- Thread starter
- #21
Vyama vya siasa havina interest au vimekata tamaa au vimesusa?Kwa ufahamu wangu, Kwa sheria za tume ya uchaguzi, hilo jimbo uchaguzi unapaswa kufanyika, na kwa sasa michakato ya uchaguzi ilipaswa iwe imekamilika.
Vyama vya suasa ndio wadau wa chaguzi hizo, sisi wananchi hatuwezi kuishinikiza tume ifuate sheria, ila vyenyewe vinaweza, lakini sijasikia hata vyombo vya habari kuandika au kuuliza.
Vilipaswa viwe vimeanza heka heka za kampeni na uchaguzi, hata mbunge akidumu wiki mbili, chama kitapata ruzuku, na mbunge atalipwa kiinua mgonho cha milioni 500.
Sielewi kwanini havichangamki.