Jimmy Mponda, Ni Uadilifu, Nidhamu au hajafikia Ustaa?

Jimmy Mponda, Ni Uadilifu, Nidhamu au hajafikia Ustaa?

mbotoki

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2015
Posts
268
Reaction score
115
Imekuwa ni kawaida sana kwa wasanii wetu wa tasnia mbalimbali kufanya mambo fulani au hata vioja na kupelekea majina yao kutengeneza headlines katika vyombo mbali mbali vya habari (wengine nasikia hufikia hatua hata ya kutengeneza visa au hata kutoa fedha kwa waandishi ili tuwasikie na kuwasoma) na hivyo hujikuta majina yao hayakauki vinywani mwetu na kuzidi kuwaona mastaa.

Kuna jamaa mmoja anaitwa Jimy Mponda, jamaa huyu leo nimetazama movie zake za kibabe flani hivi, mie mwenyewe zikanipendeza kimtindo.

Nasikia ameshacheza movie kama;

- Shamba kubwa. Unga adui. Misukosuko.
- Double J.

E bana eh jamaa sijawahi kumuona gazetini wala kumsikia redioni. Labda nyinyi wenzangu. Ila muuzaji wa DVD aliniambia jamaa anauza sana kazi zake. Anatumia pia jina la Jimy Master.

Hapo nikajiuliza sasa kumbe bila mastory unaweza piga biashara ya kazi za sanaa?

Au ni uadilifu na nidhamu? Wito wangu kwa wasanii wengine wafuate mfano huu, na kwa sasa mascandal tuwaachie wakulima na watu wa Politiki.
 
Jamaa haongelewi sana kwenye media hasa magazetini ila namkubali pamoja na yule mwenzio afande Seba.

Anyhow......promo ina umuhimu wake ili kazi iuzike kwa wingi na msanii kutengeneza jina pia kuongeza fan base.

Kwa huyu jamaa huenda hana vituko/scandal "pendwa" na kina Shigongo!
 
Huyu ndo muigazji wa ukweli na DVD zake zinastahili kuuzwa hata elfu tano lakini waliobaki dvd zao nadhani hata jero ni sahihi.
 
Anajua anachokifanya, Ndio maana hata movie zake hakuna Ujinga Ujinga.!
 
Kweli tunatofautiana mimi movie zake na za huyo sijui afande seba siwezi ziangalia mwanzo mwisho, jambazi lazima avae sun glasses, avae koti refu, akunje sura.
Zinanichekesha hadi naona aibu kuendelea kuziangalia.
 
Back
Top Bottom