Jina la mji wa Magufuli limefutwa? - Mwandishi ahoji

Jina la mji wa Magufuli limefutwa? - Mwandishi ahoji

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Baada ya hotuba ya Waziri Mhe. Kabudi, mbele ya waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa Mji wa Serikali, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, mwandishi wa habari Awadhi Omary kutoka KANIKI TV ameibua hoja kuhusu jina la Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika kipindi cha maswali na majibu, Awadhi Omary alihoji sababu za hotuba hiyo kutotaja jina la Hayati Rais Magufuli, ambaye amekuwa akihusishwa na uanzishwaji na ujenzi wa Mji wa Serikali, huku akieleza kuwa jina la Magufuli City au Mji wa Magufuli limekuwa likitumika katika mazoea ya wengi wanapoutaja mji huo.

Swali hilo limeibua hoja kuhusu utambuzi wa mchango wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika kuanzisha na kusimamia utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kimkakati wa Serikali.

Wewe kama mdau unahisi jina la Magufuli City litaendelea kuwepo au ndo imeisha hiyoo 🤔 🤔

 
Back
Top Bottom