Na mimi ndicho nilichomaanisha ...
Ila nimecheka leo yaani hadi kinjekitile alikuwa sheikh aliyetoka kuhiji mecca na wenzie hadi kuleteana na maji ya zamza ili wapate baraka za allah [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Nimeamini hakuna ulevi mbaya kama wa dini
Eyce,
Unasema hayo kwa kuwa huijui historia ya Maji Maji.
Nami wala sikulaumu nitakachofanya ni kukuonyesha ili uifahamu historia ya watu hawa.
Nakuwekea hapa nukuu kutoka kwa wanahistoria Wazungu walivyomwandika Songea Mbano
tena kwa kumtaja kwa jina la Rauf:
''This letter written to Sheikh and Sultan Mataka bin Hamin Massaninga reads:
Sultan Songea bin Ruuf writes: To the Shaykh and Sultan Mataka bin Hamis Massaninga. Greetings, etc. I am sending you a letter through Kazembe. We have received an order from God that the Europeans must leave the country. We are in the process of fighting them here. I believe that we have long since been reconciled,[so] send me your children, so that we may make an alliance. I had wanted to send you some cattle as a gift, but am not able to
do so, as the war which God desired is continuing. Send me a hundred riflemen, and support me in storming the Boma (Songea).
I am also sending you a flask of the Prophet Muhammad, which contains the means for conquering the Europeans. Have no doubt about it, it possessed great power. And when we have taken the Boma (Songea), we shall go on the stations on the Nyasa together, you and I. Now, let us forget our old quarrels.
This bottle, with a da’wa, has been sent by Chinyalanyala himself, the war leader. He also sends the container (kombe), and sends you many greetings.
If your men will come, then Chinyalanyala himself will come and will give you many of the holy things.
Hassan bin Isma’il greets you.
Many salutations,
Sultan Songea bin Ruuf.” [1]
[1] C.H. Becker, ‘Material for the Understanding Islam in German East Africa’,
Tanzania Notes and Records, No. 68, February, 1968, p.58.
Barua hii aliyoandikiwa Sheikh, Sultan Mataka bin Hamin Massaninga inasema:
Sultan Songea bin Ruuf anasema: Kwa Sheikh Sultan Mataka bin Hamin Massaninga. Asalaam Aleikum, Ninakuletea barua kupitia Kazembe. Tumepata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa Wazungu lazima waondoke nchini. Tupo katika kupigananao hapa. Naamini tumeshapatana muda mrefu, (kwa hiyo) niletee wanao, ili tufanye ushirikiano. Nilitaka kukuletea mifugo kama zawadi, lakini sipo katika hali ya kuweza kufanya hivyo, kwa kuwa vita ambavyo Mwenyezi Mungu amevitaka vinaendelea. Niletee watumiaji bunduki mia moja, na niunge mkono katika kulivamia Boma (Songea).
Ninakuletea chupa ya Mtume Muhammad, ambayo ndani yake ipo nguvu ya kuwashinda Wazungu. Usiwe na shaka nayo, ina uwezo mkubwa. Tutakapoliteka Boma (Songea), tutakwenda kwenye vituo katika Nyasa pamoja, mimi na wewe. Hivi sasa tusahau ugomvi wetu wa zamani.
Chupa hii, na dawa, imeletwa na Chinyalanyala mwenyewe, kiongozi wa vita. Ameleta vilevile kombe, na anakupa salamu nyingi.
Endapo watu wako watakuja, Chinyalanyala mwenyewe atafika na atakupa vitu vingi vilivyo vitukufu.
Hassan bin Ismaíil anakusalimu.
Salam nyingi,
Sultan Songea bin Ruuf.
Eyce,
Sasa kitu cha kushangaza ni kuwa hawa majemadari wote waliotajwa katika
barua hii walinyongwa lakini majina haya yote yaliondolewa katika ile
orodha ya awali iliyokuwapo katika Makumbusho ya Vita Vya Maji Maji.
Kwa kufanya hivyo historia yote imepotezwa.