Jina la "Ukuta wa Yericko " ni jina ambalo limekwenda kuficha uozo wa mabeki wa Simba SC

Jina la "Ukuta wa Yericko " ni jina ambalo limekwenda kuficha uozo wa mabeki wa Simba SC

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Simba sc imekua ikiruhusu magoli kirahisi sana (mepesi) Tena magoli mengine ni uzembe wa mabeki waliopewa jina kubwa kuliko uwezo wao (Ukuta wa Yericko).

Nimesikitishwa na mashabiki walioanza kumlaumu kipa Ayubu na kusema siyo kipa baada kufungwa goli la pili kwenye mechi dhidi ya Power dynamoo.

Lakini hakuna aliyepiga makelele na kusema kuwa beki wa kimataifa mcheza na jukwaa (inonga bacca) ndiyo alilitumbukiza kambani goli la kwanza kwa kua ni beki mcheza na majukwaa Hilo siyo tatizo.

Kuanzia beki namba mbili, tatu na mabeki wa kati Kuna shida kubwa sana katika uzuiaji na ukabaji wa mipira.

Jina "Ukuta wa Yericko" limeficha makosa makubwa sana ya mabeki, unakuta beki anafanya makosa lakini kwa kuwa kichwani Kuna neno Ukuta wa Yericko unakuta mashabiki wanatafuta mchawi mwingine na kuacha Ukuta wa biskuti ulioziba shimo la panya.

Kwa Ukuta huu wa Yericko unaoimbwa na kupambwa sidhani Kama utaweza kumzuia Al ahly.
 
KILA NENO LITASEMWA HUU UZI ULIMALIZA KILA KITU.

Nilikuunga mkono,
Ninakuunga mkono,
Nitakuunga mkono.
 
Simba sc imekua ikiruhusu magoli kirahisi sana (mepesi) Tena magoli mengine ni uzembe wa mabeki waliopewa jina bwa sidhani Kama utaweza kumzuia Al ahly.
Kwa mfuatliaji makini hawezi kukupinga. Simba kiulinzi ina tatizo kubwa zaidi ya Kapombe na Zimbwe. Combination ya Malone na Inonga inahitaji marekebisho Makubwa Kwa sababu wote wanacheza style inayofanana na kusababisha beki nzima kukosa utulivu.

Makosa mengi ya Inonga msimu uliopita yalifichwa na Mtu Chuma na yeye aliposhindwa lawama zote zikwangukia yeye bila watu kukumbuka tatizo lilipoanzia. Humu imekuwa kama dhambi kumsema Inonga, sidhani kama mashabiki wa Simba wanaomkosoa JF wanazidi 3.
 
Kwa mfuatliaji makini hawezi kukupinga. Simba kiulinzi ina tatizo kubwa zaidi ya Kapombe na Zimbwe. Combination ya Malone na Inonga inahitaji marekebisho Makubwa Kwa sababu wote wanacheza style inayofanana na kusababisha beki nzima kukosa utulivu. Makosa mengi ya Inonga msimu uliopita yalifichwa na Mtu Chuma na yeye aliposhindwa lawama zote zikwangukia yeye bila watu kukumbuka tatizo lilipoanzia. Humu imekuwa kama dhambi kumsema Inonga, sidhani kama mashabiki wa Simba wanaomkosoa JF wanazidi 3.
Hili halikusemwa kabisa ila tukiwa banda umiza nilimwambia jirani yangu, hii combination ya Inonga na Malogne haifai kwa sababu inaonekana hakuna wa kumtuma mwenzake, na kuna muda wanakaa mstari mmoja. Haikuchukua muda goli likaingia.

Ukiangalia lile goli, alikuwa ni kama vile Malogne alikuwa ndani ya kumi na nane anamfuata mshambuliaji wa Dynamo nyuma, huku Inonga akienda pembeni kuzuia krosi baada ya Kapombe kuachwa. Cha ajabu Malogne akamuacha yule mshambuliaji, na Inonga akashindwa kuzuia ile krosi na ikamkuta mshambuliaji wa Dynamo akapiga mpira akiwa huru kabisa. Kwa nini Malogne hakumkaba mpaka mwisho yule mshambuliaji ili kumbughuzi asipige kirahisi?
 
Wenye timu Yetu Tumetulia Kimya.... Timu mpaka muda huu ipo Vizuri , Inaendelea Kuelewana Kazi Mbele kwa mbele...

Sasa Utopolo ndio Viherehere... Mara Robertino, mara Kapombe ,mara Inonga ,mara Che Malon.....

Baada ya Xmas itajulikana Wapi pabovu..
Nani ana beki fupi fupi...
Nani ana viungo bora...
 
ME NNACHOJUA UKUTA WA YERIKO ULIDONDOSHWA NA KELELE ZA TARUMBETA, HAYO MENGINE SITAKI KUJUA
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
1694971501705.jpg
 
Huyo mnayemuita ukuta wa Yeriko ukimchungunza kwa makini utaona ni mzuri kublock mipira yaani one v one kumpita huwa ni ngumu. Udhaifu wake sasa, jamaa anakuwa overconfident to the extent anaexpose makosa kibao hususani anapokuwa na mpira Passing zake hususani katika eneo lake huwa zinatia shaka. Na akiendelea hivyo balls in the net zitaokotwa sana.
 
Che malone ni mzito sana hasa akiwa na mpira akifanyiwa presha uwa hajiamini anapoteza mipira kilrahisi.

Mechi na Mtibwa alifanyiwa presha akafungisha, kule Zambia na apa Dar amefanyiwa presha na kupoteza mipira kwenye maeneo ya hatari zaidi ya mara moja bahati yake haja adhibiwa.

Kwenye hatua za uko mbele kama ataendelea kuwa mzito, jumba bovu liko njiani kumwangukia.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom