Jina la mtoto limekosewa kwenye matokeo ya darasa la saba, msaada wa nini chakufanya

Jina la mtoto limekosewa kwenye matokeo ya darasa la saba, msaada wa nini chakufanya

JMF

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
1,758
Reaction score
2,770
Salaam wanajukwaa la sheria.
Nina changamoto hiyo hapo juu, nimeileta jukwaa hili kupata ushauri wa nifuate utaratibu gani mwanangu aanze kidato cha kwanza na jina lake lilolopo kwenye cheti chake cha kuzaliwa. Limekosewa herufi mbili hivyo naona kabisa ataingia nalo form one na litakuja kusumbua kwenye vyeti mbeleni. Kwa sasa nifanye nini kurekebisha hilo? Msaada tafadhali.
 
Anatakiwa kupata Affidavit ya majina.
 
Mwisho wa kubadilisha Jina/majina ni kidato cha tatu.

Hivyo mtoto akishaingia kidato cha kwanza tu, nenda shule husika waambie unahitaji kubadilisha majina ya mtoto yaendane na unavyoona wewe

Ni rahisi sana ndugu mzazi
Sawa mwalimu
 
Shukrani sana mkuu
 
mkuu JMF mbona hujaweka wazi hilo jina limekosewa kwenye document ipi cheti cha kuzaliwa,cheti cha kumaliza darasa la saba au kwenye matokeo ya mtihani wa taifa wa Necta? na kama jina lake sahihi lipo kwenye cheti cha kuzaliwa ww kama mzazi ulimuandikisha darasa la kwanza kwa kukosea jina je,hukujua au ulipotezea tu why ushtuke sasa, ina maana miaka yote saba alitumia hilo jina lilikosewa au imetokea jina limekosewa darasa la saba tu pia mtihani wa taifa darasa la nne alitumia jina lipi na vp NECTA wanalitambua jina lipi ambalo wametolea matokeo yake ya mtihani je, lilikosewa au la cheti za kuzaliwa.?
 
Kajaze fomu ya affidavit of confirmation of names.
Ukifanya hivo basi majina yote mawili hilo lilopo kwenye matokeo na la cheti cha kuzaliwa yatatambulika kama majina ya mtoto.
 
Back
Top Bottom