Jimbo la Kiteto Tumepokea Fedha Kwaajili ya Miradi ya Maendeleo Kiasi cha Tsh. 965,280,029

Jimbo la Kiteto Tumepokea Fedha Kwaajili ya Miradi ya Maendeleo Kiasi cha Tsh. 965,280,029

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

JIMBO LA KITETO: TAARIFA KWA WANANCHI WA KITETO

TUMEPOKEA FEDHA KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO KIASI CHA SHS 965,280,029

Ndugu wananchi wenzangu wa Jimbo la Kiteto, nachukua fursa kuwafahamisha kuwa tumepokea fedha 965,280,029 Shs kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Nimezungumza na Mhe. Waziri wa Tamisemi, Mhe. Mohamed Mchengerwa na amethibitisha kuwa pesa zimetumwa na Mkurugenzi wetu CPA Hawa Hassan Abdul amenithibitishia kupokelewa kwa fedha hizo na kuwa fedha hizo zitatumwa katika Kata za Ndirigish na Makame bila kuchelewa. Mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:

1. Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Makame Kata ya Makame - Shs 584, 280,029

2. Ujenzi wa Mabweni, Madarasa na Vyoo Shule za Sekondari Ndirigish, Kata ya Ndirigish - Shs 381,000,000

Kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo la Kiteto, tunamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote Serikalini kwa kuendelea kuboresha maisha yetu Wana Kiteto kwa kuendelea kutuletea miradi mikubwa ya maendeleo na kushughulikia changamoto za wananchi katika wilaya yetu. Ahadi za CCM zinaendelea kutekelezwa.

Ndugu wananchi wenzangu wa Kiteto, tunayo kila sababu ya kutoa shukrani kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupa fedha nyingi kwa ajili ya kutatua miradi ya maendeleo. Tumwombe Mhe. Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan Mwenyezi Mungu ampe afya njema na kumlinda vyema ili aendelee na maono yake mazuri katika kujenga taifa letu.

Mhe. Rais wetu mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kusikia kilio chetu kupitia sauti yenu Bungeni.

Ndugu wananchi wenzangu, kwa dhati kabisa nawahakikishia kuwa nitaendelea kuwa sauti yenu Bungeni na kuwawakilisha ipasavyo kwa unyenyekevu na uaminifu mkubwa.

MUHIMU Natoa wito kwa watumishi wote kuhakikisha kuwa miradi hii inasimamiwa vizuri na kwa ufanisi mkubwa ili wananchi wapate huduma hizi kwa wakati.

Kiteto yetu inaendelea kung'ara!

Mungu Ibariki Kiteto!

Mungu Ibariki Tanzania!

Mungu ambariki Mhe. Rais wetu mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge

Edward Ole Lekaita Kisau
(Mbunge wa Jimbo la Kiteto)

Leo tarehe 24.6.2024

Kazi Iendelee
 
Back
Top Bottom