Wana Iramba habari.
Kama kuna mambo ya kufanyia majaribio na mambo mengine siyo, mkumbuke kuna watu kazi yao ni kutaka kuharibu tu.
Tuna mbunge wetu, wa kwetu wenyewe mzawa ( local native) na mzalendo kwa nchi yetu na msomi Mwigulu Lameck Mchemba, hakuna haja ya kuanza kufanya majaribio nyakati hizi za kazi na mh Rais wetu wa kazi MAGUFULI.
Mwigulu amepikwa kimila, darasani na siasani ni mjuvi wa mambo na ni moja kati ya vijana wa nchi hii wenye uthubutu, maono, na asiyetetereka.
Kwa kuwa tuka naye hapa Iramba tusimbeze ila tumtie moyo anafanya kazi nzuri sana,kama huamini waulize wenzetu kwenye majimbo mengine watakwambia maana kuna orodha ya wabunge watoro, waliokuwa mawaziri mizigo zinasambaa mitandaoni.
Kwangu mimi sisi wana Iramba tunamuhitaji mh Mwigulu zaidi ya yeye anavyotuhitaji sasa.
Mwigulu siyo wa ( local level) hapa, huyo ni national figure with an international repute, anaweza kuwa mbunge kokote kadri atakavyopendezwa iwe Dar,Arusha, Morogoro, Mwanza, Manyara, Pwani nk.
Kaka mwigulu wananchi wako sisi tunakuomba tena uchukue form na tunawaomba wajumbe wa mkutano mkuu CCM wilaya wakupitishe uje tukuchague umalizie kazi uliyoianza.
Umeweka kumbukumbu kwetu hatutaki kufanya majaribio.
Viva Mwigulu,
Viva Iramba.