Jimbo la kigamboni halina uwakilishi tangu Dr.Ndugulile afariki

Jimbo la kigamboni halina uwakilishi tangu Dr.Ndugulile afariki

Tangu Dr. NDUGULILE afariki ni miezi sasa, kigamboni haina mbunge wala hakuna uchaguzi mdogo, tatizo nini?

Tume imesahau au wanasiasa wamesahau, au muda hauruhusu?
Siku hizi sheria hazifuatwi kihivyo. Uchaguzi hautakiwi kwa sasa maana kwenye kampeni kutapandisha joto la no reforms, no election.

Hata hivyo kwa kuangalia muundo wa kiutawala na kiuongozi, hata mbunge asipokuwepo hakuna athari ya msingi, hasa kama mbunge wake alikuwa ni wa kuunga mkono chochote kinacholetwa na serekali, bungeni ama nje.
 
Basi badala kuongeza majimbo tupunguze, mikoa iwe majimbo ya uchaguzi.
 
,muda hauruhusu?
Yes
Kwa mujibu wa Ibara ya 49 (5) ya Sheria Mpya ya Uchaguzi inasema (5) Endapo uchaguzi mdogo unatakiwakufanyika na tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge imetangazwa au imejulikana kwa mujibu wa matukio yaliyo ainishwa katika Ibara ya 90(3) ya Katiba, uchaguzi mdogo hautafanyika katika muda wowote wakati wa kipindi cha miezi kumi na mbili mara tu baada ya tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge
P
 
Kwa ufahamu wangu, Kwa sheria za tume ya uchaguzi, hilo jimbo uchaguzi unapaswa kufanyika, na kwa sasa michakato ya uchaguzi ilipaswa iwe imekamilika.
 
Kwahiyo alikufa muda mbaya?

Alipaswa afe lini ili kigamboni wapate mbunge mwingine?
Kigamboni walipaswa kupata mbunge, maana alifariki zaidi ya miezi 6 kabla ya bunge kuvunjwa. Ila hofu ni kuwa uchaguzi ukifanyika sasa utasababisha nio ovu ya wizi wa uchaguzi mkuu kuonekana. Na neno no reforms, no election litashika kasi.
 
Lakini no reform no election ina mwezi mmoja tu tangu ianzishwe?

Dr.Ndugulile alikuwa kesha fariki.
 
Sasa wananchi wanawakilishwaje muda huu, au wanaadhibiwa kwa mbunge wao kufariki kipindi kibaya?
Mbunge ww ccm hata asipokuwepo hakuna madhara, maana michango ya wabunge wa ccm hudhibitiwa na party caucus ya chama, hivyo awepo asiwepo ni sawa tu. Na uchaguzi ukifanyika ni kupoteza muda, kwani mbunge wa atatangazwa kimabavu. Na pia ni kutoa fursa kwa vyama vya upinzani kuamsha hisia za watu dhidi ya ulegelege wa ccm, na wizi wao wa kura.
 
Lakini no reform no election ina mwezi mmoja tu tangu ianzishwe?

Dr.Ndugulile alikuwa kesha fariki.
Hiyo no reform no election ilipitishwa na vikao halali vya cdm Freeman Mbowe akiwa bado mwenyekiti. Ila sasa Lisu ndio anaipazia sauti sana.
 
Back
Top Bottom