Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa kiluga chetu, mdudu huyo anaitwa kobe.
mimi nlimfuga siku tatu nlipokua darasa la tano akaja akantoroka. mia
Inkuru-Kikurya
Mbulumundu huyo Kiluguru
Kimbofya huyo Kichagga
mmh...uyu naye. kobe si kiswaili icho. nimesema naomba viluga.
Kwa hiyo kiswahili sio kiluga?
Viluga ni nini?
Huelewi kuwa kiswahili ni luga ya waswahili?
Kimakonde ni lug(h)a ya wamakonde.
Kinyamwezi ni kiluga ka wananyamwezi. Kihehe, kichaga ...
Kiswahili kimepewa hadhi ya kuwa kiluga/lugha ya Taifa vilevile lakini haiondoi kuwa kenyewe ni kiluga pia.
Cameroun anaitwa Etoo'
aah bwana ondoka hapo unanchanganya mie!
lung,umbe-sukuma
ng,olombe-kiha
ng,ung,umbe-fipa
ifwammbo-kinyanja
ink,imah-mambwe(zambia)
Fugwe=kiha leka tutigite
Nilifikiri unapata shule...haya bana usijichanganye.
Kiswahili si kiluga bali ni liluga!
....
Basi alitokea mama mmoja kabeba uyu mdudu kwenye kapu la kusuka (yale makapu ya vipande vya matete ambayo karibu kila kabila la kibantu wanajua kusuka). Si watu walianza kunyang'anyiana wanataka kununua---eti chakula! Aise.....nilishangaa?!
Unashangaa watu kula uyo mdudu?
Umeshaona watu wa Tanzania wanaokula wo,wo,woh(mbuzi wa Mbeya)? https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/273150-nimekula-nyama-ya-mbwa-5.html
Wanaokula nyoka je? Wanaokula panya?. mamba? mende? vyura? utumbo wa ng'ombe, mbuzi.kuku? wanaokula nguruwe?
Kuna mdudu ambaye haliwi ulimwengu huu? usifungue links kama una moyo!
Binadamu analiwa link Some Thailand Cannibals 'Eating' A Human (Gruesome Pictures - Viewers Discretion Advised!) - Ethnic, Racial, Or Sectarian Politics - Nairaland
link Thai Cannibal Kills And Eats Sons Thought They Were Pigs - Wazaap!
Aise mineogopa kufungua izo links nina kikombe cha kahawa hapa mezani.
Ila nikupe hii: kule kwetu panya ni chakula muhimu sana jamaa yangu. na mimi hii leo ukinipatia panyapori, namuoka vizuri, namnyunyizia chumvi na pilipili halaf namla wakati ukiangalia. Wala sitakuwa na chembe moja ya aibu! Wale panyapori ni watamu aise. Miaka ya 1960 wakati nakua kijijini moja ya stadi za maisha ilikuwa kujua mitego mbalimbali. Kabila langu tuna historia ya uwindaji, ufugaji na kilimo. Mimi nilikuwa fundi wa mitego ya panya, ndege njiwa na kware. Bibi yangu mzaa baba alikuwa fundi sana wa mitego ya ndege kwa ulimbo. Alinifundisha ufundi ule. Sema sasa nimeishajichanganya sana hapa dar ufundi ule unapotea sasa.
Sasa mkuu
Kama unakula panya pori, kwa nini ulishangaa watu wanaotaka kununua kobe kama mboga/kitoweo(nyamachoma)? Soma post #32 .
Mimi hapa ninapoishi niko karibu na pori na panya wanakuja hapa nyumbani kunitembelea. Nitakualika uje utege mitego yako ili tutengeneze nyamachoma(kuoka msosi wa nguvu).
hilo nalo neno mkuu wangu.
Mboga mbili naweza kula na ugali mkubwa nikaumaliza pasipo shida
ni Mlenda, au panyapori. Itabidi tu uniPM nijue unaishi karibu na pori gani.