Chukwu emeka
JF-Expert Member
- Jan 12, 2018
- 25,299
- 40,929
Habari wa JF,
Katika hali ya kushangaza na kustaajabisha,jimbo la Kisesa hakuna MwanaCCM yeyote aliyechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kukiwakilisha Chama kugombea ubunge.Pamoja na mafuriko ya wanachama wa Chama hicho maeneo mengine, lakini Kisesa bado wanaCCM wameufyata.
Chanzo changu kilichonitonya taarifa hii kinasema makada wengi wanamuogopa sana Mpina kwasababu ya mizizi aliyoiweka jimboni humo na kukubalika sana na wananchi wake pamoja na wanaCCM wenyewe.Pia inatajwa imani za kishirikina,mwamba inasemekana yupo vizuri katika eneo hilo,hivyo wengi kuwa na uoga wa kumvaa na hata kuogopa kuchukua fomu.
Pamoja na Rais kumsema namna hasi,lakini bado jamaa ananguvu kubwa Kisesa.Sasa itakuaje wakati Mbunge huyu aliyetajwa kama Mbunge wa kitaifa akirudi kuchukua fomu na kurudisha peke yake
Ngoja tuone mwisho wa jambo hili.