki na Mtoto mmoja tu, Tunamuombea Mwenyezi ampe Ahueni.

Abeid alipokuwa kitandani NENO ambalo alikuwa akisisitiza tuwe makini na Gesi, tufanye namna Gesi ikae nje ya jiko, mpira wa Gesi ndiyo uingie jikoni hata ikivuja na kulipuka haiwezi kuleta madhara kiasi kile.
Dah pole sana Mwenyezi Mungu awafariji. May their soul rest in eternal peace
 
Nauliza hivi ukiwa na fire extinguisher ndani ya nyumba inaweza saidia kwenye moto wa gesi?
 
tunapojenga majumba yetu tunapaswa pia kuzingatia majanga mbalimbali kama moto nk...

Either jiko liwe nje na chakula kipikwe huko then kiletwe sebuleni, na huko nje kwenye jiko mtungi wa gas ukae nje na piping ndio ziende ndani..
Kama una jiko la ndani ni vyema mtungi ukakaa nje na ndani ukaingiza piping za gas.

Wengi wetu tuna shida ya uelewa na matumizi ya hivi vitu hasa nyumba zenye watu wengi.....ni vyema ukachukua tahadhari .
Itapendeza zaidi ukiacha kabisa kutumia gas maanake hata hizo pipe zinaleta gas ndani na inaweza kuvuja kwenye jiko lenyewe ikawa ajali. Tumia mkaa tu.
 
Hii stori kuna vitu havijakaa sawa. Huwezi kuwa umezingirwa na moto halafu uwe macho unaingia na kutoka.

Mtu aliyeungua kiasi hicho hawezi kuongea na kukupa stori namna hii.
walimwengu hebu kuweni na simile kidogo. Hata stori za majonzi pia mnataka kuletea ujuaji. Abeid nilikuwa namjua na mpaka mauti yanamfika alikuwa anaziungumza. Baba yake alikwenda kumuona hospitali na walikuwa wanaongea kabisa japo hali yako haikuwa nzuri. Asubuhi ya tarehe 25 kwenda hospitali ndio mzee wake anaambiwa mwanae kafariki.
Usipende kuishi kwa mazoea kuwa kila muhanga wa moto anakuwa na athari ya aina moja. Kisichokaa sawa kwako ndo ukweli wa uchungu kwa wenzako.
 
Ume-note vizuri kabisa. Hii ni ya kutunga. Watanzani tunapenda sana kusimulia na kusoma story za majanga na vifo. Hii siyo bure. Ni kutokana na maisha tunayoishi ya shida. Wana saikolojia wanasema mtu aliye kwenye shida anaposikia kuna binadamu mwingine amepata janga kubwa zaidi yake hujiona ahuweni.
Mtu mmoja aliehoji kashambuliwa sana, kuna vitu na mimi nilitaka kuuliza ila nikawa mpole.
 
Hii stori kuna vitu havijakaa sawa. Huwezi kuwa umezingirwa na moto halafu uwe macho unaingia na kutoka.

Mtu aliyeungua kiasi hicho hawezi kuongea na kukupa stori namna hii.
Eti gas ilisambaa nyumba nzima hadi vyumbani na milango ilikua wazi na moto ulisambaa kwote🤨 na hapo hapo nyumba haijaungua. Labda inawezekana ila kwangu naona wamenogesha tu kutoa tahadhali ila hakuna uhalisia kwenye hii story.
 
walimwengu hebu kuweni na simile kidogo. Hata stori za majonzi pia mnataka kuletea ujuaji. Abeid nilikuwa namjua na mpaka mauti yanamfika alikuwa anaziungumza. Baba yake alikwenda kumuona hospitali na walikuwa wanaongea kabisa japo hali yako haikuwa nzuri. Asubuhi ya tarehe 25 kwenda hospitali ndio mzee wake anaambiwa mwanae kafariki.
Usipende kuishi kwa mazoea kuwa kila muhanga wa moto anakuwa na athari ya aina moja. Kisichokaa sawa kwako ndo ukweli wa uchungu kwa wenzako.
Mkuu poleni sana kwa tukio hilo la kuhuzunisha. Mungu awafariji.

Hata hivyo maelezo ya mwandishi yametengeneza picha tofauti na unachosema wewe.
 
Eti gas ilisambaa nyumba nzima hadi vyumbani na milango ilikua wazi na moto ulisambaa kwote🤨 na hapo hapo nyumba haijaungua. Labda inawezekana ila kwangu naona wamenogesha tu kutoa tahadhali ila hakuna uhalisia kwenye hii story.
Ni kweli kabisa mkuu. Aliyeleta stori kaongeza chumvi sana. Habari kama ingekuwa hivyo tungeiona magazetini front page.
 
hii story ina fundisho ila ni ya Uongo wa kutunga tu eti unaungua moto na bado unapata nguvu ya kuingia ndani kwenda kuokoa watu huku unawaka tu moto...
 
Tema mate chini mkuu. Ni haki Yako kuwa na doubt, lakini usiongee as if upo sure na kauli Yako.

Namfahamu huyo jamaa, na kilichotokea sio story.
 
hii story ina fundisho ila ni ya Uongo wa kutunga tu eti unaungua moto na bado unapata nguvu ya kuingia ndani kwenda kuokoa watu huku unawaka tu moto...
Mkuu hili tukio ni la ukweli, last week nilikua Sewahaji nauguza mdogo wangu, na hao marehemu ndio ilikua topic ndani mule wodini. Stori haijapishana na jinsi ilivyokua inaongelewa mule wodini.
 
Huyu ndo Abeid Falhum??? Kwa wanaomjua
FB_IMG_1654336231505.jpg
 
Habar wakuu ujumbe huu nimeupata kutuko group moja nikaona ni vyema kushare wa Watanzania wenzangu Ili tuchukue tahadhari[emoji24][emoji24][emoji24] Inauma Sana

Ndugu zangu nataka kuwapa uzoefu na ushuhuda wa kifo Cha jamaa na mdogo wangu Abeid falhum,

Asubuhi saa12 ya Tarehe 19, May nimeamka nikashika simu yangu nikakuta Missed Call 08 za Baba yangu. Wakati najiandaa kumpigia nikaona Notification ya msg kuifungua nakuta ujumbe "..abeid na familia yake wamelipukiwa na gesi Jana usiku, wamelazwa Muhimbili.."
Nikampigia Baba, akanambia tu kifupi kuwa taarifa zipo hivyo.
Nikafunga safari muda huo huo kuelekea Muhimbili,

Nikafika Muhimbili haikuwa ngumu Sana kuingia Wodini sababu nilikuwa na kitambulisho kinachonitambulisha kuwa pia ni Medical Personnel.

Mungu wangu naingia wodi ya SEWAHAJI jicho langu linakutana na Ndugu yangu ABEID, ameungua uso wote hauna ngozi, kwa uchungu sana abeid akaanza kulia.

"..akhaa, kaka nimeungua ndugu yangu, nimeungua aisee, niangalie nilivyoungua.." kiukweli Nilishindwa kumkazia Abeid macho yakiwa yamewiva na machozi nikatoka nje ya wodi nikafuta machozi, nilipojiona nipo sawa sawa nikasema sasa naweza kurudi wodini.

Nikamkuta Abeid pia ametulia, nikampa pole kichwani nikasema hapa sina Cha kuongea na Abeid nikatafuta stori ambayo nitazuga nae pale wodini, akatulia! Unajua nilikuwa Nina mawazo na maswali mengi iweje waungue wote watano, nikajisemea hapa Hilo swali ni gumu kuuliza acha akipona atahadithia. Nikamuaga, nikamwambia naomba nikawaangalie pia Watoto, shemeji na Dada wa kazi.. Iko hivi Abeid alikuwa na familia ya watu wanne na yeye watano. Watoto wawili, Mke na Dada wa kazi, Masikini waliungua woteee.

Kesho nikarudi kumjulia hali mara hii Abeid Wala Hakulia tukawa tunapiga stori pale wodini katikati ya stori bila ya kumuuliza akaanza kunihathia
"...ilikuwa mida ya saa1 usiku (jumatano) nipo nyumbn wife akiwa jikoni akaniita jiko linasumbua kuwaka ni jiko lile la plate, basi nikaenda jikoni na mwanangu wa mwisho akanifata, nilipofika jikoni Bali kujali harufu ya Gesi nika'switch jiko, kaka! kiasi cha sekunde 0 wote tukawa tunaogelea kwny moto, nikamshika mtoto kukimbia nae nje sabb mlango ulikuwa umerudishwa tu, wote tukiwa tunawaka nikambwaga mtoto nje, ndani zimejaa kelele nikarudi tena ndani, sebule imelipuka pia lkn mtoto mwngn alikuwa chumbani (chumba Cha watoto) nikaingia huko kote kunawaka mwanangu anawaka nikamvuta akiwa analia huku anaungua nikakimbia nae nje, Hilo tukio lote la kuungua ninalokuelezea ni ndani hata dakk 5 hazifiki aisee, Moto mkali nikamtupa mtoto nje, nikawa nimewabakiza Mke na mfanyakazi ndani nikiwa naungua nikaona zoezi la kuingia na kutoka ni gumu nikaenda jikoni sabb jiko na sebule ni karibu, nikaushika mtungi wa Gesi nauburuza kuelekea nje (huku nawaka moto) nikautupa nje. Nikarudi tena ndani moto umepungua nasikia harufu ya ngozi yangu namna inanuka kwa kuungua na moto, Mke wangu na msichana wa kazi wote wameungua sabb ya uoga walikuwa wanagalagala huku wanaungua, nikawavuta nje, Wote tukalala nje tunasubiri msaada wa majirani, wengine wakawa wanatufunika na kutuzima moto wengine wanajaribu kuudhibiti moto kuunguza Nyumba.."

Anamalizia "...braza toa Gesi nje ndugu yangu ni hatari sana, hatari mnoo!!

Baada ya kumaliza kuongea na Abeid, nikamuaga kutembelea SEWAHAJI wanawake kumuangalia Mke wa Abeid na Dada wa kazi, wameungua aisee ingawa wanaongea macho wanaona lakini moto wa Gesi umeunguza miili Yao vibaya sana..

Tarehe 23 Alfajiri mtoto wa Abeid wa miaka miwili Akafariki dunia haraka Saa7 mchana wa siku hiyo hiyo tukamzika, tarehe 24 ikawa ni siku tunayomfariji Abeid huku tukiwa tumemficha taarifa za kifo Cha mtoto wake

Tarehe 25 alfajiri Abeid Akafariki, tukasafirisha kuelekea Moshi- Usangi kumhifadhi Abeid, tupo njiani tarehe 26 May alfajiri tukapigiwa simu Dada wa kazi ambae amelazwa Muhimbili amefariki, tukazika haraka Ili tuwahi taratibu za kumhifadhi dada wa kazi, ikawa ni lazima tusafirishe Mwili wa Dada wa kazi maana ni Mkazi wa Masasi.

Tukasafirisha tukazika tukarudi Dar.

Mind you wodini amebaki Mke wa Abeid, na mtoto wa miaka mitano.
Tarehe 31 May Mke wa Abeid Akafariki.

Familia ya watu watano, wanne wamefariki imebaki na Mtoto mmoja tu, Tunamuombea Mwenyezi ampe Ahueni.

Abeid alipokuwa kitandani NENO ambalo alikuwa akisisitiza tuwe makini na Gesi, tufanye namna Gesi ikae nje ya jiko, mpira wa Gesi ndiyo uingie jikoni hata ikivuja na kulipuka haiwezi kuleta madhara kiasi kile.
Aisee[emoji24]
 
Back
Top Bottom