Jimbo gani ligawanywe, kwanini?

Jimbo gani ligawanywe, kwanini?

Tumesikia hii leo Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akitangaza Tume kufungua pazia la kuanza kupokea maombi ya ugawanywaji na ubadilishaji wa majina ya majimbo ya uchaguzi.

Lakini Je! Unadhani ni Jimbo gani linastahili kugawanywa na kwanini.
Tupunguze na Visiwani iwe na majimbo mawili tu yaani Pemba na Zanzibar.
 
Jimbo la Ngara ni kubwa
Ni vyema tupate majimbo mawili ambayo ni Jimbo la Rulenge na Jimbo la Ngara
 
Jimbo la BUKOBA Vijijini ni kubwa mno
Jimbo la MULEBA kusini ni kubwa mno
Jimbo la KIGOMA kusini ni kubwa mno
 
Kumbe tuna hela,tunataka tena kuongeza wasinziaji afu baada ya masaa 6 tunawalipa laki 3,nchi ya kijinga sana hii
 
Tumesikia hii leo Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akitangaza Tume kufungua pazia la kuanza kupokea maombi ya ugawanywaji na ubadilishaji wa majina ya majimbo ya uchaguzi.

Lakini Je! Unadhani ni Jimbo gani linastahili kugawanywa na kwanini.
Hivi si tulimsikia chura kiziwi akisema hakutakuwa na mgawanyo wa maeneo mapya ya utawala kwa kigezo cha Bajeti!
Mbona wanatofautiana na huyo jaji!?

NB: ni lini tumepata tume huru ya uchaguzi? Mchakato wake ulifanyikaje?
 
Igawanywe mikoa badala ya majimbo ya kisiasa ya Uchaguzi.
Pia tubadilishe Katiba ya nchi ili Wabunge watokane na mikoa, kila Mkoa utoe Wabunge wa kuchaguliwa wapatao wawili au wanne, yaani Wabunge Wanaume Wawili na Wabunge Wanawake pia wawe wawili. Kusiwepo na Wabunge wa Viti Maalumu wa kuteuliwa Kutokea Majimboni au wa kuteuliwa kutoka kwenye Uwakilishi wa Majimbo au Mikoa.

Rais wa nchi apewe nafasi zake Kumi tu (10) za kuteua Wabunge wa Kuteuliwa, pasiwepo na idadi nyingine zaidi ya Wabunge wa kuteuliwa zaidi ya hao Kumi wa kuteuliwa na Rais wa nchi.
Sasa lile jengo la bunge pale dodoma si litabaki tupu?
 
Hakuna sababu ya kugawa majimbo ni kutuongezea gharama za bure walipa kodi, tena majimbo yapunguzwe
 
Hivi si tulimsikia chura kiziwi akisema hakutakuwa na mgawanyo wa maeneo mapya ya utawala kwa kigezo cha Bajeti!
Mbona wanatofautiana na huyo jaji!?

NB: ni lini tumepata tume huru ya uchaguzi? Mchakato wake ulifanyikaje?
Ni mambo ya ajabu sn kule bungeni wamejaa wagonga meza tupu hakuna la maana
 
Back
Top Bottom