Jina halisi la msanii Ravany (Raymond) ni lipi?

enockino

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2014
Posts
273
Reaction score
171
Msaada anayejua jina halisi la msanii Ravany ( Raymond wa kundi la WCB)

Au short history ya huyu msanii.
 
Anaitwa Raymond Hvyohvyo,jina la babake silijui..
Kabila ni Mnyakyusa..
Anatokea Iyunga,Mbeya..(ndipo wanapoishi wazazi wake na alipokuwa anaishi yeye)..

Alikuwa msanii underground Mbeya wa Miondoko Ya Rap,akashinda shindano lililoandaliwa na Clouds Fm la Freestyle ambapo Judge alikuwa Marehemu Albert Mangwea mwaka 2012,.
Zawadi za ushindi huo ilikuwa ni kurekodi bure kwa Mako chali(Mj Records) na kusainiwa na TipTop..

Baada ya ushindi huo akachukuliwa na Tiptop na kuja dar,katoa nyimbo za rap si chini ya 10 akiwa Tiptop ila hakutoka,akabaki kuwa mbeba mabegi wa madee kwenye show alizokuwa anapiga madee..

Baadae Alikutana Na Diamond Kupitia kwa Msanii Wa Yamoto Band Anaeitwa Maromboso(msanii ambae diamond anamkubali kuliko wote waliopo Yamoto band),,kwa kutambulishwa ni kuwa ni kichwa wa Utunzi Na Anawasaida wao kuandika mistari..baada ya Diamond kushuhudia ubora wake akawa na mtindo wa kuzunga nae maeneo mbalimbali anayopiga show na kumtumia kumsaidia kuandika mashairi ya baadhi ya nyimbo zake..mpaka akaja kumchukua jumla na kumsaini kwenye Label yake..

Akashauriwa aache kuchana na kuanza kuimba ndipo akarekodi wimbo wa Kwetu aliosaidiwa kuandika Mashairi Na Quen Darleen na Tudd Thomas..
 
Kwani nayeye anahusika na Unga??
Jina lake halisi lanini??? Mnataka mliandike kwenye list sio????
 
Anaitwa Raymond Shaban Mwakyusa..ana umri wa miaka 26,kabila ni Mnyakyusa wa Mbeya..Inatosha
 
Anaitwa Raymond Hvyohvyo,jina la babake silijui..
Kabila ni Mnyakyusa..
Anatokea Iyunga,Mbeya..(ndipo wanapoishi wazazi wake na alipokuwa anaishi yeye)..

Alikuwa msanii underground Mbeya wa Miondoko Ya Rap,akashinda shindano lililoandaliwa na Clouds Fm la Freestyle ambapo Judge alikuwa Marehemu Albert Mangwea mwaka 2012,.
Zawadi za ushindi huo ilikuwa ni kurekodi bure kwa Mako chali(Mj Records) na kusainiwa na TipTop..

Baada ya ushindi huo akachukuliwa na Tiptop na kuja dar,katoa nyimbo za rap si chini ya 10 akiwa Tiptop ila hakutoka,akabaki kuwa mbeba mabegi wa madee kwenye show alizokuwa anapiga madee..

Baadae Alikutana Na Diamond Kupitia kwa Msanii Wa Yamoto Band Anaeitwa Maromboso(msanii ambae diamond anamkubali kuliko wote waliopo Yamoto band),,kwa kutambulishwa ni kuwa ni kichwa wa Utunzi Na Anawasaida wao kuandika mistari..baada ya Diamond kushuhudia ubora wake akawa na mtindo wa kuzunga nae maeneo mbalimbali anayopiga show na kumtumia kumsaidia kuandika mashairi ya baadhi ya nyimbo zake..mpaka akaja kumchukua jumla na kumsaini kwenye Label yake..

Akashauriwa aache kuchana na kuanza kuimba ndipo akarekodi wimbo wa Kwetu aliosaidiwa kuandika Mashairi Na Quen Darleen na Tudd Thomas..
Anatokea Nzovwe Mbeya. Na kasoma elimu yake ya O level shule ya Nzondahaki Secondary School.
 
Back
Top Bottom