Tetesi: Jimbo la Kisesa analotoka Mpina,hakuna aliyechukua fomu mpaka leo hii

Habari wa JF,

Katika hali ya kushangaza na kustaajabisha,jimbo la Kisesa hakuna MwanaCCM yeyote aliyechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kukiwakilisha Chama kugombea ubunge.Pamoja na mafuriko ya wanachama wa Chama hicho maeneo mengine, lakini Kisesa bado wanaCCM wameufyata.

Chanzo changu kilichonitonya taarifa hii kinasema makada wengi wanamuogopa sana Mpina kwasababu ya mizizi aliyoiweka jimboni humo na kukubalika sana na wananchi wake pamoja na wanaCCM wenyewe.Pia inatajwa imani za kishirikina,mwamba inasemekana yupo vizuri katika eneo hilo,hivyo wengi kuwa na uoga wa kumvaa na hata kuogopa kuchukua fomu.

Pamoja na Rais kumsema namna hasi,lakini bado jamaa ananguvu kubwa Kisesa.Sasa itakuaje wakati Mbunge huyu aliyetajwa kama Mbunge wa kitaifa akirudi kuchukua fomu na kurudisha peke yake

Ngoja tuone mwisho wa jambo hili.
MPina jembe
 
Sio uwaziri mkuu, hata ubunge hatoboi. Akichukua form watamuandalia mpinzani feki na kumtangaza kibabe. Hiyo imeenda. Alikuwa lakini sasa sio. CCM kwa fitna hakuna mfano.
Ccmu hawana fitna yoyote , watz ni vilaza huo ndo mseleleko wa watz

Kwa wanaojitambua wangemchukulia form Mpina kama wanamwitaji
 
Samia sidhani kwa mawazo yangu anaweza kumpa upm jamaa😀
Anaweza kumpatia maana katika watu imara na yeye yumo, uzuri awamu hii list siyo ndefu mfano;

1. MPINA-Mtu mwenye misimamo hapa CCM italamba dume lakini VP(Nchimbi) lazima atumike kumfunga kizibiti mwendo maana mwamba achelewi kuchukua taji.

2. J MAKAMBA-chuma ukikipa nafasi utafurahi mwenyewe ni vile uafrica bado upo kwa kichwa.

3. D BITEKO-Huyu atahitajia kuwa na msaidizi(kama alivyo sasa) ili aweze kumove vizuri maana mikimiki haiwezi/hajaizoea.

4. H. BASHE -Kichwa kimetulia sana ingawa mwepesi kuelemea upande mmoja lakini akipikwa ataivaa vizuri.
 
Habari wa JF,

Katika hali ya kushangaza na kustaajabisha,jimbo la Kisesa hakuna MwanaCCM yeyote aliyechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kukiwakilisha Chama kugombea ubunge.Pamoja na mafuriko ya wanachama wa Chama hicho maeneo mengine, lakini Kisesa bado wanaCCM wameufyata.

Chanzo changu kilichonitonya taarifa hii kinasema makada wengi wanamuogopa sana Mpina kwasababu ya mizizi aliyoiweka jimboni humo na kukubalika sana na wananchi wake pamoja na wanaCCM wenyewe.Pia inatajwa imani za kishirikina,mwamba inasemekana yupo vizuri katika eneo hilo,hivyo wengi kuwa na uoga wa kumvaa na hata kuogopa kuchukua fomu.

Pamoja na Rais kumsema namna hasi,lakini bado jamaa ananguvu kubwa Kisesa.Sasa itakuaje wakati Mbunge huyu aliyetajwa kama Mbunge wa kitaifa akirudi kuchukua fomu na kurudisha peke yake

Ngoja tuone mwisho wa jambo hili.
Kama ni hivyo, basi kesho naenda kuchukua fomu huko.
 
Back
Top Bottom