Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
-
- #121
Luggy,kwa nn hujibu maswali yote?,jibu yote hasa hilo la ugaidi wahusika kuwa na majina ya Kiarabu,je ni sahihi kuwahusisha wao na dini ya Kiislamu kwa sababu ya majina yao?
kinawashinda nini mpaka sasa kujenga shule na vyuo mpaka mkapa alipowafanyia hisani morogoro?Luggy,
Inaelekea hujui historia ya Waislam wa Tanzania.
Ungekuwa unajua usingekuja na kauli hiyo.
Baada ya uhuru Waislam waliitisha Muslim Congress 1962 na 1963 na waliamua kujenga shule nchi nzima na Chuo Kikuu.
Nawaachie wengine wakueleze nini kilitokea.
Lukubuzo,kinawashinda nini mpaka sasa kujenga shule na vyuo mpaka mkapa alipowafanyia hisani morogoro?
Lukubuzo,kinawashinda nini mpaka sasa kujenga shule na vyuo mpaka mkapa alipowafanyia hisani morogoro?
blaming game 21th century?Lukubuzo,
Hatujashindwa kujenga taasisi na laiti ungelijua ukweli usingekuja na maswali haya tena una uliza kwa ufedhuli.
Inaelekea huijui historia ya Waislam na matatizo yaliyowafika.
Historia hii imeandikwa na ukitaka kuijua itabidi usome.
Anza na rejea hizi: Bergen (1981), Sivalon (1992), Njozi (2002).
Ukipenda soma kitabu cha Abdul Sykes (1998).
Rejea hizi zimefungua wengi macho.
alipewa na wakoloni ukikataa unachinjwaHATA KAMA UTAINGIZWA UDINI CHA MSINGI UKWELI UFAHAMIKE ILI KUWEKA SAWA HISTORIA.MIMI PIA NI MGONI NA BABU YAKE NA BABA ALIKUWA NA JINA LA KIISLAM JAPO SIJUI ALILITOA WAPI.
uislam waliupataje kama sio kwa wakoloni wa kiarabuSehemu nyingi wapigania uhuru walikuwa ni waisilamu dhidi ya wakoloni wakiristu.
tumia neno zuri majina ya kiarabu maana kuna waarabu ambao sio waislam na wanamajina kama hayo.Mack...
Hii ndiyo hatari ya kujadili jambo usilolijua.
Hebu soma hapo chini:
''Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.
Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam. Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo. Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona na kuwaona wakubwa wa kituo hicho. Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko.
Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.''
Ikitaka habari zaidi ingia hapo chini:
Mohamed Said: MAREHEMU SHEIKH ILUNGA HASSAN KAPUNGU MAKALA YAKE KUHUSU VITA VYA MAJI MAJI
historia imepindishwa na hao waarabu waliowapa viongozi wetu wa jadi majina yao ya kiarabu ,wakaona majina yetu ya asili ni upuuziSon,
Nilichofanya ni kueleza kuwa historia imepindishwa na hii imefanya ipungue.
Nimeeleza hayo ili kuikamilisha na watu wajue ukweli.
Hili si jambo kukukasirisha labda kama unachomwa na ukweli.
Ikiwa ukweli unakuumiza basi ipo sababu.
Yaani anajifanya ana uchuuuuungu na hayo majina anayoyaita 'Ya Kiislamu' wanafamilia wa hao marehemu. Huyu mzee hajui kuwa Waarabu waliitwa Abdula, Rashid, Muhamad n.k even before Uislam?ndio anaona.cha muhim sana kurithisha watoto. mkuu watu dizain hii wala usihangaike nao maana ndivyo alivyo ni nature yao.
Hapa kwetu Afrika ya mashariki Uisilamu haukuletwa na wakoloni,ila ulitokea uhabeshini ukatiririka mpaka kwetu.huo
uislam waliupataje kama sio kwa wakoloni wa kiarabu
ukatirirka wenyewe tu duh? naona unajaribu kumtetea mwarabu bila mafanikioHapa kwetu Afrika ya mashariki Uisilamu haukuletwa na wakoloni,ila ulitokea uhabeshini ukatiririka mpaka kwetu.
Mfalme Najash baada ya kuwapokea maswahaba na akawaambia wamsomee quran tukufu...bingo' mpaka leo uisilamu raha aisee! Uisilamu wa kikoloni huko zenj ni tofauti (ibadhi) huo haukuenea sana.ukatirirka wenyewe tu duh? naona unajaribu kumtetea mwarabu bila mafanikio
Mwana...Yaani anajifanya ana uchuuuuungu na hayo majina anayoyaita 'Ya Kiislamu' wanafamilia wa hao marehemu. Huyu mzee hajui kuwa Waarabu waliitwa Abdula, Rashid, Muhamad n.k even before Uislam?
Mbili, nawafahamu watu walau wawili wa nasaba ya Kleist Sykes, mmoja ni mwanamuziki anajiita Dully na mwingine ni mhasibu wa kampuni ya Statoil...wote hawa wanatumia jina la Kleist Sykes. Je hawa ubin wao waliusoma kaburini kwa babu yao?
Anapozungumzia WAKOLONI, huyu mdini aso na haya anasahau kuwa hata Waarabu nao walikuwa wakoloni?
fogoh2,historia imepindishwa na hao waarabu waliowapa viongozi wetu wa jadi majina yao ya kiarabu ,wakaona majina yetu ya asili ni upuuzi
MMMwinyikungu,
Ahsante kwa maelezo yako.
Mimi nimeeleza ukweli katika historia kuwa Mkwawa alikuwa na jina lingine
nalo ni Abdallah na alikuwa kaijua kuandika na kusoma kwa irabu za Kiarabu
na alikuwa na urafiki mkubwa na Rumaliza.
Rumaliza jina lake halisi ni Muhammad bin Khalfan bin Khamis al-Barwani.
Nnilijaliwa kukutana na kitukuu cha Rumaliza, Mohamed Said Dubai mwaka
wa 1999 na anajua mengi katika historia ya babu yake mkuu na Mkwawa.
Vitabu vinamwandika kama ''Chief,'' na chief tafasiri yake ni sultani lakini iwe
iwavyo hayo ni majina na vyeo, ukweli wa historia kuhusu maisha yake ndiyo
muhimu.
Tusitishike na historia hizi ambazo wako ambao kwa sababu zao hawakupenda
zijulikane.
Ya wapi matusi kwenye matamshi yangu?Mwana...
Tunaweza tujafanya mjadala wa heshima na staha.
Ukiwa una hasira na kuja na lugha kali za matusi kwangu inakuwa shida kukujibu.
Umewahi kusoma kitabu cha Sivalon?
Angalia hapo chini:
je majina yao halisi ya kiasili ya kiafrika yalibaki?fogoh2,
Uislam una utamaduni wake na ninachozungumza na nimeandika sana si
tatizo la jina kama jina kumtambulisha mtu.
Ninachoandika na kueleza ni kwa nini wanahistoria wamelikwepa hili jina
la Abdulrauf na kuamua kutumia majina yake mengine ya Songea Mbano.
Nikaeleza kwa nini wale majemadari walionyongwa na Wajerumani majina
yao ya Kiislam yamefutwa?
uislam ibadh wa kikoloni uliasisiwa na mtume gani?Mfalme Najash baada ya kuwapokea maswahaba na akawaambia wamsomee quran tukufu...bingo' mpaka leo uisilamu raha aisee! Uisilamu wa kikoloni huko zenj ni tofauti (ibadhi) huo haukuenea sana.
Lukubuzyo,blaming game 21th century?
ilunga kafa akilalamika tu hajafanya 'initiatives' zozote.wewe pia umebaki kulaumu tokea uhuru mpaka sasa.Umechukua hatua gani kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya elimu?
mliitwa dodoma na jk2 na mkaulizwa mnataka nini?,bakwata mkataka tende nyingi wakayi wa mfungo na majamvi.
wewe unajinasibu sio bakwata,haya hizo taasisi nyingine unazozikubali zimefanya nini?,utasikia tulitaka kujiunga na oic,mara gadafi alitaka kujenga zikatokea figisu.
nyinyi mmechukua jukumu gani? hizi blaming games hazitawafakisha popote.