Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tupunguze na Visiwani iwe na majimbo mawili tu yaani Pemba na Zanzibar.Tumesikia hii leo Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akitangaza Tume kufungua pazia la kuanza kupokea maombi ya ugawanywaji na ubadilishaji wa majina ya majimbo ya uchaguzi.
Lakini Je! Unadhani ni Jimbo gani linastahili kugawanywa na kwanini.
Rombo kusini na kaskaziniLa kwetu watupeleke KENYA
Vipi kuhusu idadi ya watu mvomero?Jimbo la Mvomero ni kubwa sana.
Hivi si tulimsikia chura kiziwi akisema hakutakuwa na mgawanyo wa maeneo mapya ya utawala kwa kigezo cha Bajeti!Tumesikia hii leo Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akitangaza Tume kufungua pazia la kuanza kupokea maombi ya ugawanywaji na ubadilishaji wa majina ya majimbo ya uchaguzi.
Lakini Je! Unadhani ni Jimbo gani linastahili kugawanywa na kwanini.
Sasa lile jengo la bunge pale dodoma si litabaki tupu?Igawanywe mikoa badala ya majimbo ya kisiasa ya Uchaguzi.
Pia tubadilishe Katiba ya nchi ili Wabunge watokane na mikoa, kila Mkoa utoe Wabunge wa kuchaguliwa wapatao wawili au wanne, yaani Wabunge Wanaume Wawili na Wabunge Wanawake pia wawe wawili. Kusiwepo na Wabunge wa Viti Maalumu wa kuteuliwa Kutokea Majimboni au wa kuteuliwa kutoka kwenye Uwakilishi wa Majimbo au Mikoa.
Rais wa nchi apewe nafasi zake Kumi tu (10) za kuteua Wabunge wa Kuteuliwa, pasiwepo na idadi nyingine zaidi ya Wabunge wa kuteuliwa zaidi ya hao Kumi wa kuteuliwa na Rais wa nchi.
Ni mambo ya ajabu sn kule bungeni wamejaa wagonga meza tupu hakuna la maanaHivi si tulimsikia chura kiziwi akisema hakutakuwa na mgawanyo wa maeneo mapya ya utawala kwa kigezo cha Bajeti!
Mbona wanatofautiana na huyo jaji!?
NB: ni lini tumepata tume huru ya uchaguzi? Mchakato wake ulifanyikaje?
Kwani sababu za kuwachagua Wabunge ni zipi hasa? Ili wakajaze ukumbi wa Bunge kule Dodoma au kwa sababu waende huko Bungeni kwa ajili ya kuwasilisha Maoni yetu sisi Wananchi???Sasa lile jengo la bunge pale dodoma si litabaki tupu?