Jina lake ni Abdulrauf Songea Mbano siyo Songea Mbano Sultani wa wangoni wakati wa vita vya Majimaji 1905 - 1907

Eyce swali ninalouliza mimi ni kwa nini pamekuwa na juhudi za kufuta majina ya Kiislamu?

Ikiwa hujui sababu basi si lazima ujadili.
Huwezi kuendelea kung'ang'ania ni majina ya kiislamu kama huwezi kudhihirisha uislamu wao kwa kuyajibu maswali yangu na kwa nini yawe ni majina ya kiislamu na si kiarabu !!!!!........

Ni nani mwenye jitihada hizo ????....

Kama kungekuwa na jitihada hizo mbona mpaka miaka ya 2000 mliikuta hiyo historia ambayo ni miaka 100 baada ya hiyo vita kutokea na zaidi ya miaka 40 ya tanganyika kupata uhuru wake !!!!......

Toka nimezaliwa hadi kufikia umri huu sijawahi kusikia jina la chief wa kihaya au makabila ya kanda ya ziwa yakiandikwa kwa majina ya kiingereza ambayo walikuwa nayo lakini yalikuwa ni utambulisho tu pasi na kuwa na heshima kimila ama kijamii...
Pamoja na hii hali sijawahi kusikia popote wakristo wakipigania hayo majina kuwa historia iliyameza au kuyafuta makusudi
Je, kwa nini iwe kwa waislamu tu na si wakristo ????........
 
Eyce sina tatizo na fikra zako lakini huko Uhayani wakati natafiti historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika nimekuta majina haya: Sued Kagasheki, Abdallah Rutabanzibwa, Ali Migeyo kwa kutaja majina machache...

Mohamed Said: Search results for ali migeyo
 
Eyce sina tatizo na fikra zako lakini huko Uhayani wakati natafiti historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika nimekuta majina haya: Sued Kagasheki, Abdallah Rutabanzibwa, Ali Migeyo kutaja machache...
Mohamed Said: Search results for ali migeyo
Hongera sana kwa kupata majina hayo kwa maana hata ukienda muleba kagera ...kuna nshamba ambayo ni kama ngome ya waislamu na Rubya ambayo ni ya wakristo hivyo uhayani kuna hizo zote mbili

Lakini nimejua kitu kuwa upo biased sana na huoni kingine katika historia zaidi ya uislamu na mbaya zaidi hujibu maswali zaidi kuing'ang'ania misimamo ambayo haina fact kama sharia ...... wewe ni mtu mwenye akili sana lakini udini kwa kiasi fulani umekulevya ila jua tu kuwa hata waliopandikiza mbegu ya mauaji ya Rwanda hawakujua kuwa wanaandaa mauti ya watu hapo mbeleni ...

Unachokitengeneza ni kama bomu la wahutu kuwa wao wana stahiki zaidi kihistoria hivyo wanapaswa kupata more kuliko wengineo na usidhani hizo historia unazoziandika zinaishia pale unapokomea wino wako bali zinaganda na kuleta maafa katika kizazi kijacho...
Mungu wangu ni wa amani na ninaomba akufunulie mazuri ya hekima katika uzee wako ili upate kuona ni kizazi gani unakiandaa
 
Eyce,
Hakika katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika Waislam walitawala.

Kama wewe una historia nyingine kinyume ya hii tuwekee tusome.
 
Jina majimaji halitokani nakuamini ukisema maji risasi zinakua maji huo niuongo wa mchana kweupe.bali ktk wapiganaji wavita kuna waliotoka kuhiji makka walirudi namaji ya zamzam,ndio wakawa wanaambiana tunywe maji yazamza tupate baraka.ndio likapatikana jina lamajimaji.namiongoni mwao hao waliotoka makka ni shekh kinjeketile.nawala sio mganga kama ulivyoongopewa.
 
Wewe ni ktk wale wanaoamini waarabu walikua wanawafunga minyororo waafrika nakuwapeleka masokoni kama nyanya vile au mbuzi èee?sasa hapa tumia akili ndogo tu!nikwanini waafrika hatuna ktk histori yetu sehemu inayoonyesha tumewahi kupigana vita nawaarabu?na kinyume chake tukapigana na wazungu?bara lote laafrika sio ukanda huu tu!nitafutie ktk usomi wake.yaani alietufunga minyororo hatujapigana nae ila aliekua anatujengea reli na mahospitali tukapigana nae!!!mmmm haya nimatango yaulaya
 
Mmmmmh
 
Ukweli ni upi kuhusu utawala wa waarabu?
 
Mi ninavyojua waarabu walikuja wakawakuta hawa watawala wana majina yao ya asili,walipokuja hao waarabu ndipo walipokuja na hayo majina ya kidini ikiwa ni pamoja na kuineza dini yao,kwa vyovyote hayo majina ya kiislamu yaliotajwa kwenye mada ni huenda walipewa tu na hao waarabu na sio majina halisi waliozaliwa nayo
 
mpk leo zanzibar wanatoa shule za mwsho 6/7 ktk top10 za shule zilizofanya vibaya.kusini ndo usiseme huko...21st C bado una na blaming game,hizo hazitawafikisha popote take initiatives...wacha porojo za kkoo huu co wakati wake.
 
Mkuu,uwe unaandika kwa facts,achana na udini,madai yako hayana historical/scientific proof
 
sasa ilunga atatoa kitu gani kipya wakati ni mfia dini kama wewe..yeye mpaka anakufa anazurura analalamika et anaonewa mfumo kristo...porojo zake angejenga hata nursery.
 
kwel ww pumbav dini imekufanya uwe fala mpaka unakataa ukweli.
 
Na mimi ndicho nilichomaanisha ...
Ila nimecheka leo yaani hadi kinjekitile alikuwa sheikh aliyetoka kuhiji mecca na wenzie hadi kuleteana na maji ya zamza ili wapate baraka za allah [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

Nimeamini hakuna ulevi mbaya kama wa dini
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] usishangae,utakuja utafiti mwingine utaambiwa yale yalikua ni maji ya baraka kinjektile alikua padre alitoka nayo Roma
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] usishangae,utakuja utafiti mwingine utaambiwa yale yalikua ni maji ya baraka kinjektile alikua padre alitoka nayo Roma
Hahaaaaaa hata hili jina la kinjikitile litakuwa si sahihi kabisaaa...

Watu watofautishe FACTS na OPINIONS...
Sijawahi kuona mtu anapinga uwepo wa utumwa katika pwani ya Afrika mashariki yaani makumbusho ya masoko yote ya utumwa yaliyopo ;bado kuna mtu anaamini huu ni uzushi ilhali anakubali kuwa ukoloni ulikuwepo pasipo kujua kuwa utumwa ulikufa kutokana na maandalizi ya ukoloni katika Afrika......

Ukristu sio uzungu na uarabu si uislamu ...sijui ni nini kigumu watu kuelewa
 
Ni kweli,tukisema kwamba biashara ya utumwa haikuwepo wakati vielelezo vipo ni kujifanya tu kichwa ngumu
 
Eyce,
Unasema hayo kwa kuwa huijui historia ya Maji Maji.
Nami wala sikulaumu nitakachofanya ni kukuonyesha ili uifahamu historia ya watu hawa.

Nakuwekea hapa nukuu kutoka kwa wanahistoria Wazungu walivyomwandika Songea Mbano
tena kwa kumtaja kwa jina la Rauf:

''This letter written to Sheikh and Sultan Mataka bin Hamin Massaninga reads:

Sultan Songea bin Ruuf writes: To the Shaykh and Sultan Mataka bin Hamis Massaninga. Greetings, etc. I am sending you a letter through Kazembe. We have received an order from God that the Europeans must leave the country. We are in the process of fighting them here. I believe that we have long since been reconciled,[so] send me your children, so that we may make an alliance. I had wanted to send you some cattle as a gift, but am not able to

do so, as the war which God desired is continuing. Send me a hundred riflemen, and support me in storming the Boma (Songea).

I am also sending you a flask of the Prophet Muhammad, which contains the means for conquering the Europeans. Have no doubt about it, it possessed great power. And when we have taken the Boma (Songea), we shall go on the stations on the Nyasa together, you and I. Now, let us forget our old quarrels.

This bottle, with a da’wa, has been sent by Chinyalanyala himself, the war leader. He also sends the container (kombe), and sends you many greetings.

If your men will come, then Chinyalanyala himself will come and will give you many of the holy things.

Hassan bin Isma’il greets you.

Many salutations,

Sultan Songea bin Ruuf.” [1]

[1] C.H. Becker, ‘Material for the Understanding Islam in German East Africa’, Tanzania Notes and Records, No. 68, February, 1968, p.58.

Barua hii aliyoandikiwa Sheikh, Sultan Mataka bin Hamin Massaninga inasema:

Sultan Songea bin Ruuf anasema: Kwa Sheikh Sultan Mataka bin Hamin Massaninga. Asalaam Aleikum, Ninakuletea barua kupitia Kazembe. Tumepata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa Wazungu lazima waondoke nchini. Tupo katika kupigananao hapa. Naamini tumeshapatana muda mrefu, (kwa hiyo) niletee wanao, ili tufanye ushirikiano. Nilitaka kukuletea mifugo kama zawadi, lakini sipo katika hali ya kuweza kufanya hivyo, kwa kuwa vita ambavyo Mwenyezi Mungu amevitaka vinaendelea. Niletee watumiaji bunduki mia moja, na niunge mkono katika kulivamia Boma (Songea).

Ninakuletea chupa ya Mtume Muhammad, ambayo ndani yake ipo nguvu ya kuwashinda Wazungu. Usiwe na shaka nayo, ina uwezo mkubwa. Tutakapoliteka Boma (Songea), tutakwenda kwenye vituo katika Nyasa pamoja, mimi na wewe. Hivi sasa tusahau ugomvi wetu wa zamani.

Chupa hii, na dawa, imeletwa na Chinyalanyala mwenyewe, kiongozi wa vita. Ameleta vilevile kombe, na anakupa salamu nyingi.

Endapo watu wako watakuja, Chinyalanyala mwenyewe atafika na atakupa vitu vingi vilivyo vitukufu.

Hassan bin Ismaíil anakusalimu.

Salam nyingi,

Sultan Songea bin Ruuf.

Eyce,
Sasa kitu cha kushangaza ni kuwa hawa majemadari wote waliotajwa katika
barua hii walinyongwa lakini majina haya yote yaliondolewa katika ile
orodha ya awali iliyokuwapo katika Makumbusho ya Vita Vya Maji Maji.

Kwa kufanya hivyo historia yote imepotezwa.
 
sasa ilunga atatoa kitu gani kipya wakati ni mfia dini kama wewe..yeye mpaka anakufa anazurura analalamika et anaonewa mfumo kristo...porojo zake angejenga hata nursery.
Lukubuzo,
Unaandika kwa ghadhabu na hamaki zinatoa utamu wa mjadala.

Unatumia maneno ya kifedhuli, ''mfia dini,'' hapana haja ya haya.

Tujadiliane kwa heshima na staha ili sote tufaidike katika mjadala
huu.

Ilunga si kuwa alikuwa na chekechea bali alikuwa na sekondari na
madras pia akisomesha dini.

Ilunga ni alim, yaani msomi hawezi kuwa mtu wa porojo.

Mimi nilikuwa kila nikiwa Mwanza nahudhuria darsa zake kuongeza
elimu.

Nakuwekea picha ya Sheikh Ilunga niliyompiga shuleni kwake mwaka
2010 akisomesha:

Ikiwa unataka kumfahamu Sheikh Ilunga tafadhali ingia hapo chini:
Mohamed Said: KIFO CHA SHEIKH ILUNGA HASSAN KAPUNGU NI MSIBA KWA VIJANA

 
mpk leo zanzibar wanatoa shule za mwsho 6/7 ktk top10 za shule zilizofanya vibaya.kusini ndo usiseme huko...21st C bado una na blaming game,hizo hazitawafikisha popote take initiatives...wacha porojo za kkoo huu co wakati wake.
Lukubuzo,
Huijui historia ya elimu ya Zanzibar...
Haya unayoyaona sasa ni matokeo ya Mapinduzi.

Zanzibar ikiongoza Afrika ya Mshariki katika elimu.
In Shaa Allah nitakufahamisha...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…