Jimbo la Ukonga wataka mabadiliko Ubunge, wamtaja Msama kuwa ni mpambanaji

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
435
Reaction score
733
Wakati vuguvugu la uchaguzi mkuu likipamba moto nchini kwa nafasi ya urais, ubunge na udiwani, wapiga kura wa Jimbo la Ukonga wamemtaja Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama kuwa ni mtu sahihi kwa 2025-2030.
Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo wanapoongelea uchaguzi wa mwaka huu, wamekuwa wakimtaja Alex Msama kwa maelezo kwamba anaweza kusimamia mambo yakaenda mbele.
Baadhi ya watu wamesema jimbo hilo liko nyuma kwa mambo muhimu, zikiwemo barabara za ndani kwa sababu ya kukosa mbunge sahihi anayesimamia maendeleo.
Jimy Matiku, mkazi wa Mombasa, amesema: "Mimi naamini katika majimbo hayana maendeleo hapa Dar es Salaam, Ukonga linaongoza. Au niseme ni jimbo la mwisho kwa maendeleo. Miundombinu mingi huku haiko sawa. Nimeona yule bwana Msama naye anataka ubunge. Naamini atatufaa."
Mkazi mwingine, Said Abuu, kinyozi wa Gongolamboto yeye alisema anatamani Ukonga impate mbunge kama Alex Msama. Akatoa sababu:
"Yule bosi aliweza kuratibu mambo ya dini (Tamasha la Pasaka) siku za nyuma na watu walikuwa wanajaa kwenye shughuli. Lakini pia ni mtu ambaye tuko naye bega kwa bega," alisema Abuu.
Naye Mwanaidi Sule, muuza mbogamboga na mkazi wa Madafu, alisema: "Ukonga tunatakiwa kumpata mbunge mpya. Tujaribu watia nia wapya ili tuone watatufikisha wapi kwa sababu waliyopita wamepita. Walichofanya wamefikia mwisho."
Wananchi wengi walitaja ubovu wa barabara jimboni humo kiasi cha kusema kuwa, wapo watu wanashindwa kufaidi magari yao kwa sababu ya ubovu wa barabara.
Anna Alfred, mkazi wa Chanika anasema kuwa, malalamiko ya ubovu wa barabara za jimbo hilo yaliwahi kuandikwa na baadhi ya vyombo vya habari lakini anaamini kunatakiwa mabadiliko ya mwakilishi.
"Wakati wa mvua barabara zinajaa maji. Hazipitiki. Nauli za daladala zinapanda au madereva wanakatisha safari kwa kukwepa ubovu wa barabara. Sasa kama tumekuwa na mbunge miaka yote amefanya nini?
"Tuliambiwa Tarura watafanikisha haraka sana kujenga barabara zote lakini hatujaona huo uharaka wao," alisema Anna.
Muuguzi Mariam Joseph anayeishi Pugu Kajiungeni na kufanya kazi Banana alisema tatizo la barabara katika jimbo hilo ni kama mtu aliyevaa nguo nzuri nje lakini ndani amevaa malapulapu.
"Ukipita barabara kuu ya kutoka mjini kwenda Chanika au kwenda Kisarawe utasema hata barabara za ndani mitaani ziko hivyohivyo lakini sivyo. Barabara ni tatizo sana. Hali hii imewafanya waendesha bodaboda au Bajaj kutoza nauli wanavyojisikia," alisema Mariam.
Katika vikao vya wazee wanakunywa kahawa huku wakibadilishana mawazo pale Mombasa, wengi walisema mabadiliko ya mwakilishi kwa mwaka huu wa 2025 ni muhimu huku wakimtaja Msama kama mpuliza filimbi wa kati katika kinyang'anyiro hicho.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliyokwisha chukua fomu na kurejesha kwa ajili ya kuomba ridhaa ya chama kugombea ubunge ni 11.
Baadhi yao ni; Alex Msama, William Mwila, Jerry Silaa na Alfred Tukiko.

IMG-20250125-WA0059(1).jpg
 
Huyu Msama aliyemdhulumu Rose Mhando na kumpiga kamati za ufundi na mapepo? Hivi wakati Jerry akiwa Waziri wa Ardhi kumbe ugomvi wao chanzo jimbo?
 
Ambakucha, wewe ni msama mwenyewe ama chawa wake.

Kama vyote sivyo basi hao wote uliowahoji ni MAZUMBUKUKU, bado yanaamini mbunge kuleta maendeleo.
.yote 9, 10 msama huyu si ndio aliwatapeli watu viwanja, kamtapeli rose muhando, atashindwa nini kuwatapeli wana ukonga?
 
Wakati vuguvugu la uchaguzi mkuu likipamba moto nchini kwa nafasi ya urais, ubunge na udiwani, wapiga kura wa Jimbo la Ukonga wamemtaja Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama kuwa ni mtu sahihi kwa 2025-2030.
Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo wanapoongelea uchaguzi wa mwaka huu, wamekuwa wakimtaja Alex Msama kwa maelezo kwamba anaweza kusimamia mambo yakaenda mbele.
Baadhi ya watu wamesema jimbo hilo liko nyuma kwa mambo muhimu, zikiwemo barabara za ndani kwa sababu ya kukosa mbunge sahihi anayesimamia maendeleo.
Jimy Matiku, mkazi wa Mombasa, amesema: "Mimi naamini katika majimbo hayana maendeleo hapa Dar es Salaam, Ukonga linaongoza. Au niseme ni jimbo la mwisho kwa maendeleo. Miundombinu mingi huku haiko sawa. Nimeona yule bwana Msama naye anataka ubunge. Naamini atatufaa."
Mkazi mwingine, Said Abuu, kinyozi wa Gongolamboto yeye alisema anatamani Ukonga impate mbunge kama Alex Msama. Akatoa sababu:
"Yule bosi aliweza kuratibu mambo ya dini (Tamasha la Pasaka) siku za nyuma na watu walikuwa wanajaa kwenye shughuli. Lakini pia ni mtu ambaye tuko naye bega kwa bega," alisema Abuu.
Naye Mwanaidi Sule, muuza mbogamboga na mkazi wa Madafu, alisema: "Ukonga tunatakiwa kumpata mbunge mpya. Tujaribu watia nia wapya ili tuone watatufikisha wapi kwa sababu waliyopita wamepita. Walichofanya wamefikia mwisho."
Wananchi wengi walitaja ubovu wa barabara jimboni humo kiasi cha kusema kuwa, wapo watu wanashindwa kufaidi magari yao kwa sababu ya ubovu wa barabara.
Anna Alfred, mkazi wa Chanika anasema kuwa, malalamiko ya ubovu wa barabara za jimbo hilo yaliwahi kuandikwa na baadhi ya vyombo vya habari lakini anaamini kunatakiwa mabadiliko ya mwakilishi.
"Wakati wa mvua barabara zinajaa maji. Hazipitiki. Nauli za daladala zinapanda au madereva wanakatisha safari kwa kukwepa ubovu wa barabara. Sasa kama tumekuwa na mbunge miaka yote amefanya nini?
"Tuliambiwa Tarura watafanikisha haraka sana kujenga barabara zote lakini hatujaona huo uharaka wao," alisema Anna.
Muuguzi Mariam Joseph anayeishi Pugu Kajiungeni na kufanya kazi Banana alisema tatizo la barabara katika jimbo hilo ni kama mtu aliyevaa nguo nzuri nje lakini ndani amevaa malapulapu.
"Ukipita barabara kuu ya kutoka mjini kwenda Chanika au kwenda Kisarawe utasema hata barabara za ndani mitaani ziko hivyohivyo lakini sivyo. Barabara ni tatizo sana. Hali hii imewafanya waendesha bodaboda au Bajaj kutoza nauli wanavyojisikia," alisema Mariam.
Katika vikao vya wazee wanakunywa kahawa huku wakibadilishana mawazo pale Mombasa, wengi walisema mabadiliko ya mwakilishi kwa mwaka huu wa 2025 ni muhimu huku wakimtaja Msama kama mpuliza filimbi wa kati katika kinyang'anyiro hicho.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliyokwisha chukua fomu na kurejesha kwa ajili ya kuomba ridhaa ya chama kugombea ubunge ni 11.
Baadhi yao ni; Alex Msama, William Mwila, Jerry Silaa na Alfred Tukiko.

View attachment 3408421
Sasa ukipewa hiyo nafasi si utaishia tu kuwatapeli wananchi viwanja na nyumba zao! Au unataka kusema utaacha kweli utapeli ndugu Msama promotion!!
 
Jerry slaa kijana makini kabisa ardhi aliinyoosha haswa arudi Tena bungeni ana kitu atafika mbali.matatizo ya barabara mbovu ni janga la kitaifa sio ukonga tu
 
Msama ni wa kumlinganisha na Jerry Slaa mhhh, huku ni kumtukana Jerry.
 
akipata kura mbili moja ni yake yapili yakwako
 
Back
Top Bottom